Wazenji wafurika viwanja vya lumumba(muungano usio na ridha ni jinamizi lisilo kubaduka) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wazenji wafurika viwanja vya lumumba(muungano usio na ridha ni jinamizi lisilo kubaduka)

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by abdulahsaf, May 1, 2012.

 1. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #1
  May 1, 2012
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  [h=3][/h]

  [​IMG]
  Mwanasheria Maarufu Zanzibar, Salum Tawfiq akitoa mada katika Kongamano la Kitaifa kuhusu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar katika viwanja vya Lumumba Mjini Zanzibar
  [​IMG]
  Wazanzibari waliofurika katika viwanja vya Lumumba katika kongamano lililozungumzia Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambapo watu kadhaa walitoa uzoefu wao wa maisha ndani ya Muungano


  Mimi naamini kabisa kwamba Muungano ni ridhaa baina ya Nchi mbili zilizoungana. Muungano wa Serikali mbili au viongozi wawili bila ya baraka za watu wa nchi hizo hauna maana yoyote. Hivyo iwapo upande mmoja katika Muungano utasita kuridhia kubaki katika Muungano, huo unakuwa si Muungano tena. Sasa leo ya nini kuunda Tume na kupoteza mabilioni ya fedha kujaribu kuutenganeza upya Muungano ambao tayari viashiria vyote vinaonesha Muungano ushapitwa na wakati. Si ungetosha tu kuwauliza Watanzania suala la msingi kwanza kabla ya kuingia katika gharama zisizo za lazima. Suala lenyewe: jee unautaka au huutaki? Kungekuwa na haja gani ya kutaka Muungano uwe madhubuti kama walio wengi hawautaki?
  UTATUZI WA KUDUMU WA KERO ZA MUUNGANO
  Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambao juzi tu ulitimiza miaka 48 umejaa kero ambazo kila upande, hasa Zanzibar, unaona zimekua karaha. Muungano huu na kero zimekuwa ni vitu vinavyokwenda pamoja – huwezi kuzungumzia Muungano bila ya kuanza kutaja mapungufu yake. Katika mada hii, nitajaribu kupendekeza namna ambavyo kero hizi tunaweza kuzitatua.Mwalimu Nyerere akihojiwa na Gazeti la Observer la Uingereza tarehe 18 Aprili 1968 alisema:Kama ni Rais wa Tanzania, ni jukumu langu kulinda kuwepo kwa Jamhuri ya Muungano. Lakini iwapo umma wa Wazanzibari, bila ya kutumiwa na wageni, wakiwa na sababu zao binafsi, wakaona kuwa Muungano hauna maslahi kwao, sitoweza kuwalazimisha kubaki katika Muungano. Muungano utakuwa tayari umesita kuwepo endapo upande mmoja utaondoa ridhaa yake. (Tafsiri ni yangu).Nukuu hiyo ndio chimbuko la mada yangu. Katika harakati au wasemavyo siku hizi “mchakato” wa kupitishwa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya Mwaka 2011, Wazanzibari wameonesha wazi kwamba wamechoshwa na Muungano uliopo sasa. Wazanzibari walio wengi pamoja na viongozi wao, wakiwemo Mawaziri na viongozi wa dini, wamesema waziwazi kwamba Muungano huu wa miaka 48 hauna maslahi kwao. Na “Baba wa Taifa” alishaota ndoto hio; leo kero za Muungano zinaonekana zaidi kwa ndugu mdogo (Small Brother) kuliko kwa kaka mkubwa (Big Brother).Wapo baadhi ya Watanganyika ambao nao wamekuwa wakidai Tanganyika yao lakini hawa ni katika wachache. Waliowengi, kuwepo au kutokuwepo kwa Zanzibar katika Muungano hakuathiri chochote kwao. Hawa wanaona ukubwa wa