Wazee wenzangu wa kuweka mzigo (Kubet) - karibuni tubashiri mechi za leo!

Rockcity native

Rockcity native

JF-Expert Member
Joined
Dec 31, 2012
Messages
2,094
Points
1,500
Rockcity native

Rockcity native

JF-Expert Member
Joined Dec 31, 2012
2,094 1,500
Karibuni tuinvest katika soko letu la hisa iwe meridian, iplay8 casino, m-bet, premier betting, skybet, landbrokerz, bet365... n.k
GG (maana yake tim zote zifungane).. GGGG ( tim zote zifungane kila kipindi)

2+ (katika mechi yote yapatikane magoli kuanzia mawili)...

I 2+ (kipindi cha kwanza yapatikane magoli kuanzia mawli)...

II2+ (kipindi cha pili yapatikane magoli kuanzia mawili)....

H2+ (tim ya nyumbani ipate magoli kuanzia mawili)...

A2+ (timu ya ugenini ipate magoli kuanzia mawili)...
Watu wengi katika ulimwengu wa GAMBLING wanajikuta wakipoteza kiasi kikubwa cha pesa bila hata ya kujitambua.Ni kutokana na kutokujua au kutambua misingi kadhaa ya kushiriki katika Mchezo huu

LEO NAOMBA NIWAJULISHE WADAU WA MCHEZO JINSI AU NAMNA YA
KUSHIRIKI KIKAMILIFU NA KUFANIKIWA KUSHINDA KWA KIASI KIKUBWA.
KWA KUZINGATIA MAMBO HAYA #8 ,UTAWEZA KUFANIKIWA KUTENGENEZA FAIDA KUBWA KATIKA MCHEZO HUU.


#1 . UFANYE UWE MCHEZO,KISIWE CHANZO CHA MAPATO.


Watu wengi hufanya mchezo wa football betting kama ni kituo cha kujipatia mapato kwa ajili ya kukidhi haya mbalimbali za kimaisha kama vile
1.kulipa kodi ya nyumba,
2.Kupata ada ya watoto,
3.Kupata fedha ya kununua mali fulani i.e Pikipiki, Simu.
4. Kupata fedha ya kulipa Deni. ...na mengineyo!
Hili ni kosa kubwa sana. Unapofanya huu mchezo kama ni chanzo cha pesa kwa ajili ya suala fulani, linakupotezea nafasi ya kuweza kufanya machaguzi ya Odds
yaliyo sahihi.Watu wenye utaratibu huu ,huwa wanachagua Odds ambazo zitawaletea zao kubwa la pesa na kusahau kuwa si michezo yote katika orodha inayoweza kukupa tokeo chanya.
(Kumbuka, Mahesabu ya kina hufanywa na wenye hizi Betting Companies kuhakikisha hakuna mtu anaweza kupata kiasi kikubwa cha pesa kama matokeo ya betting(Mkeka) wake).

#2 . ZITAMBUE LIGI VIZURI.

Watu wengi hujihisisha katika huu mchezo hata bila ya kutambia mienendo (Trend) ya ligi kuu mbalimbali barani Ulaya.Kutokana na Betting Companies kuwa na aina mbali mbali za "kubet", Pia kuna baadhi ya ligi zina "facilatate successful betting" kutokana na aina ya betting.

Kwa mfano:- Ligi ya Uingereza(EPL) , inafaa sana kutumika katika kubeti katika category ya "NORMAL" kwa asilimia 80%.Hii ni kutokana na ligi kuwa na wababe wanaotabirika , Baadhi ya timu kuwa out-of-form kwa muda mrefu, Mjeruhi ya mara kwa mara.
Ligi ya Spain(LA LIGA), inafaa sana kutumika katika "NORMAL" kwa silimia 70% na "HANDCAP" kwa silimia 30%( timu za R.madrid,Barca,A.madrid)

Ligi ya Ufaransa(LIGUE 1).Kutokana na hii ligi kuto kuwa na wababe wa kueleweka , hapa ni mahali salama sana kuitumia "HANDCAP" 80% na.Pia ni ligi iliyo na idadi ndogo sana ya magoli hivyo basi "FOURTYFIVE" prediction inafaa.Hii ni kutokana na matokeo mengi ya ligi hii kuwa na tofauti ya goli moja.
Ligi kuu ya Itali (Serie A), hii ligi haina tofauti sana na ligi kuu ya Ufaransa.Baadhi ya mechi huwa na tofauti ya goli moja, na mara nyingi huwa na matokeo ya suluhu katika dakika 45 za kwanza. Hivyo "HANDCAP" ina asilimia 60% na "FOURTYFIVE" ina asilimia 40%.(Tahadhari: Hii ligi inahitaji uchambuzi wa kina katika mechi zake kabla ya kuweka bet,)

#3 . BOBEA KWENYE LIGI CHACHE TU.

