Wazee wasema jimbo la Same Magharibi liko wazi, waomba Chadema wajipange

tarehe 26/04/2012 kupitia forum hii nilitangaza mkutano wa kusimika mabalozi wa chadema kijiji cha nkwini kata ya makanya wilaya ya same na niliomba kusaidiwa kadi 500 na bendera 50 za cdm kutoka uongozi wa taifa. Ninafuraha kuwajuza kuwa mkutano ulifanyika kama ulivyopangwa tar 29/04 na nilipata kadi na bendera . Katika hali ya kustaabisha wazee wakitongoji cha nkwini kata ya makanya wilayani same wameng'ang'ania kadi chache za chadema na kulaani ccm kwa kuwapotezea matumaini yao na vizazi vyao kwa muda wa miaka 50. Wamesema jimbo la same magharibi limekuwa wazi tangu uchaguzi upite 2010. Hii nikutokana na mbunge wao david matayo kutofanya chochote tangu wa mchague, huku akiacha udongo aina ya boxite ukisafirishwa toka chome kwenda kenya bila wananchi kunufaika. Wameelezea kero zao kuwa ni pamoja na migogoro ya ardhi, shule kukosa choo, kukosa dispensar, maji, na ujira mdogo wanaolipwa kama vibarua katika shamba la mkonge. Wazee hao wamewataka viongozi wa chadema kujipanga vizuri ili kuchukua jimbo la same magharibi ambao kwao wanaona kama liko wazi. Hapa nime attach picha ya mzee wa miaka 80 akipokea kadi ya chadema baada ya kurudisha ya ccm. Mkutano ulifanywa na mwanaharakat godson mbaga (0752225501)

usimuamshe aliyelala, utalala wewe
 
wakati sahii wa kukuondoa hicho chama cha matapeli ni sasa, hongereni sana.
 
Kuna wakati fulani wakati wa enzi za siasa ya Ujamaa na Kujitegemea, Wapare walijulikana kama Wachina wa Tanzania. Jina hili lilitokana na uwezo wao wa kuchapa kazi za kuleta maendeleo yao. Walipata sifa hizo kwa kuweza kuchonga barabara za milimani, ujenzi wa mashule, Ushirika (Vuasu Cooperative Uinion) na kazi mbalimbali za kujitolea. Kazi hizo zilifanyika kwa kushirikiana pamoja ambayo ilijulikana kama 'msaragambo'. Tabia hii ya kushirikiana kwa pamoja kuleta maendeleo ya kijamii inaelekea imekufa kwa sasa. Nikiangalia, kwa mawazo yangu, nadhani kuwa hali hii imetokana na kukosekana kwa uongozi katika jamii, uongozi ambao ungweweza kutunga na kusimamia sera za kimaendeleo.

Hali hiyo inaweza kubadilika kama tutapata viongozi ambao wanaweka maslahi ya wananchi kwanza, viongozi ambao watawapa msukumo wananchi kuleta maendeleo yao wenyewe, maenedelo ambayo yatakuwa endeluvu kwani wananchi wenyewe wataona faida za juhudi zao. Wakati umefika sasa wa kujitokeza na kurudisha hadhi ile iliyokuwepo enzi zile, lakini sasa kwa bidii zaidi.
 
