Wazee wenzangu wa kuweka mzigo (Kubet) - karibuni tubashiri mechi za leo!

Rockcity native

JF-Expert Member
Joined
Dec 31, 2012
Messages
2,094
Points
1,500

Rockcity native

JF-Expert Member
Joined Dec 31, 2012
2,094 1,500
Karibuni tuinvest katika soko letu la hisa iwe meridian, iplay8 casino, m-bet, premier betting, skybet, landbrokerz, bet365... n.k
GG (maana yake tim zote zifungane).. GGGG ( tim zote zifungane kila kipindi)

2+ (katika mechi yote yapatikane magoli kuanzia mawili)...

I 2+ (kipindi cha kwanza yapatikane magoli kuanzia mawli)...

II2+ (kipindi cha pili yapatikane magoli kuanzia mawili)....

H2+ (tim ya nyumbani ipate magoli kuanzia mawili)...

A2+ (timu ya ugenini ipate magoli kuanzia mawili)...
Watu wengi katika ulimwengu wa GAMBLING wanajikuta wakipoteza kiasi kikubwa cha pesa bila hata ya kujitambua.Ni kutokana na kutokujua au kutambua misingi kadhaa ya kushiriki katika Mchezo huu

LEO NAOMBA NIWAJULISHE WADAU WA MCHEZO JINSI AU NAMNA YA
KUSHIRIKI KIKAMILIFU NA KUFANIKIWA KUSHINDA KWA KIASI KIKUBWA.
KWA KUZINGATIA MAMBO HAYA #8 ,UTAWEZA KUFANIKIWA KUTENGENEZA FAIDA KUBWA KATIKA MCHEZO HUU.


#1 . UFANYE UWE MCHEZO,KISIWE CHANZO CHA MAPATO.


Watu wengi hufanya mchezo wa football betting kama ni kituo cha kujipatia mapato kwa ajili ya kukidhi haya mbalimbali za kimaisha kama vile
1.kulipa kodi ya nyumba,
2.Kupata ada ya watoto,
3.Kupata fedha ya kununua mali fulani i.e Pikipiki, Simu.
4. Kupata fedha ya kulipa Deni. ...na mengineyo!
Hili ni kosa kubwa sana. Unapofanya huu mchezo kama ni chanzo cha pesa kwa ajili ya suala fulani, linakupotezea nafasi ya kuweza kufanya machaguzi ya Odds
yaliyo sahihi.Watu wenye utaratibu huu ,huwa wanachagua Odds ambazo zitawaletea zao kubwa la pesa na kusahau kuwa si michezo yote katika orodha inayoweza kukupa tokeo chanya.
(Kumbuka, Mahesabu ya kina hufanywa na wenye hizi Betting Companies kuhakikisha hakuna mtu anaweza kupata kiasi kikubwa cha pesa kama matokeo ya betting(Mkeka) wake).

#2 . ZITAMBUE LIGI VIZURI.

Watu wengi hujihisisha katika huu mchezo hata bila ya kutambia mienendo (Trend) ya ligi kuu mbalimbali barani Ulaya.Kutokana na Betting Companies kuwa na aina mbali mbali za "kubet", Pia kuna baadhi ya ligi zina "facilatate successful betting" kutokana na aina ya betting.

Kwa mfano:- Ligi ya Uingereza(EPL) , inafaa sana kutumika katika kubeti katika category ya "NORMAL" kwa asilimia 80%.Hii ni kutokana na ligi kuwa na wababe wanaotabirika , Baadhi ya timu kuwa out-of-form kwa muda mrefu, Mjeruhi ya mara kwa mara.
Ligi ya Spain(LA LIGA), inafaa sana kutumika katika "NORMAL" kwa silimia 70% na "HANDCAP" kwa silimia 30%( timu za R.madrid,Barca,A.madrid)