Si mbaya sana ukichagua baadhi ya timu zenye nguvu kutoka ligi nyingine, bali umuhimu wa kubobea katika ligi chache ni veyma zaidi.Hii itakufanya uwe mwenye uelewa na utambuzi wa kutosha na mwenendo wa hizo ligi chache. Pia hii itakuwezesha kuweza kufanya maamuzi sahihi yaliyo na ufahamu na uelewa yakinifu.,

#4 . MARA NYINGI NI VYEMA KUFUATA HISIA.

Umeshawahi kutazama orodha ya michezo/mechi za siku husika kuanzia ya kwanza hadi ya mwisho, na katika akili yako kuna hisia/vochochezi ambavyo vina kuambia kwamba "huyu anashinda" au "huyu anafungwa" au "hii mechi suluhu"?
Basi kwa taarifa yako, hizo hisia-za-mwazo(PRESCIENCE) husadikika kuwa sahihi kwa asilimia 80%.
Hii ni kwa upande wa wale wanao-Bet katika category ya "NORMAL".

#5 . EPUKA USHABIKI.

Kuna nyakati ambazo inakuhitaji uchague mechi ambayo timu uipendayo inacheza.Hiki kimekuwa kipindi kigumu sana kwa watu wengi.Hupenda kuchagua timu zao kuwa zitashinda hata kama ukweli ni kwamba zinauwezekano mkubwa sana wa kupoteza mchezo.
Au kuwekea timu fulani ishindwe kwa mategemeo timu yake(anayoishabikia) iendelee kuongoza ligi.
Ukiona umejawa na hisia za ushabiki na huwezi shindana nazo, basi ni bora kuacha kabisa kuchagua mechi hizo.

#6 . FANYA UCHAMBUZI YAKINIFU.

Hili ni pamoja na kuzingatia aina ya mchezo unaocheza. Mfano
-NORMAL; katika hii category unashauriwa kuchagua mechi zenye timu dhaifu na imara.Hii inaleta uwezekano wa kutokea kwa matokeo yaliyo-tabiriwa.
-HANDCAP; hapa unashauriwa kuchagua mechi zenye timu ambazo zenye uwezo unaokaribia na kulingana,kwa kuwa timu moja hupewa goli la kufikirika ambayo mara nyingi huwa ni ile dhaifu basi ni vyema kuchagua matokeo ya Suluhu huku ukiamini kuwa ile timu yenye nguvu zaidi huenda ikashinda kwa tofauti isiyozidi goli 1.Yaani 2-1 au 1-0 au hata 3-2.
-FOURTYFIVE(45); hapa sasa ni mahala ambapo mechi za machaguo ya suluhu kuzingatiwa.Kutokana na mechi kuanza kwa suluhu ya bila kufungana,kuna uwezekano wa asilimia 80% ya hizo mechi kumaliza dakika 45 za kwanza bila kufungana ili uweze kuchagua suluhi ya dakika 45, inashauriwa kuchagua mechi ambazo zina upinzani mkubwa sana baina yao au mechi zenye timu zilizodhaifu sana.

#7 . JIWEKEE KIASI KATIKA KU-BET.

Huu mchezo unaathiri sana tabia-ya binadamu (Addictive).Kuna kipindi unasikia hamu ya kubet kila mara hata pale unapoona mkeka(Betting Form) umeharibika, ili tu uweze kurudisha kile kiasi cha pesa ulicholiwa.Hii hutokea kwa sababu ya kutojiwekea "kikomo".
Weka kikomo ,mfano Tsh 5000/= tu itumike ndani ya saa 72.Itakufanya uwe na kikomo katika mchezo na kukusaidia kutopoteza kiasi kikubwa cha pesa kutoka mfukoni mwako.

#8 . FUATILIA UTABIRI WA MITANDAONI.

Ni vyema kufuatilia utabili wa mitandaoni kwa sababu huwa na takwimu sinazoonyesha historia, Perfomance, na matarajio ya mechi husika.
Hakikisha una-zingatia mechi tano(5) zilizopita.
-Head-to-head ya timu hizo.
-Perfomance ya timu katika dakika 45 za kwanza
-Majeruhi walio n'je ya kikosi kikuu.
-Usajili waliofanya
-zingatia idadi ya magoli ambayo timu hizo zinafunga(score) na kufungwa(concede).
-zingatia idadi ya mechi ambazo timu imeshinda na kupoteza.
-zingatia msimamo/stance ya timu katika mechi za nyumbani na ugenini.
Kuna baadhi ya mitandao maarufu ambayo hutumika kutoa tabiri za mechi mbalimbali.
(1)windrawin.com
(2)predictZ.com

(3)soccervista.com na
(4)livescore.com tu kwa matokeo yaliyo "live" na ya mechi zilizopita.

