Wazee Yanga: Uonevu ukiendelea dhidi ya Yanga SC tutakwenda mahakamani kusitisha Ligi

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Siku moja baada ya Klabu ya Yanga kufanya mkutano na waandishi wa vyombo vya habari, wakieleza malalamiko yao kuhusu uendeshaji wa Ligi Kuu Tanzania NBC Premier League.

Leo February 9, 2022 Wazee wa Klabu hiyo wamefanya mkutano na waandishi wa habari, kusisitiza kwamba wameandika barua ya kuomba kukutana na Mh Rais Samia Suluhu Hassan kuwenda kuishitaki maovu ya TFF.

Wazee wamesema kuwa wamechoshwa na mwenendo wa waamuzi wanaochezesha Ligi Kuu Tanzania (NBC Premier League) na wanataka mpira uchezeshwe kwa misingi ya haki na kuacha uonevu.

Pia wamesema uonevu ukiendelea dhidi ya Yanga SC, basi watakwenda mahakamani kusitisha Ligi Kuu Tanzania huku wakidai kwamba kama kuna bingwa ameandaliwa, apewe kombe kisha wao waendelee na mambo mengine.
 
Kwangu yeyote anayetangaza upopoma wa Waamuzi wa Tanzania namuunga mkono. Nchi ina waamuzi zaidi ya 150 wa daraja la Kwanza lakini Cameroon kaenda mmoja tena kazi yake kuinua vibao vya kubadilisha Wachezaji na kuonesha Muda wa nyongeza!
 
Wanasimba wote naomba tuwafariji wana Yanga maana toka GSM afurumushwe wana wasiwasi sana na hata ofisini kwao hawakai. Mm leo nilienda ofisi eti mapokezi hakuna mtu na kwa hali ilivyomtaani sio mda makundi ya waasi yatongezeka ADF,M23,Y23 n.k.
 
Kwangu yeyote anayetangaza upopoma wa Waamuzi wa Tanzania namuunga mkono. Nchi ina waamuzi zaidi ya 150 wa daraja la Kwanza lakini Cameroon kaenda mmoja tena kazi yake kuinua vibao vya kubadilisha Wachezaji na kuonesha Muda wa nyongeza!!
Haya malalamiko kwa waamuzi hayawezi kuisha isipokuwa yatapungua tu..Cameroon ulikotaja yalikuwepo maamuzi yaliyo umiza timu na kunifaika timu nyingine, ambapo akina Sikazwe kumaliza mchezo kabla ya wakati dakika 85 akarudia tena 89 kumaliza mchezo na bila hata dakika za nyongeza.

VAR, Ulaya inatumika mno lakini bado malalamiko yapo..!
 
Haya malalamiko kwa waamuzi hayawezi kuisha ipokuwa yatapungua tu..Cameroon ulikotaja yalikuwepo maamuzi yaliyo umiza timu na kunifaika timu nyingine, ambapo akina Sikazwe kumaliza mchezo kabla ya wakati dakika 85 akarudia tena 89 kumaliza mchezo na bila hata dakika za nyongeza.

VAR, Ulaya inatumika mno lakini bado malalamiko yapo..!
Sijawahi kuona mwamuzi anaboronga halafu watu wanazuiwa kulalamika. Huu utaratibu wa Wenye maamuzi kuboronga lakini watu wakilalamika wanakejeliwa ni Aina mpya ya Udikiteta wa kisoka?
 
kesho wabibi wa Yanga nao wataitisha press🤪

FB5B0C04-3B26-4164-91E6-674E92610789.png
 
Wamwtumwa na GSM kututoa kwenye reli, ya kuvunja mkataba,sasa ni rasmi ndoa ya GSM na utopolo imekufa rasmi,wazee wa yanga=wachawi wa yanga,
 
Kumbe kweli Yanga ni kusanyiko la vilaza si vijana si wazee,nani kawadanganya kuwa mambo ya mpira yanamalizwa mahakamani? Yaani Rais aache shughuli zake asikilize jopo la wachawi wa Utopolo?
 
Back
Top Bottom