Ligi ya Ufaransa(LIGUE 1).Kutokana na hii ligi kuto kuwa na wababe wa kueleweka , hapa ni mahali salama sana kuitumia "HANDCAP" 80% na.Pia ni ligi iliyo na idadi ndogo sana ya magoli hivyo basi "FOURTYFIVE" prediction inafaa.Hii ni kutokana na matokeo mengi ya ligi hii kuwa na tofauti ya goli moja.
Ligi kuu ya Itali (Serie A), hii ligi haina tofauti sana na ligi kuu ya Ufaransa.Baadhi ya mechi huwa na tofauti ya goli moja, na mara nyingi huwa na matokeo ya suluhu katika dakika 45 za kwanza. Hivyo "HANDCAP" ina asilimia 60% na "FOURTYFIVE" ina asilimia 40%.(Tahadhari: Hii ligi inahitaji uchambuzi wa kina katika mechi zake kabla ya kuweka bet,)

#3 . BOBEA KWENYE LIGI CHACHE TU.

Si mbaya sana ukichagua baadhi ya timu zenye nguvu kutoka ligi nyingine, bali umuhimu wa kubobea katika ligi chache ni veyma zaidi.Hii itakufanya uwe mwenye uelewa na utambuzi wa kutosha na mwenendo wa hizo ligi chache. Pia hii itakuwezesha kuweza kufanya maamuzi sahihi yaliyo na ufahamu na uelewa yakinifu.,

#4 . MARA NYINGI NI VYEMA KUFUATA HISIA.

Umeshawahi kutazama orodha ya michezo/mechi za siku husika kuanzia ya kwanza hadi ya mwisho, na katika akili yako kuna hisia/vochochezi ambavyo vina kuambia kwamba "huyu anashinda" au "huyu anafungwa" au "hii mechi suluhu"?
Basi kwa taarifa yako, hizo hisia-za-mwazo(PRESCIENCE) husadikika kuwa sahihi kwa asilimia 80%.
Hii ni kwa upande wa wale wanao-Bet katika category ya "NORMAL".

#5 . EPUKA USHABIKI.

Kuna nyakati ambazo inakuhitaji uchague mechi ambayo timu uipendayo inacheza.Hiki kimekuwa kipindi kigumu sana kwa watu wengi.Hupenda kuchagua timu zao kuwa zitashinda hata kama ukweli ni kwamba zinauwezekano mkubwa sana wa kupoteza mchezo.
Au kuwekea timu fulani ishindwe kwa mategemeo timu yake(anayoishabikia) iendelee kuongoza ligi.
Ukiona umejawa na hisia za ushabiki na huwezi shindana nazo, basi ni bora kuacha kabisa kuchagua mechi hizo.

#6 . FANYA UCHAMBUZI YAKINIFU.

Hili ni pamoja na kuzingatia aina ya mchezo unaocheza. Mfano
-NORMAL; katika hii category unashauriwa kuchagua mechi zenye timu dhaifu na imara.Hii inaleta uwezekano wa kutokea kwa matokeo yaliyo-tabiriwa.
-HANDCAP; hapa unashauriwa kuchagua mechi zenye timu ambazo zenye uwezo unaokaribia na kulingana,kwa kuwa timu moja hupewa goli la kufikirika ambayo mara nyingi huwa ni ile dhaifu basi ni vyema kuchagua matokeo ya Suluhu huku ukiamini kuwa ile timu yenye nguvu zaidi huenda ikashinda kwa tofauti isiyozidi goli 1.Yaani 2-1 au 1-0 au hata 3-2.
-FOURTYFIVE(45); hapa sasa ni mahala ambapo mechi za machaguo ya suluhu kuzingatiwa.Kutokana na mechi kuanza kwa suluhu ya bila kufungana,kuna uwezekano wa asilimia 80% ya hizo mechi kumaliza dakika 45 za kwanza bila kufungana ili uweze kuchagua suluhi ya dakika 45, inashauriwa kuchagua mechi ambazo zina upinzani mkubwa sana baina yao au mechi zenye timu zilizodhaifu sana.

#7 . JIWEKEE KIASI KATIKA KU-BET.

Huu mchezo unaathiri sana tabia-ya binadamu (Addictive).Kuna kipindi unasikia hamu ya kubet kila mara hata pale unapoona mkeka(Betting Form) umeharibika, ili tu uweze kurudisha kile kiasi cha pesa ulicholiwa.Hii hutokea kwa sababu ya kutojiwekea "kikomo".
Weka kikomo ,mfano Tsh 5000/= tu itumike ndani ya saa 72.Itakufanya uwe na kikomo katika mchezo na kukusaidia kutopoteza kiasi kikubwa cha pesa kutoka mfukoni mwako.