ardhi, idadi ya watu na rasilmali nyingi walonazo zinaitoa Zanzibar kama mshiriki mwenza (equal partner) katika Muungano. Hili likichanganyika na “kero ya Wazanzibari” kila siku kufanya kelele linawafanya waone Muungano hauna maana tena kwa Tanzania.Wapo Watanganyika wengine wanaona Zanzibar “haina shukrani” kwa kuwa ati Zanzibar inategemea kila kitu – kuanzia chakula, nguvu kazi na hata fedha za kuendeshea nchi kutoka Bara. Hawa ndio wengi wanaosema Muungano unawanufaisha zaidi Wazanzibari na itakuwa ni kujitia kitanzi iwapo Zanzibar itajitowa katika Muungano.
  Tabaan. Kwa wote hawa basi na warudi wenyewe kwa Mwalimu Nyerere. Sasa Zanzibar na Wazanzibari washaridhika kwamba Muungano umewachosha. Kuna haja gani ya kuunda Tume ya Katiba kukusanya maoni ya wananchi?Sheria ya kuanzisha Tume ya Katiba imeweka hadidu za rejea au muongozo kwa Tume hiyo ambayo inategemewa kuanza rasmi kazi yake mwanzo wa mwezi wa Mei, 2012. Hadidu rejea hizi zimetajwa katika kifungu cha 8, 9 na 17 vya Sheria hiyo (Nam. 8 ya 2011). Baadhi ya majukumu yake ni:
  Kukusanya maoni ya wananchi Kutoa mapendekezo kwa kila hadidu rejea
  Kutayarisha na kuwasilisha ripoti kwa kuzingatia hadidu rejea. Agenda kubwa kwa Wazanzibari ambayo ni suala la kuwepo au kutokuwepo kwa Muungano si miongoni mwa hadidu rejea za Tume ya Katiba. Na wakati wa kuapishwa kwa Wajumbe wa Tume Ikulu Dar es Salaam tarehe 13 Aprili 2012, Rais Kikwete alisema wazi kwamba wanaohubiri kuvunjika kwa Muungano hawatasikilizwa! Mtu ataweza kujiuliza: nini sasa faida ya kukusanya maoni kama kiini cha matatizo hutaki kijadiliwe? Katika kulijadili hili naomba tukakisome tena kitabu cha Baraza la Katiba, Zanzibar:Katiba Tuitakayo – Sheria ya Kuandika Katiba Mpya ya Tanzania na Suala la Muungano kwa Zanzibar, hususan Sura ya Nne (Uk.22 – 29).
  Maana yake ni kwamba kwa mujibu wa Sheria ya Tume, hata kama Wazanzibari asilimia 100 wakisema wamechoshwa na Muungano hawatasikilizwa! Hapa ndio udhaifu mkubwa wa Sheria ya Tume unapoonekana. Nini hasa faida ya kuunda Tume na kutumia zaidi ya bilioni 40 na kumalizia kwa kuongeza tu katika orodha ya kero za Muungano?Napenda hapa niunganishe hili la kuundwa kwa Tume ya Katiba na kupitishwa kwa Marekebisho ya 10 ya Katiba ya Zanzibar (Sheria Nam. 9/2010). Marekebisho haya yameingiza vifungu vingi ambavyo kwa maumbile yake vinaonekana vikisisitiza Utaifa (Nationhood) wa Zanzibar. Kifungu cha 1 kinasema:Zanzibar ni Nchi ambayo eneo la mipaka yake ni eneo lote la visiwa vya Unguja na Pemba pamoja na visiwa vidogo vilivyoizunguka na bahari yake ambayo kabla ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ikiitwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar.Kifungu cha 2A nacho kimetowa mamlaka kwa Rais wa Zanzibar kuigawa Zanzibar katika mikoa, wilaya na maeneo mengineyo. Pia viko vifungu vyengine vinavyoonesha dhahir kujibu kejeli ya kaka zetu wakubwa kwamba Zanzibar ni mkoa tu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tunafahamu jinsi mara kadhaa wanasiasa wa Tanzania Bara na hata Mahkama ya juu kabisa ya Tanzania (Mahkama ya Rufaa) walivyosisitiza kwamba Zanzibar si Nchi. Kwa maana hiyo hata ukifanya njama ya kutaka kumuondoa Rais wa