Nakaribisha maswali na Maoni kwenye eneo lolote lisilo eleweka...!

DemiGod,
Top Handcapper in Tanzania
 
2

2odds

Member
Joined
Sep 25, 2019
Messages
31
Points
125
2

2odds

Member
Joined Sep 25, 2019
31 125
Ungekuwa na lain ya safaricom shida usingepata, kuna 22bet kwa kenya ndo inatumika hiyo kuweka na kutoa pesa, ila 1xbet kutoa tu kwa njia ya simu, mana operator wanakata unapoweka ,nazani walikwepa makato wakatoa njia ya simu kuweka ila hao 22bet is the same as 1xbet.
BetWiner
1xBet
MelBet
22bet
Na 1XBIT

Naona hawa jamaa wanatumia platform moja. Mpaka napata mashaka asije akawa mmiliki ni mmoja wa haya makampuni

Kuna makampuni mengi machanga hayana majina. Yakiona kuna customer anakula kila wiki zaidi ya $500 ghafla bin vuuuh wanaifunga account yako na huwez tena kuitumia
 
Mac Alpho

Mac Alpho

Member
Joined
Aug 5, 2019
Messages
31
Points
125
Mac Alpho

Mac Alpho

Member
Joined Aug 5, 2019
31 125
Hakuna kitu kinauma ka timu zinacheza umezipa under 3.5, af hadi dk ya 80 ngoma lbd iko 1-0, huku ka moyo kanaanza kufurahia, unatoka livescore unajua mkeka ushatiki, ile unakua kucheki unakutana na LOST, unahisi bookmaker matapeli, kwa hasira unaingia livescore, unakuta magoli yalifungwa dk ya 85, 87 90. Af stake mlima,Hapo ndo utajua dunia haina huruma.Unaeza ukapata mafua ghafla ile DAIMA MBELE NYUMA MWIKO we ukaisema DAIBA BELE NYUBA BWIKO. mmh, ukitaka kubet, agana na presha kwnz Mamaeeeeeee..!!
 
Shanyangy

Shanyangy

JF-Expert Member
Joined
Jan 8, 2013
Messages
219
Points
225
Shanyangy

Shanyangy

JF-Expert Member
Joined Jan 8, 2013
219 225
Hii kitu ilinikutaga kuna timu niliipa ishinde mpaka dk ya 86 ilikuwa inaongoza 2 zero na hyo ndo ilikuwa game ya mwisho kwenye mkeka wang nivune bas bana moyo ukaanza kusherehekea ushindi nikatoka live score baadaye naenda kucheki pm nakuta hela bado kuchek mkeka ety lost yaan sikuamin walitoka 2:2 kwel mpira dk 90 yaan unaweza sema kuna uchawi ety.
Hakuna kitu kinauma ka timu zinacheza umezipa under 3.5, af hadi dk ya 80 ngoma lbd iko 1-0, huku ka moyo kanaanza kufurahia, unatoka livescore unajua mkeka ushatiki, ile unakua kucheki unakutana na LOST, unahisi bookmaker matapeli, kwa hasira unaingia livescore, unakuta magoli yalifungwa dk ya 85, 87 90. Af stake mlima,Hapo ndo utajua dunia haina huruma.Unaeza ukapata mafua ghafla ile DAIMA MBELE NYUMA MWIKO we ukaisema DAIBA BELE NYUBA BWIKO. mmh, ukitaka kubet, agana na presha kwnz Mamaeeeeeee..!!
 
Kirikou Wa Kwanza

Kirikou Wa Kwanza

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2013
Messages
3,545
Points
2,000
Kirikou Wa Kwanza

Kirikou Wa Kwanza

JF-Expert Member
Joined May 24, 2013
3,545 2,000
Hii kitu ilinikutaga kuna timu niliipa ishinde mpaka dk ya 86 ilikuwa inaongoza 2 zero na hyo ndo ilikuwa game ya mwisho kwenye mkeka wang nivune bas bana moyo ukaanza kusherehekea ushindi nikatoka live score baadaye naenda kucheki pm nakuta hela bado kuchek mkeka ety lost yaan sikuamin walitoka 2:2 kwel mpira dk 90 yaan unaweza sema kuna uchawi ety.
Ha ha ha ha ha kuna muda unaweza kuhisi labda umerogwa. Hii kazi fixed, ndumba & bahati inahusika sana!
 

Forum statistics

Threads 1,343,109
Members 514,937
Posts 32,774,067
Top