Wazee wastaafu mna uzalendo kweli au bora liende?

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
39,795
71,214
Kila kukicha nafuu ya Jana kuliko Leo. Na taifa likifikia hatua hiyo ni kuwa linachikichia na matumaini ya maendeleo ya kizazi kijacho hakuna.

Haya yote yanafanyika kutokana na uongozi wa awamu hii kutozingatia misingi ya utawala bora, kuheshimu katiba na sheria na pia kutokushirikisha wadau wote wa siasa na maendeleo.

Wakuu wote wa awamu zilizopita kuanzia ya pili hadi ya nne wapo, ma PM na wataalamu wastaafu wapo sasa shida ni nini hawajitokezi kutoa ushauri bali nao kuingia mkumbo wa kusifia hata tunapotumbukia kwenye shimo?

Biashara zimedoda, mahusiano kimataifa yameharibika, mikataba inavunjwa na kutuletea umasikini kwa kulipishwa fidia na utawala bora unadumaa hivyo watumishi hawana ari tena ya utumishi.

Jee hawa viongozi wastaafu Uzalendo umewaishia hivyo wanaona bora liende tuu kwa vile wao wanahudumiwa kwa pension nono?
 
Kunyamaza kimya hali wananchi masikini wanawahudumia kwa Kodi zao ni usaliti mkubwa sana wanaofanya.
Ni kukosa Uzalendo
 
Nasikia huko Jamhuri ya watu wa kusadikika wamekagua benki kuu yao wakaona hakuna pesa za kigeni. Yani reserve ya pesa za kigeni ni ndogo sana kiasi kwamba haitoshi kufanya purchase nje kwa miezi kadhaa ijayo. Kwahiyo wameamua kwenda kuzitafuta kwenye maduka ya kubadili fedha. Wanaamini zimefichwa huko. Kwamba wenye maduka wamezibana na hawataki kuziachia. Kwahiyo wameamua kwenda kuzisaka kwa mitutu ya bunduki. Songombingo za Kaboka mchizi.!

Ngoja niwape shule kidogo. Sababu za msingi za kupotea kwa 'dola' katika nchi hiyo ni hizi hapa.

#Mosi; nchi huwa inapata pesa za kigeni kwa kuuza bidhaa na huduma nje. Lakini nchi ya kusadikika imezuia kuuza mazao nje. Nasikia huko mahindi yanaozea ndani, mbaazi ndo kwisha habari yake, tangawizi hata ukitupa watu hawaokoti. Hivyo vyote vilikuwa vina soko kubwa nje ya nchi na vinaingizia nchi hiyo pesa nyingi za kigeni. Lakini mfalme wao akapiga marufuku wasiuze nje. Leo wanamtafuta mchawi. Maajabu.!

Koro-show nasikia nayo imezuiwa kuuzwa nje. Serikali ktk nchi ya kusadikika imesema itanunua yote. That means hakuna pesa zozote za kigeni nchi hiyo itaingiza. Kama makampuni binafsi kutoka nje yangeruhusiwa kununua yangekuja na 'dola'. Wangechange na kupata madafu ya kulipa wakulima. Hayo 'madola' yaliyochenchiwa yangeingia kwenye mabenki na hatimaye benki kuu. Kwahiyo serikali ingeongeza reserve yake ya pesa za kigeni. Lakini wameamua kununua koro-show zote wenyewe, leo wanatafuta dola kwa mitutu?

Na mfalme wao amesema akikosa soko atamwambia kila mtu kwenye nchi hiyo ale ratili mbili za koro-show. Hizo ratili mbili kwa kila raia zinanunuliwa kwa pesa ya madafu na zitaliwa na raia wa humohumo ndani. Kwahiyo koro-show zote zinaweza zikaisha bila kuingiza hata dola moja kwenye nchi hiyo. Hii ni biashara kichaa ktk historia ya biashara duniani.!