Zanzibar madarakani kwa mtutu wa bunduki, hiyo haitokuwa uhaini (treason).Ni sawa sawa na kujaribu kuiondosha Halmashauri ya Mji wa Chake Chake, si jambo la kushtua!Mimi naamini kabisa kitendo cha Baraza la Wawakilishi kupitisha Marekebisho hayo kimekuja katika wakati muwafaka kabisa. Unapokuwa na mwenzako ambae hafahamu lugha unayozungumza inabidi utafute lugha pekee atakayoifahamu. Kubadilisha Katiba imekuwa lugha muwafaka kuwafanya wenzetu waone nini tunataka. Marekebisho ya Katiba yameibua lawama tele kutoka kwa wanasiasa na hata miongoni mwa wanasheria mahiri wa Tanzania Bara. Wengine wamesema Muungano wa Tanzania haupo tena pale Zanzibar ilipojitangaza kuwa ni Nchi! Mie naziona hizi zote ni kelele za mlango tu.Kwa upande mwengine naamini Marekebisho ya Katiba ya Zanzibar ya 2010 pamoja na kuwepo kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (GNU) ndiko kulikopelekea kaka zetu wakubwa kuleta kiini macho cha Tume ya Katiba. Kama kweli lengo la Tume ni kushughulikia kero za Muungano na kuufanya Muungano wetu kuwa madhubuti basi hilo lilipaswa kufanywa zamani sana, pale kelele za Wazanzibari na hata za makundi kama G 55 ya Tanzania Bara yalipoibuka kudai Serikali ya Tanganyika na ya Zanzibar.
  Badala yake hali ya kisiasa ikawachwa kuwa tete. Waliokosoa Muungano wakaitwa wasaliti wasioitakia mema Tanzania. Kuunda Tume ya Katiba sasa hivi ni sawa na kujaribu kuyazuia maji ya bahari yasifike ufukweni wakati wa bamvua!Suala la kuwepo au kutukuwepo kwa Muungano ndio suala la msingi hata kabla ya kuunda Tume. Hapa Zanzibar tunayo Sheria ya Kura ya Maoni, 2010. Bara hawana, lakini hilo haliathiri chochote. Kama alivyonukuliwa Nyerere mwanzoni mwa mada hii;Muungano hauwezi kuwepo endapo upande mmoja utaukutaa. Cha msingi ni kulipeleka suala hili kwa wananchi wenyewe walitolee uamuzi. Kwani viongozi wanahofu ya kitu gani? Isije ikatufika hadithi ya Abunuwasi ya kuwekwa uchi halafu tukaamini hatuonekani!Mimi naamini kabisa kwamba Muungano ni ridhaa baina ya Nchi mbili zilizoungana. Muungano wa Serikali mbili au viongozi wawili bila ya baraka za watu wa nchi hizo hauna maana yoyote. Hivyo iwapo upande mmoja katika Muungano utasita kuridhia kubaki katika Muungano, huo unakuwa si Muungano tena. Sasa leo ya nini kuunda Tume na kupoteza mabilioni ya fedha kujaribu kuutenganeza upya Muungano ambao tayari viashiria vyote vinaonesha Muungano ushapitwa na wakati. Si ungetosha tu kuwauliza Watanzania suala la msingi kwanza kabla ya kuingia katika gharama zisizo za lazima. Suala lenyewe: jee unautaka au huutaki? Kungekuwa na haja gani ya kutaka Muungano uwe madhubuti kama walio wengi hawautaki?Kwa mawazo yangu endapo Wazanzibari watasema hawautaki Muungano, dawa iliyobaki ni moja tu nayo ni kumaliza taratibu mambo ya Muungano. Udugu wa watu wetu na mahusiano ya kidiplomasia yatandelea. Marehemu Karume aliunasibisha Muungano na koti: likikubana utalivua tu. Nadhani koti la Muungano limekuwa linawabana sana Wazanzibari na lililobaki ni kulivua tu. Tukingoja sana itabidi tulichane kwani litashindwa kuvuka!
  Ahsanteni Sana
  Imetayarishwa na:
  Salum Toufiq, Wakili
  (Mada iliyotolewa katika Kongomano lililofanyika Lumumba tarehe 01 Mei 2012)

  www.mzalendo
   
 2. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #2
  May 1, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,401
  Trophy Points: 280
  1.Wazanzibar wakijitenga hasa kwa ulevi wa madaraka dhambi ya ubaguzi itawatafuna
  2.Wazanzibar hawana tofauti na makaburu coz ya ubaguzi sitawaonea haya hata kidogo ni makaburu tu.
  3.Nchi ye2 imekumbwa na ufa wa kwanza ni wa muungano,wazanzibar hawaelewi kwamba nje ya muungano hakuna wazanzibar
  4.Wazanzibar wakijitenga 2nawakatia umeme,2nawafukuza wote huku bara vunja maduka yao yote na 2nachukua nyumba zao na hakuna mpemba au muunguja(nje ya union hakuna waznzbri) atakayeomba uraia wa jamhuri ya tanzania.
   
 3. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #3
  May 1, 2012
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kwa nini Watanganyika hamuna harakati za kurudisha historia ya nchi yenu muliopigania uhuru 1961 Tanganyika kabla mambo hayajawa mabaya sana?.

  Hakuna shaka kuwa Wazanzibar hivi sasa hawana hamu na Muungano na wanaweza kuvunja wakati wowote, hii sio siri mambo yako wazi sasa , zamani ilikuwa Muungano unasimamiwa baina ya Dodoma na Kiswanduwi Zanzibar.

  Lakini hivi sasa hata hata huko Kiswanduwi makao makuu ya ccm Zanzibar kumeanza vuguvugu la kujigawa viongozi kuna wenye kutaka Serekali kuendelea na Serekali 2 na kuna wenye kutaka 3 na kuna wenye kungana mkono na Wananchi wengi wa Zanzibar wenyekusema Zote zimeshapitwa na wakati sasa nikuvunja tu kwa vile uongo na viraka vimekuwa vingi.

  Wazanzibar wanasema kuwa kujadili katiba nikupoteza muda na pesa za umma , muhimu chakujadiliwa ilikuwa ni Muungano kwa vile Muungano ndio wenye madatizo mengi ya kisheria na katiba ndio imezaliwa na Muungano.

  Lakini kutokana na ukinzi na ukaidi wa Viongozi wa ccm imekuwa kakilipiga chenga chambo hili na kujifanya hamunazo lakini hivi sasa kasi ya Wazanzibar nikubwa kuliko harakati za kisiasa.

  Wazanzibar wameungana na kuwacha muelekeo wao wa kisiasa na kudai nchi kwanza siasa badae, na hali hii imekuwa ikisimamiwa na tasisi na jumuia mbalimbali Zanzibar ikiwemo jumuia za Wanasheria,Dini, na NGO nyengine za kibinafsi.

  Bada ya serekali kuwa wakaidi sasa huenda wakakosa yote kwa vile nguvu ya Wazanzibar nikubwa na nitabu kuizuia kisiasa hivi sasa, sababu nyingi kuhusu kasoro za Muungano ndio zilizo wafikisha hapa leo na kuona kuwa Muungano hauna maslahi yoyote ispokuwa kwa chama cha mafisadi ccm.
   
 4. Puppy

  Puppy JF-Expert Member

  #4
  May 1, 2012
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 2,268
  Likes Received: 653
  Trophy Points: 280
  mimi pia siupendi muungano. fanyeni haraka kuuvunja
   
 5. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #5
  May 1, 2012
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ndugu yangu zungumza vitu vya msingi usizungumze utumbo na uoza, wewe mwenyewe huumii kumezwa nchi yako Tanganyika ulioipigania uhuru na historia yako kwa itikati za chama cha mafisadi?.

  Sizani kuwa utawatisha Wazanzibar kuwa uvunjikapo Muungano utawafukuza na kuvunja maduka kwa sababu tu eti wame vunja muungano, hii itaonyesha ile tamaa ya ujambazi, wazanzibar wataondoka salama na hayo maduka na yumba zitabakia huko huko.

  Lakini ujuwe tu kuwa warisi wa maduka na majumba itakuwa ni wachina na wa south africa , wazanzibar hawako Tanganyika tu, wako kila nchi na wana maduka na majumba sio Tanganyika tu , wako Bara arab,europ na nchi ntingine.

  Mimi nakuliza kwani bila ya Wazanzibar hamuwezi kuichi ndani ya nchi yenu bila ya wazanzibar?, mbona unakuwa mkali kwa kusema wazanzibar wanataka kujitenga hofu yako nini? kabla ya Muungano ulikuwa unaishi vipi?.
   
 6. nxon

  nxon JF-Expert Member

  #6
  May 1, 2012
  Joined: Jul 16, 2011
  Messages: 1,149
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  bora uvunjike afu tuone maanake wanapiga sana kelele
   
 7. dosama

  dosama JF-Expert Member

  #7
  May 1, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 786
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Nyie tumeshawachoka kila siku mnaweka makongamano ya kukataa muungano si mvunje bwana. Mnalia kila siku kama vipi mwanaume hakuandikii taraka jiandikie then atasaini kuridhia.

  Na msisahau kuwachukua na ndugu zenu walioko huku bara na mkizaliana kama kawaida yenu muhishie hukohuko
   
 8. B

  Bob G JF Bronze Member

  #8
  May 1, 2012
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 2,354
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Hofu ya Rais kulazimisha watu wasitoe maoni yao kuwepo ama kutokuwepo kwa muungani ni hofu ya kuogopa historia kuwa muungano ulivunjika ktk utawala wake. na hofu hii ni dhaifu coz huwezi kuwazuia watu kuamua hitima ya maisha yao ktk muungano na hii itasababisha tume ya kukusanya maoni ya katiba kupigwa mawe tena zanzibar na endup yake utakua ni mgogoro na machafuko. Rai yangu waruhusu kura ya maoni ya kuamua hitima ya muungano, tupige kura na waiache demokrasia ifanye kazi, NI KWELI KOTI LIKIKUBANA UNALIVUA haina ubishi, MUUNGANO SI NDOA YA KIKRISTO kwamba haiwezi kuvunjika. Na kwakuzuia watu kusema NIKUCHOCHEA VURUGU NA MACHAFUKO YATAKAYO GHARIMU MAISHA YA WATU
   
 9. PENDING'ULA

  PENDING'ULA JF-Expert Member

  #9
  May 1, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 269
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wazanzibari ni watu wenye maamuzi yao. Ikiwa wao wanadhani muungano hawautaki,Achaneni nao! Wanakoelekea kunajulikana, acheni waende. Niwajuavyo mimi mkiwaendekeza hamtakuwa na lakufanya jingine la maana ila kuzungumzia Muungano! Wao kila wakati wanahitaji kuwa na jambo la kuumiza vichwa! Pamoja na faida zote zilizopo kama wao hawaoni acha waende! Tutaonana kwenye vikao vya usuluhishi! Watu wa Bara tuna mambo ya muhimu ya kuyashughulikia, kuliko kukaa na kujadili mambo yasiyo na tija! Kuwe na Serikali kumi, moja , saba, nk kama hatutafanya kazi kwa kujituma, na badala yake tukadhani tutapata misaada kutoka katika jumuia zinazotoa misaada kama rafiki zetu wanavyodhani tutabaki malofa tu!
   
 10. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #10
  May 1, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 18,520
  Likes Received: 10,438
  Trophy Points: 280
  muungano ukivunjika zanzibar kitakua kituo cha kuzalishia magaidi.!!
   
 11. PENDING'ULA

  PENDING'ULA JF-Expert Member

  #11
  May 1, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 269
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hiyo jazba ni proparty ya wenzetu, mnataka mitazamo yenu kila mtu aunge mkono! Kuna ukweli katika baadhi ya madai yenu, lakini mengi ni ya kilevi tu. Nawasihi tumieni "NGUVU YA HOJA NA WALA SI HOJA YA NGUVU". Msijione very special, kwamba mkiondoka kuna watakaokufa njaa, bali hii ni historia tu. Kumbukeni talaka inaweza kutolewa na yeyote katika wanandoa, kama umechoka toa talaka, SEPA!
   
