Wazee wetu ndio walifurahia ndoa, sisi vijana wa sasa tunapambana tu

RaiaMimi

Member
Jun 3, 2021
11
51
Habari Wadau,

Kwa maisha niliyoshuhudia mwenyewe na si kuhadithiwa nina kila sababu ya kusema kuwa wazee wetu ndio waliofurahia ndoa na sisi vijana wa sasa tunapambana tu.

Sababu za kwanini nasema wazee wetu ndio walifurahia ndoa ni chache tu ila ni nzito na zinasababisha ndoa kuwa mzigo mkubwa sana na kuchosha wakati mwingine.

1. Katika maisha yangu ya ukuaji, sijawahi ona Mama yangu (Mke wa Baba) akimshinikiza Baba kufanya au kumfanyia jambo iwe kwa njia za moja kwa moja au zisizo za moja kwa moja (yaani manipulations). Hii naiona sana ata kwenye ndoa yangu binafsi yaani kuna muda kunakuwa na mashinikizo hasa yasiyo ya moja kwa moja na kila ukiyatafakari unaona kabisa hapa kuna uelekeo napelekwa.

2. Katika maisha yangu ya ukuaji pia, sijawahi kuona Bibi yangu (Mama wa Baba yangu) akiona kama mkwe wake (Mama yangu) anafaidi sana kwa mwanae (Baba yangu). Bibi na Babu walibaki vijijini na ilikuwa ni ishu ya kutembeleana tu na hata kama kuna msaada utahitajika huko kijijini utaombwa na kwa upendo na busara utatolewa bila mashinikizo yoyote. Mashinikizo yakiwepo hapa mara nyingi yanaleta picha ya ushindani kati ya Mama Mkwe na Mkamwana wake. Si ajabu Mama mkwe akatamka kuwa mbona kwa mke wako umefanya hivi na vile? Hii inafanya ndoa zinakuwa ngumu sana. Mama wakwe wa sasa tafadhali mjitahidi kuwa kama waliokuwa Mama wakwe zenu.

Vile vile, ikitokea ukafanya jambo kwa wazazi wako na mke akajua, ni balaa pia. Si ajabu akashinikiza umfanyie na yeye au ufanye na kwa wazazi wake.

Haya mambo yanafanya hizi ndoa zinakuwa ngumu sana. Ni vyema sana kama haya ndio maendeleo yaliyotokana na Mama wakwe na Wake zetu wote kuwa watoto wa mjini basi wajitahidi kuishi kama ilivyokuwa zamani. Haya mambo yanafanya ndoa hizi hazileti tena furaha bali karaha tu.

Tunaambiwa tuishi na wake zetu kwa akili lakini haya mambo yanafanya hadi akili inazidiwa wakati mwingine na vichwa vinachemsha kabisa.

Kubalance hii ligi ni mziki sana.
 
Mimi si shabiki wa ndoa. Napenda furaha na amani ktk ndoa za Sasa n majanga
 
Tuzitumie ndoa kutafuta mitaji kwa ajili ya biashara zetu, kijana wapaswa kuoa ata mara 3
 
Back
Top Bottom