#Pili; nchi inapata pesa za kigeni kupitia mikopo na misaada mbalimbali ya kimataifa kama vile kutoka Benki ya dunia, IMF, na mataifa wahisani kama Marekani, Umoja wa Ulaya etc. Sasa nasikia Benki ya dunia imesitisha mikopo na misaada kwenye nchi hiyo. Baadhi ya mashirika ya kimataifa nayo yamesitisha shughuli zake huko. Umoja wa Ulaya nao unafikiria kusitisha misaada yote kwa nchi hiyo, na tayari balozi wao ameshafurushwa. Kwahiyo hakuna 'foreign grant wala loan' ambayo inaingiza pesa za kigeni kwenye nchi hiyo kwa sasa. Lakini wanaenda kutafuta pesa za kigeni kwa AK47 kwenye maduka ya kubadili fedha. Hekaya za Abunuasi.!

#Tatu; Nchi inapata pesa za kigeni kwa kukaribisha wawekezaji wa kigeni kwa wingi (Foreign investors). Mwekezaji akienda kujenga kiwanda katika nchi fulani haendi na pesa za madafu, anaenda na dola. Akifika huko hizo dola anazibadili na kupewa madafu. Dola zinaingia kwenye system na kuongeza reserve ya pesa za kigeni.

Lakini kwenye nchi ya kusadikika foreign investors wanafokewa na kunyang'anywa passport. Kiongozi akishashiba 'ugali tembele' anaropoka tu 'mnyang'anyeni passport'. Matokeo yake wawekezaji wanahamisha mitaji na kwenda kuwekeza kwenye nchi nyingine. Leo nchi ya kusadikika iko busy kutafuta nani kaficha pesa za kigeni kwenye sandarusi. Harakati za pimbi.!

#Nne; nchi inaingiza pesa za kigeni kutokana na jinsi inavyouza utaalamu wake nje ya nchi. Lakini kwenye nchi ya kusadikika wataalamu wamezuiwa kwenda kufanya kazi nje. Serikali yao imesema mtu yeyote anayepata kazi nje ya nchi inabidi aombe kibali kwanza akiambatanisha mkataba wa ajira. Na serikali inaweza kumruhusu au kumkatalia. Leo serikali hiyohiyo ipo 'busy' kutafuta dola kwenye maduka ya wahindi. Futuhi.!

#Tano; Njia nyingine ya kumaintain pesa za kigeni ni kuregulate kiwango cha kununua na kuuza bidhaa na huduma nje ya nchi. Unatakiwa kuuza zaidi kuliko unavyonunua. Hakikisha unanunua nje vitu vya muhimu tu. Vingine vitengeneze mwenyewe. Hii ni kwa sababu kila unapoagiza bidhaa yoyote nje ya nchi unapunguza reserve yako ya pesa za kigeni. Lakini kanchi ka kusadikika kanatumia reserve yake ya pesa za kigeni kununulia hadi toilet paper, halafu leo kanatafuta pesa zilikofichwa. Inna Lillahi wa inna ilayhi raji'un.!

Malisa GJ
 
Rais ajae Atakuwa na Kazi kubwa sana kuirudisha nchi kwenye mstari huyu kainyosha hadi imepinda na kukatika kabisa,ajae ana Kazi kubwa sana ya kulipa madeni kupunguza deni la taifa,kuinua uchumi mfu, kurejesha tija na morali ya Kazi kwa Watumishi, kuwasukuma ndani wasiojulikana, kujenga demokrasia, kuvutia na kushawishi wawekezaji, kurejesha diplomasia ya kimataifa, kupunguza ttzo la ajira,kuimarisha shillings yetu, kuujenga upya umoja wa kitaifa,kurejesha imani ya vyombo vya dola kwa wananchi, kufukua makaburi yote na kuwasukuma ndani wote waluotumia vibaya Madaraka, vibaya kodi zetu,kukaa kimya juu ya upotevu wa watu,kuinua elimu,kurejesha mifumo ya haki ya kodi, kuifufua Bandari iwe bize kama zamani,nk.Kazi ni kubwa si ya kitoto.Ajae awe na nyota ya Pesa na mwenye BARAKA kila kitu kitakuwa sawa.PhD ya korosho si sawa na PhD ya uchumi.
 