 12. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #12
  May 1, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,799
  Trophy Points: 280
  Eeeh! wanaonekana wako serious! ngoja tuone itakuaje, wakijitenga tuishawishi zaire tuungane nayo ili jina libakie hili hili (TANZANIA)sijakosea, namaanisha tuwashawishi warudishe kwanza jina la zairwaaa, ili mambo yajipe. Naamini itakuwa byeeeee bandugu.
   
 13. PENDING'ULA

  PENDING'ULA JF-Expert Member

  #13
  May 1, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 269
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama kuna wenye akili timamu za kutambua uzito wa mambo hayo, watagundua kwamba jambo la muungano peke yake ni mjadala mkubwa, ukichanganya katiba na Muungano, utaichanganya kamati. Kama unaona huo ni uoga mshaurini rais wenu mwenye ujasiri aunde kamati ya kuratibu maoni huko kwenu ili mvunje Muungano.
   
 14. Y

  Yasser5 JF-Expert Member

  #14
  May 2, 2012
  Joined: Mar 15, 2012
  Messages: 207
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Muungano anao ccm na nyinyi hamtaki kuachana na sisiem tuwafanyeje endeleeni mijadala yenu
   
 15. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #15
  May 2, 2012
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,073
  Likes Received: 1,806
  Trophy Points: 280
  we idawa kwanini unasema hivo...?!
   
 16. MD25

  MD25 JF-Expert Member

  #16
  May 2, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 3,078
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Hili swala la muungano ni bomu linalongojea kulipuka...
   
 17. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #17
  May 2, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,552
  Likes Received: 18,231
  Trophy Points: 280
  Wanabodi,

  Nijuavyo mimi, Tanzania ni taifa moja (One Nation) ambayo ndani yake kuna Zanzibar state!.

  Kitendo cha kujadili kuuvunja muungano ni kujadili kuivunja nchi na huu ni "Uhaini"!.

  Kinachoweza kujadilika ni kuuboresha muungano wetu adhimu na sio kuuvunja!.

  Hata hivyo endeleeni kujifurahisha kwa kujadili kuuvunja muungano!, mtajadili wee, mtajadili wee mchana lakini usiku mtalala na siku itapita!.

  Ni busara kujadili ni muungano wa aina gani ndio mngeutaka ili kuuimarisha na sio kujadili kuuvunja!.
   
 18. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #18
  May 2, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,867
  Likes Received: 6,220
  Trophy Points: 280
  Pasco

  ni vyema ukawaamnia maneno hayo wapemba na waunguja maana ndo wanaofanya chokochoko za muungano. Na kama wakiamua kujitoa mtawafunga kamba?

  Wao ni watu wazima wacha wafanye maamuzi, afterall we've got nothing to loose, acha wapelekeshwe na wenye uchu wa madaraka......
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 19. d

  dandabo JF-Expert Member

  #19
  May 2, 2012
  Joined: Feb 18, 2012
  Messages: 303
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 45
  Nawahurumia wazenj!, hasa wale masikini wenzangu tunaoponea kwa majahazi ya ruti za pemba-Tanga! wakati wakomoro wakitamani kuwa sehemu ya tz, hawa bandugu wanataka kutimua!
   
 20. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #20
  May 2, 2012
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,224
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  Abdulahsaf; mbona unatumia nguvu nyingi kwenye keyboard kujaribu kuwalazimisha watanganyika kuukataa muungano?, watanganyika wanawaomea huruma nyie wazanzibara kwa kuwa bila muungano mutaishi maisha ya taabu, hamjiwezi kwa lolote, nyie mwaishi kama viwete, wewe mwenyewe waishi bara na jukwaa lako la kukuliwaza ni JF"la bara", tukikufukuza humu JF wewe utapata kwashakoo. Acha chokochoko zako za kijinga.
   
Loading...