Wazee wote kulipwa pesa ya kujikimu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wazee wote kulipwa pesa ya kujikimu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Luteni, Jul 1, 2010.

 1. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #1
  Jul 1, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Serikali iko katika hatua za mwisho kutekeleza majaribio ya mpango wa pensheni kwa wazee wote nchini wenye umri wa kuanzia miaka 60 na kuendelea bila kujali kuwa walikuwa watumishi serikalini au la ili kuwazesha kujikimu mahitaji yao muhimu ya kila siku.

  Tanzania inakadiriwa kuwa na wazee wapatao milioni mbili ambayo ni sawa na asilimia nne ya wananchi wote.

  My take: Nakumbuka miaka ya 70s na mwanzoni mwa 80 kulikuwa na nyumba za kulelea wazee mfano pale Mwanza Community Centre eneo la Mviringo kulikuwa na nyumba ambapo wazee walikuwa wakihudumiwa na serikali sijui mpango huo uliishia wapi.

  Serikali imekuja na mpango mzuri inaonesha imewakumbuka wazee wake lakini je utakuwa endelevu au ni mradi wa wajanja?
   
 2. D

  DoubleOSeven JF-Expert Member

  #2
  Jul 1, 2010
  Joined: Jul 5, 2008
  Messages: 661
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  ...... hii kali. Sikukuu ingine ya wajinga Wadanganyika yaja October 2010 na haiko mbali. Mtasikia upuuzi wa kila aina. Just for starters, mwendawazimu aliyetamka haya maneno anajua IDENTITY ya wazee anaozungumzia? Wadanganyika wengine wanaishi kwenye mashimo sehemu flani nchini na inawezekana hata kwenye miti. Uendeshaji wa mamabo mengi umewashinda. Usanii wanaweza. Atakayegawa kura with such silly hopes has to be equally silly!
   
 3. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #3
  Jul 1, 2010
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,933
  Likes Received: 2,085
  Trophy Points: 280
  Kila kitu sasa hivi ni 'hatua za mwisho'! Baada ya October 2010 tutaambiwa majaribio hayajaonesha mafanikio! Wale wazee wa EA mpaka leo wamesahaulika kutokana na siasa hizi mbofumbofu!
   
 4. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #4
  Jul 1, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Tutasikia mengi mwaka huu, i like this season!!
   
 5. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #5
  Jul 1, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Kweli, kwa nini serikali isiwalipe kwanza wazee wa EA malimbikizo yao ndipo ije na mpango huu au ni danganya toto ya uchaguzi?
   
 6. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #6
  Jul 1, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Mwaka wa uchaguzi huu...si bongo flava tu hata NGO nazo zinawapigia debe. arkhhhhhhhhhhh!!!!!!!!!
   
 7. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #7
  Jul 1, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Mbali ya kutokuwa na permanent address nani atahakiki umri wao maana wengine wanachokumbuka ni kuwa walizaliwa wakati wa njaa kali au wakati wa nzige, labda tusubiri ID za Masha zinaweza kusaidia.
   
 8. b

  blackpepper JF-Expert Member

  #8
  Jul 1, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 382
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  miaka mitano iliyopita waliingia na gia ya Mahakama ya Kadhi....waislam wakaingia mkenge wakamwaga KURA sasa wamewakalia vibaya so wamekuja na gia ya kuwalipa wazee pesa ya kujikimu.CCM kwa Usanii kiboko
   
 9. A

  ALLY KILUNGUZO SALUM Member

  #9
  Jul 1, 2010
  Joined: Feb 28, 2007
  Messages: 50
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 15
  Ccm ni wanjanja wanajua gia ya kuingilia katika uchaguzi haya mambo ya pensheni za wazee yatapita na mengine
  yatakuja na yatapita hakuna kitakachofanikiwa.mbona hayo makambi ya wazee kama yale ya nungwi hakuna hata
  wa kwenda kuwasalimia wacha kuwapa chochote
   
 10. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #10
  Jul 1, 2010
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  kweli uchaguzi umekaribia:A S tongue:
   
 11. Lyampinga

  Lyampinga Senior Member

  #11
  Jul 1, 2010
  Joined: Apr 13, 2008
  Messages: 143
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 45
  Luteni wewe unaishi ulaya nini?:A S-eek: Changa la macho hilo, wazungu wenyewe they struggle to upkeep their elderly. Wawalipe wale wazee wa East African Community kwanza halafu ndio tuanze kukubali huu upuuzi. CCM waongo bwana wameshatia kibindoni hizo kura za hao wazee milioni mbili:mad:
   
 12. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #12
  Jul 1, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Nafikiri unayoyasema ni yale yale niliyosema kuwa walipwe wazee wa iliyokuwa EAC kwanza kabla ya mpango huu, siishi ulaya mzee karibu sana Kinondoni Shamba.
   
 13. l

  luhongedzo Member

  #13
  Jul 1, 2010
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi nafikiri kabla ya kuwalipa wangeanza na kuwaomba msamaha ikiwa ni pamoja na kuwapa fedha za matibabu wale wazee walio mwagiwa maji ya upupu pale Serander bridge.

  Enhee nimekumbuka unajua kipindi kile cha ukoloni wazee waliishi kwa tabu sana ila kwa mapenzi ya mola mpaka leo baadhi bado wangali hai, sasa cha kushangaza wana kuja kuomba msaada wa kulipwa kile walicho kitolea jasho na baadae kuachwa solemba enzi zile eti wanamwagiwa maji nyie subirini msikie mtaona wenyewe kwenye tv zenu, Maana wataanza kuambiwa ati huwezi kupewa hela mpaka uwe na cheti cha kuzaliwa kama mi nadanganya mtaona
   
 14. Belo

  Belo JF-Expert Member

  #14
  Jul 1, 2010
  Joined: Jun 11, 2007
  Messages: 11,281
  Likes Received: 4,286
  Trophy Points: 280
  Hatudanganyiki
   
Loading...