Rais ajae Atakuwa na Kazi kubwa sana kuirudisha nchi kwenye mstari huyu kainyosha hadi imepinda na kukatika kabisa,ajae ana Kazi kubwa sana ya kulipa madeni kupunguza deni la taifa,kuinua uchumi mfu, kurejesha tija na morali ya Kazi kwa Watumishi, kuwasukuma ndani wasiojulikana, kujenga demokrasia, kuvutia na kushawishi wawekezaji, kurejesha diplomasia ya kimataifa, kupunguza ttzo la ajira,kuimarisha shillings yetu, kuujenga upya umoja wa kitaifa,kurejesha imani ya vyombo vya dola kwa wananchi, kufukua makaburi yote na kuwasukuma ndani wote waluotumia vibaya Madaraka, vibaya kodi zetu,kukaa kimya juu ya upotevu wa watu,kuinua elimu,kurejesha mifumo ya haki ya kodi, kuifufua Bandari iwe bize kama zamani,nk.Kazi ni kubwa si ya kitoto.Ajae awe na nyota ya Pesa na mwenye BARAKA kila kitu kitakuwa sawa.PhD ya korosho si sawa na PhD ya uchumi.
Hawa wastaafu wanaharakisha watu wachoke na kumuondoa aliyepo na kumuweka ambaye hatawalinda tena.
Hiyo ni hatari ambayo hawajui kuwa itawajia kutokana na kimya chao
 
Bado wanaamini kuwa hata nchi ikigawanyika na kuingia vitan watakuwa salama. Watabeba passpot na kad zao za bank kwenda kuishi zao ulaya. Wanasahau hata uwe na mali kivip nyumban kwako ni zaid ya popote utembeapo dunia hii. Maisha haya tuishiyo tazanzania kuna watu wako ulaya wanayataman.
Wanasahau kuwa, kuna watu wako ulaya wanataman hii socialization yetu, mara tukutane chako ni chako baa kupiga mbili tatu, mara tuzinguane kwenye kuchangiana michango ya harusi. Mara tutaniane ohhh mim muha namiliki meli zote tanganyika.
Mara nikitaka kuoa au kuolewa najichagulia rangi tu au kama ana wezere au bambataa au ana dimple, badala ya kuangalia kabila au dini anayotoka.
Wanasahau kuwa ni tanzania peke ambayo ndo ina fursa kibao za kuweza kuifanya iizid hata dubai kukiwa na mipango mizuri.
Wanasahau ni tanzania pekee ambapo watu wake wanashindana kusomesha shule nzuri za mamilion huku wanaishi chumba kimoja cha uswaz ili tu kizaz kijacho kiwe cha kistaarab.
Wanasahau huko ulaya hakuna wandengereko wala wazaramo ambao kwao mafiga matatu ni kawaida.
Wanasahau moshi haiko ulaya , mambo yakiharibika hakuna kwenda kuhiji mwez wa kum na mbili.
HAWAJUI KUWA WAKITUONDOA KATIKA HII KADHIA WATAISHI VIZUR NA HISTORIA ITAANDIKWA VIZAZI NA VIZAZ HATA KAMA KUNA SEHEMU WALIWAHI HARIBU.
Adui na moja wa watanzania ni uoga sio ujinga wala elimu wala afya
 
Kama kauli zile za Leo UDSM, wao hawaoni kuwa wanaharakisha chuki ya utawala mwingine Ku review katiba na kuona kipengele chakushtakiwa kikawepo na wao hawatapona?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom