Wazee wetu wana mambo mengi sana kuhusu maisha, tukae nao tupate japo kidogo tu. Soma hii...

Phdum

JF-Expert Member
Apr 15, 2019
810
1,667
Vijana wa kileo hatuna kabisa desturi ya kukaa na wazee ili tupate madini waliyonayo. nakuhakikishia hawa wazee wanajua masuala mengi sana kuhusu maisha na vitu vingi walivyokuwa wanaona sio sahihi ila sisi vijana wa kileo tunaona ni sahihi huku tukisema ndio utandawazi.

Sikia hii. Uliwahi kusikia au unafahamu ule usemi usemao "mwanamke mwenye mimba hana ujanja"? Mimi ni miongoni mwa watu waliokuwa wanasikia tu huo msemo ila sikuwahi fahamu kuwa inamaanisha nini.

Jana nilibahatika kukaa na bibi moja nikamuuliza kuhusiana na hii kauli kwamba kwanini mwanamke mwenye mimba hana ujanja.

Kwa maelezo yake ni kwamba mwanamke mwenye mimba akichanganya damu yaani kushiriki na wanaume/mwanamme mwingine ambaye sio mhusika wa mimba siku ya kujifungua atakuwa katika hatari ya kupatwa na mambo makuu mawili

Moja: ni kupata kifafa cha mimba na hata kumpelekea kupoteza maisha yake na hata maisha ya mwanaye pia nikajagundua kuwa siku hizi nasikia vifafa vya mimba vimeongezeka labda chanzo ni hii japo kitaalam kuna chanzo chake ila hawa wazee wetu walikuwa wanaamini kifafa cha mimba hutokana na kuchanganya wanaume wakati wa mimba.

Jambo la pili: walikuwa wanaamini kuwa ukichanganya wanaume ukiwa na mimba siku ya kujifungua utapata sana shida. Unaweza kumaliza siku hata mbili bila kujifungua mpaka aje mtaalamu na kukuuliza kama umechanganya wanaume na ukikubali tu anafanya yake ndio utaweza kujifungua vizuri. hapa napo nikapata ukakasi kuwa au hata hivi vioperation vya kila siku kwa wake zetu hili linaweza kuwa ni chanzo japo wataalam wa afya nao wana sababu zao za kiafya zinazosababisha upasuaji kuongozeka kwa wingi. Maana siku hizi unakuta mwanamke mjamzito lakini mechi za ugenini wanapiga kama kawa.

Karibu na wewe mdau utoe nondo uliopata kutoka kwa hawa wazee wetu
 

Attachments

  • IMG_20191009_100559_367.jpg
    IMG_20191009_100559_367.jpg
    10.4 KB · Views: 1
Siku wakikwambia hospital sio tamaduni zetu na uende kwa mganga wa jadi wakati upo taabani kwa kuumwa na malaria ndio utakapo wakimbia.


Ndukiiiii 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
 
kumbuka dunia inabadilika, wao waliishi zama tofauti na za leo, ndio maana wazungu wana maendeleo hawafuati ushauri uliopitwa na wakati wa wazee, wanawaza yanayokuja sio yaliyopita,
 
Siku hizi tunashauriana facebook tunaelekezana Instagram. Huwezi kurudisha wakati nyuma. Wewe unadhani kwa nini hata suala la kuzuia watoto wa sekondari kuwa na simu ni gumu? Tatizo tunapambana na technology na wakati hapawezi kuwa na mshindi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom