Wazenji waamka na sasa si kulala tena.Kikwete hana tofauti na wengine.

Mwiba

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
7,607
1,744
KUMBUKUMBU ZA MKUTANO WA WAZANZIBARI HUKO LONDON UTANGULIZI:Mkutano wa Wazanzibari wanaoishi nchi za Ulaya ulifanyika tarehe 22 March, 2008 katika jiji la London kuanzia saa 8.00 mchana hadi saa 1.00 usiku kwenye ukumbi wa Durning Hall hapo Forest gate. WASHIRIKI:Kwenye mkutano wa hapo juu palikutanishwa Wazanzibari kutoka sehemu mbali mbali za Ulaya kwa madhumuni ya kuitikia kilio cha Wazanzibari Ulimwenguni kote dhidi ya uporwaji wa mamlaka ya nchi na utawala wa Zanzibar. YALIYOZUNGUMZWA:Katika Mkutano huo daraja za maendeleo mbali mbali zilizofikiwa na Zanzibar kabla ya Muungano zilitajwa kama vile: ·
Zanzibar ilikuwa nchi, dola na taifa huru kabla hata jina la nchi ya Tanganyika kujulikana.
· Zanzibar ilikuwa nchi moja baina ya nchi mbili katika Bara la Afrika kwa kuwa na watalamu wengi zaidi.
· Kufananisha na idadi ya wakaazi Zanzibar ilikuwa nchi ya tatu Afrika kwa mujibu wa kipato cha kichwa.
· Zanzibar ni nchi ya mwanzo Afrika kuwa na gari la moshi.
· Zanzibar ilikuwa nchi ya mwanzo Afrika kuwa na simu ya upepo. · Zanzibar ilikuwa na taa za umeme barabarani kabla London na New York. ·
Zanzibar ilikuwa na lifti kabla ya nchi yeyote Afrika ya Mashariki.
· Zanzibar ilikuwa na akiba ya fedha za kigeni kubwa zaidi kushinda nchi yeyote Afrika ya Mashariki. Kimaendeleo/kiuchumi leo Zanzibar iko nyuma ya nchi zote katika Afrika ya Mashariki. · Kisiasa Raisi wa Zanzibar ni sawa na Waziri mdogo katika Baraza la Mawaziri la Muungano. Baraza la Wakilishi la Zanzibar na maamuzi yake hayavuki Chumbe. Mawaziri wa Zanzibar wako chini ya Wakuu wa Wilaya wa Muungano. Wabunge wa Zanzibar katika Bunge la Muungano hawawashi wala hawazimi. Zanzibar katika Katiba ya Muungano wa nchi mbili haijahakikishiwa Urais wa zamu. · Zanzibar ina matufa na sasa serikali ya Muungano inataka kuyanyakuwa na kuyageuza mali ya Muungano suala ambalo halimo katika katiba ya Muungano na wakati huo huo Madini ya Bara yamekuwa mali ya Bara.
· Zanzibar imepoteza wanasiasa wake waliosoma ama kwa kuhamishiwa Bara au kutawanya sehemu mbali mbali ulimwenguni, · Wataalamu wa Zanzibar walilazimishwa kukimbia nchi kwa makusudi na kuidhoofisha Zanzibar wakati serikali ya Muungano ikifumbia macho ·
Zanzibar imepoteza roho za Wanasiasa wa juu kwa mbinu za Muungano ·
Zanzibar imeshuhudia wanasiasa mashuhuri wa kizanzibari kufungwa katika magereza ya serikali ya Muungano kufikia miaka 6 hadi miaka 10. Kwa udhalimu wa aina hii serikali ya Muungano inabidi ishitakiwe na kulipa fidia za waliouwawa na waliofungwa bila ya hatia.
· Zanzibar chini ya Muungano imepoteza utaifa wake. · Zanzibar imepoteza Kiti chake cha Umoja wa Mataifa.
· Zanzibar imepoteza umashuhuri wake wa kibiashara kwa kuwekewa vizingiti vya kila aina. ·
Vipengele vya Katiba ya Muungano vimezidishwa kuikandamiza Zanzibar Kisiasa, Kiuchumi, Kitamaduni, Kijamii (elimu na siha) na hata Kidini. Hali mbaya ya Zanzibar unawaathir zaidi hali za Vijana,Watoto, Wanawake na kusababisha umasikini wa kutupwa. Mkutano ulitambua kwamba hali hii imewezekana kwa sababu Wazanzibari hawajaungana na wameshughulishwa zaidi na kupigana vita wenyewe kwa wenyewe na kusahau mustakbal wa Taifa la Zanzibar. Mkutano umeona kuna haja kubwa na muhimu sana ya kuwaunganisha Wazanzibari wote katika mapambano ya kupigania maslahi ya Zanzibar.
Imependekezwa kwamba kila mrengo wa kisiasa uweke mustakbal wa Taifa la Zanzibar mbele na siasa binafsi baadae. Ni pale tu ambapo Wazanzibari wataungana bila ya kujali mirengo ndipo Taifa la Zanzibar litakapo okoka. MAPENDEKEZO:Ili kuweza kufanya hivyo imependekezwa kufanyike Mkutano Jijini London baina ya tarehe 12-16.12.08 na kualika Wataalamu wa Kizanzibari ambao watashiriki katika kongamano la kulijadili suala la Utaifa wa Zanzibar, kusherehekea Uhuru wa Zanzibar kama Tanganyika wanavyosherehekea wao, kusherehekea kuingia Zanzibar katika Umoja wa Mataifa (16.12.63). Wataalam hao Wakizanzibari watatarajiwa kutayarisha maandishi ya kutetea Utaifa wa Zanzibar katika kila meddani. Kamati ya muda ya Chombo hichi kitawasiliana na Wataalamu hao mbali mbali. MAAZIMIO YA MKUTANO:Mkutano ulipitisha Maazimio yafuatayo.
Mkutano unaazimia
1. Kuunganisha Wazanzibari
2. Kulinda na Kughushisha Taifa la Zanzibar
3.. Kuziunganisha jumuia za Wazanzibari
4. Kuunda NGO za kusaidia Wazanzibari
5. Kupigania Haki za Kitaifa, Kidemokrasia na Kibinaadam za Wazanzibari
6. Kushirikiana na Mashirika ya Kimataifa kutetea Mustakbal wa Zanzibar
7. Kushirikiana na Green Peace kulinda mandhar ya Zanzibar
 
Yaani huyo Kikwete ndiyo wanaqmshtukia leo? Bora awape hiyo referrendum tu halafu ikitoka 49%-51% iwe stalemate all over again.

Im interested in some of the details, may be trivial but interesting.

Kwa hiyo Zanzibar kulikuwa na streetlights kabla ya 1887 siyo?
 
Back
Top Bottom