Wazee wetu wanatuangusha huko kijijini, Je tuwatose? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wazee wetu wanatuangusha huko kijijini, Je tuwatose?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Ngonini, Oct 6, 2010.

 1. N

  Ngonini JF-Expert Member

  #1
  Oct 6, 2010
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 2,024
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Hivi majuzi nilitembelewa na mama yangu kutoka kijijini kwetu. nilitaka kujua hali ya kisiasa huko wilayani kwetu maana ni sehemu ya ngome ya Mzee Mapesa. aliniambia kuwa mchuano ni mkali mpaka kwenye udiwani. Nilifurahia maana hata serikali za vijiji vingi vinaongozwa na MAGEUZI (kama wanavyowaita wao). Kuhusu ubunge alisema Mzee wa vijicenti atapita maana watu wanachuma mno kwake. Alisema lakini kwenye jimbo la Mzee MAPESA sisiemu hawatafua dafu. Nilipomuliza Kuhusu urais yeye alisema KIGWEDE(ndivyo wanavyomwita wao).

  Kuhusu namna kampeni zinavyoendeshwa, alisema wao huwa wanakusanywa kwenye vikundi ili kwenda kwenye mikutano ya sisiemu wakiwa wameahidiwa chumvi,kanga na fedha tasilimu. Mama yangu alikuwa akilalamika kuwa siku moja waliahidiwa kupewa fedha na baada ya mkutano waliambulia TSH 5000 (huku wakiwa watu zaidi ya 50)kama kikundi ili wagawane. waliishia kununua chumvi wakagawana kila mtu kiganja kimoja(Handful).

  Nilichokipata kutoka maongezi na mama yangu ni uelewa mdogo wa mambo, yeye anasema "sisi hata hatujiwi kama watu wingi hivi hawamtaki KIGWEDE, sisi tunajua anakubalika tu".
  Ndipo nilipomwelezea hali halisi ya watu kutaka mabadiliko. Alishangaa na kusema hata sisi tungepata mtu wakuelimisha SISIEMU tumeichoka ila hatujui cha kufanya.

  Alikili kuwa ukipewa hongo na sisiemu, watakutishia mpaka utawapigia kura maana wanaogopa kuwa wanaweza kukundulika kuwa hawakuipigia sisiemu.  MIMI NAONA KUNA HAJA YA KUWAAMBIA WAZEE WETU KAMA HAWATAKI KUBADILIKA BASI NA SISI WASITEGEMEE MSAADA KUTOKA KWETU. TUNAPATA KIMSHAHARA KIDUCHU BADO TUNAGAWANA NAO ILI WAPATE CHAKULA,DAWA, ELIMU N.K WAKATI SERIKALI IMEKAA DAR NA DODOMA WAKILA KUKU BADALA YA KUWATIMIZIA HAYA WANANCHI WAKE.

  WAZEE HAWA NI LAZIMA WATUELEWE MAANA SISI JAPO TUNA NAFUU KULIKO WAO, LAKINI BADO HAWATAKI KUTUELEWA. JIBU HAPA NIKUWANYIMA SERVICE ILI WATAMBUWE UMUHIMU WA KUWA NA SERIKALI INAYOWAJIBIKA.
  KAMA SISIEMU INAWATISHIA NA KUKUBALIANA NAYO, BASI NA SISI TUWANYIME MISAADA YETU KAMA SISIEMU ITAWAPATIA HAYO MAHITAJI. TUKIFANYA HIVI WATABADILIKA NA NDO ITAKUWA KIFO CHA SISIEMU HUKO VIJIJINI PIA.

  NILAZIMA TUONDOKE NA WAZEE WETU, HATUWAACHII SISIMU, WATATUELEWA HUKO MBELE TULIMAANISHA NIN KUWALAZIMISHA KUHAMA SISIEMU!

  TUSIPOTUMIA NGUVU KAMA HII, ITATUCHUKUA MIAKA ZAIDI KUPATA USHINDI.

  NAOMBA KUWASILISHA!
   
 2. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #2
  Oct 6, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Hapana mkuu hatuna haja ya kuwatosa wazee wetu ni kuwapa elimu ya kutosha waelewe kinachoendelea!
   
 3. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #3
  Oct 6, 2010
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  ngonini inaonekana hata wzazi wako haukuwapatia habari kuwa kigwede alikataa kuongeza mishahara ili uwezo kuwa na uwezo wa kuwaongezea kile kidogo unachowatumia. Kwa kifupi watanzania wengi hatujafanya homework zetu ili kufanikisha mageuzi. Jf ni sehemu ya kupata elimu na kubadilishana mawazo tu; tunachokipata humu tunatakiwa kukisambaza kwa wanchi wenzetu kama vile wazazi na wengineo ili kuchochea mabadiliko.
   
 4. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #4
  Oct 6, 2010
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Wanafunzi wa vyuo waliokataliwa kurudi vyuoni watumie fursa hii kuwaelimisha wazee juu ya kiongozi bora huko vijijini wasikose yote
   
 5. Nchi Kavu

  Nchi Kavu JF-Expert Member

  #5
  Oct 6, 2010
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 3,519
  Likes Received: 1,041
  Trophy Points: 280
  Kigwede bwana. Waendelee kuogopa tu ila mpe somo akawaelimishe na wenzake
   
Loading...