#8 . FUATILIA UTABIRI WA MITANDAONI.

Ni vyema kufuatilia utabili wa mitandaoni kwa sababu huwa na takwimu sinazoonyesha historia, Perfomance, na matarajio ya mechi husika.
Hakikisha una-zingatia mechi tano(5) zilizopita.
-Head-to-head ya timu hizo.
-Perfomance ya timu katika dakika 45 za kwanza
-Majeruhi walio n'je ya kikosi kikuu.
-Usajili waliofanya
-zingatia idadi ya magoli ambayo timu hizo zinafunga(score) na kufungwa(concede).
-zingatia idadi ya mechi ambazo timu imeshinda na kupoteza.
-zingatia msimamo/stance ya timu katika mechi za nyumbani na ugenini.
Kuna baadhi ya mitandao maarufu ambayo hutumika kutoa tabiri za mechi mbalimbali.
(1)windrawin.com
(2)predictZ.com

(3)soccervista.com na
(4)livescore.com tu kwa matokeo yaliyo "live" na ya mechi zilizopita.

Nakaribisha maswali na Maoni kwenye eneo lolote lisilo eleweka...!

DemiGod,
Top Handcapper in Tanzania
 

SteveMollel

JF-Expert Member
Joined
Jul 12, 2015
Messages
4,361
Points
2,000

SteveMollel

JF-Expert Member
Joined Jul 12, 2015
4,361 2,000
Mimi hata ikicheza Barcelona na Mwadui, siweki DIRECT WIN. Muwe mnajifunza jama. Jama mechi zote za UEFA zimetoa over 1.5, na 95% zimetoa over 2.5 kabisa ila mtu anaenda kukomaa Porto ashinde ... Celtic ashinde ... n.k mwishowe anakuja kutoa kilio kwamba Kanji mchawi, matokeo yameenda kinyume... Ajax anaanza kufungwa yeye, Celtic kaanza kufungwa yeye, Porto katiwa kabisa, Barnsley alikuwepo Home tena kwenye Cup akicheza na Carlisle, na akapigwa tatu bila, wa magoli kacheka wa Win anakuja mwaga machozi hapa.

Hayo ya nani atashinda mwachie Mungu wako, bangaiza na magoli, huwezi kosa mara kwa mara. Magoli ndo njia ya kuelekea ushindi, magoli pia yaweza kurandana na draw, yakikosekana magoli hata win hakuna, huoni?

Na acha kulazimisha ucheze daily. Kwamba kila siku wewe ubet, NO, kagua mechi na si siku. WEKA MKEKA KWA KUJIRIDHISHA NA MECHI na si kwa kuwahi kupata pesa alafu hatimaye hutoboi kitu. Si ajabu mkeka kuchukua siku mbili, tatu, hata nne.

Tazama leo, kama game unayoielewa ipo, weka. Kama hakuna nyingine tumia app yako kwenda kutazama games za kesho pia na hata keshokutwa na keshokutwa...
 

Santino

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2015
Messages
21,763
Points
2,000

Santino

JF-Expert Member
Joined May 11, 2015
21,763 2,000
hao ndo wadau wa makampuni,nwendo wa kuingizana chaka
Chelsea hawezi kumtikisa Liverpool kwa sasa kuna wakati macho husema kweli hata kama tukio bado halijatokea.

Hii game hata kama nina milioni 100 ukiniambia nicheze direct win siwezi kusita kumpa Liverpool.
 

if cap fits

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Messages
714
Points
1,000

if cap fits

JF-Expert Member
Joined Jul 22, 2018
714 1,000
Leo Liverpool akipigwa basi sitakaa nicheze direct win tenaaaaaa
Chelsea hawezi kumtikisa Liverpool kwa sasa kuna wakati macho husema kweli hata kama tukio bado halijatokea.

Hii game hata kama nina milioni 100 ukiniambia nicheze direct win siwezi kusita kumpa Liverpool.
 

Santino

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2015
Messages
21,763
Points
2,000

Santino

JF-Expert Member
Joined May 11, 2015
21,763 2,000
Mashabiki wa Chelsea utawajua tu
Mimi toka nigundue uwezo wa timu yangu ni mdogo huwa sibet kishabiki..

Kuna kipindi Simba kaenda Misri kapigwa 5 nilifurahi kwa sababu ilinipa pesa ila niliumia kwa sababu ni timu yangu. Furaha na raha kwa pamoja.

Liverpool hajafikia kiwango cha kufungwa na Mbeya City ya Uingereza.
 

Santino

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2015
Messages
21,763
Points
2,000

Santino

JF-Expert Member
Joined May 11, 2015
21,763 2,000
Chelsea ni wabaya sana mbele ya kombe. Hawa jamaa huwa ni hatari sana wana bahati sana na makombe kama yule jamaa anajiita cr7. Usije Shangaa hii game ikaamuliwa kwa matuta, hii game nashauri leo tuwe watazamaji tu.
Kwenye mpira bahati huambatana na kikosi bora. Hivi leo Zuma ndiye anakuwa nyuma kupambana na ile safu ya mashambulizi ya Liverpool kisha utegemee bahati?!!!!

Tuwe serious na mpira, bahati tumwachie bukuku.
 

mjr95

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2016
Messages
6,095
Points
2,000

mjr95

JF-Expert Member
Joined Oct 10, 2016
6,095 2,000
Hahahaa, ikitokea Chelsea akashinda leo mbele ya Liverpool yenye kikosi matata ulimwengu basi litakuwa ni tukio la aina yake kwa club ya Chelsea msimu huu. Yaani itakuwa walituadaa sisi mashabiki ili tuelewe ni wabovu kumbe walikuwa wanatusomea upepo tu.
Mimi toka nigundue uwezo wa timu yangu ni mdogo huwa sibet kishabiki..

Kuna kipindi Simba kaenda Misri kapigwa 5 nilifurahi kwa sababu ilinipa pesa ila niliumia kwa sababu ni timu yangu. Furaha na raha kwa pamoja.

Liverpool hajafikia kiwango cha kufungwa na Mbeya City ya Uingereza.
 

mjr95

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2016
Messages
6,095
Points
2,000

mjr95

JF-Expert Member
Joined Oct 10, 2016
6,095 2,000
Mkuu lolote laweza tokea, bahati ni kitu kingine kabisa yaani kama ipo ipo tu ata kama ukiwa mbovu kiasi gani. Ata mimi sikutegemea kama Liverpool angeweza kumtoa Barcelona kwenye nusu fainali ya uefa tena akiwa kwake huku akiwa nyuma ya goli 3 kwahiyo ile ilikuwa ni bahati tu na si vinginevyo.
Kwenye mpira bahati huambatana na kikosi bora. Hivi leo Zuma ndiye anakuwa nyuma kupambana na ile safu ya mashambulizi ya Liverpool kisha utegemee bahati?!!!!

Tuwe serious na mpira, bahati tumwachie bukuku.
 

Santino

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2015
Messages
21,763
Points
2,000

Santino

JF-Expert Member
Joined May 11, 2015
21,763 2,000
Hahahaa, ikitokea Chelsea akashinda leo mbele ya Liverpool yenye kikosi matata ulimwengu basi litakuwa ni tukio la aina yake kwa club ya Chelsea msimu huu. Yaani itakuwa walituadaa sisi mashabiki ili tuelewe ni wabovu kumbe walikuwa wanatusomea upepo tu.
Fainali ya UEFA ilikuwa ngumu kujua bingwa ni nani kutoka na ubora wa timu zote mbili. Ila hii Super Cup hata asiyejua kubet leo anapata pesa mapema sana.

Liverpool kwa sasa ni timu daraja la kwanza hivyo hata wachezaji wake huelewa nini kinatakiwa kufanywa uwanjani . Chelsea imeanza upya haiwezi kuhimili vishindo vya Liverpool.
 

Forum statistics

Threads 1,344,365
Members 515,441
Posts 32,817,454
Top