Mtoa mada heshima yako kamanda(kama ni kweli ulivyojitambulisha) nina maswali mawili ambayo yananifanya mimi niamue kutokukubaliana na habari yako uliyoitoa hapa zaidi ukikilaumu chama kwa kukutumia vifaa vichache vya uenezi tofauti nan maombi yako.
Kwanza,kama ulijishughulisha namna hiyo mpaka kuomba makao makuu wakutumie bendera na kadi ni dhahiri kuwa wewe ni kiongozi kwenye level flani ndani ya chama,hivyo unaielewa vizuri katiba,sheria na utaratibu wa kufanya mambo ndani ya chama.kwamba suala la chama kutokukutumia bendera na kadi kiasi ambacho ulikuwa unahitaji halikuwa suala la kuliongelea hapa JF.hayo mambo ulitakiwa uyafikishe kwa wahusika ndani ya chama chako.Hapa wanaJF hakuna aliyekuwepo au aliyesikia maombi yako wakati unahitaji hivyo vifaa,na wala hukutumia JF kupeleka maombi yako ya kuhitaji bendera na kadi.sasa sioni kama ni hekima ukijidai kuongelea issues ambazo hazituhusu sisi members wa JF.wananchi wanataka kusikia habari za ukuaji wa chama na sio habari za kushutumiana ndani ya uongozi wa chama.peleka shutuma zako panapo husika kwa muujibu wa sheria na utaratibu mnaoufuata manake ukiongelea hapa hutakaa upate solution yake.
Pili,kwamba kama kweli ulikuwa na uhakika ungeweza pata watu wengi namna hiyo wa kuwapa kadi na kutumia bendera zote hizo kijijini kwako hapo,lazima pia ulitakiwa uwe na vidhibitisho vya kufanya makao makuu wakuelewe zaidi.suala la kuhisi au kufikiria unaweza kugenerate watu wengi namna hiyo halina msingi wowote.uelewe kwamba kwa jinsi chama kinapanuka kwa kasi ya ajabu sio wewe tu unayehitaji vifaa vya uenezi vya bure.ni kila sehemu Tanzania nzima.
Ukisema wewe ni kamanda wa kweli lakini ushaanza kutoa shutuma sehemu ambazo hutakiwi kuzitoa,basi jua yatakupata yaliyowapata jamaa wale wa CUF na NCCR Mageuzi.Be blessed!

Acha pumba mtu wangu..wewe unataka makosa yasiongelewe wazi wazi? jamaa hajakosea kitu hata kimoja hakuna kuficha jambo kama aalipiga simu makao makuu na hakupewa vifaa lazimaaongee wazi wazi tujue mzembe ni nani na kwa nini hawakumpa vifaa, hii ndio kazi yao ili kukiimarisha chama. Sasa hapa naona hutendi haki kumlaumu jamaa ama kumkosoa
 
wakati sahihi wa kukiondoa hicho chama cha matapeli ni sasa, hongereni sana.
 
nimeipenda juhudi yako kaka, hata mwenyekiti wa bavicha katika kufungua tawi la CDM chuo cha st. john dar alitudokezea kuwa sisi vijana tunakiwa kukisaidia chama maake vijiji vya tanzania ni vingi mno vyapata kama 20,000. Let's keep on creating awareness on the issue
 
Tarehe 26/04/2012 kupitia forum hii nilitangaza mkutano wa kusimika mabalozi wa CHADEMA kijiji cha Nkwini Kata ya Makanya Wilaya ya Same na niliomba kusaidiwa kadi 500 na bendera 50 za CDM kutoka uongozi wa Taifa. Ninafuraha kuwajuza kuwa mkutano ulifanyika kama ulivyopangwa tar 29/04 Na nilipata kadi na bendera . Katika hali ya kustaabisha wazee wakitongoji cha Nkwini Kata ya Makanya wilayani Same wameng'ang'ania Kadi Chache za CHADEMA na kulaani CCM Kwa kuwapotezea matumaini yao na vizazi vyao kwa muda wa miaka 50. wamesema Jimbo la Same Magharibi Limekuwa wazi tangu uchaguzi upite 2010. Hii nikutokana na Mbunge wao David Matayo kutofanya chochote tangu wa mchague, huku akiacha udongo aina ya boxite ukisafirishwa toka Chome kwenda Kenya bila wananchi kunufaika. wameelezea kero zao kuwa ni pamoja na migogoro ya Ardhi, Shule kukosa Choo, kukosa Dispensar, Maji, na ujira mdogo wanaolipwa kama vibarua katika shamba la Mkonge. Wazee hao wamewataka Viongozi wa CHADEMA Kujipanga vizuri ili kuchukua Jimbo La Same Magharibi ambao kwao wanaona kama liko wazi. Hapa nime attach picha ya mzee wa miaka 80 akipokea kadi ya CHADEMA baada ya kurudisha ya CCM. Mkutano ulifanywa na mwanaharakat Godson Mbaga (0752225501)

Hilo la udongo kuchukuliwa limelalamikiwa sana ila baada ya wananchi kufuatilia kwa karibu wamegundua anayechimba na rafiki wa karibu wa Mbunge Mathayo na anaitwa Willy.Jamaa ametajirika sana na huo udongo na inavyoaminika anagawa percent kwa viongozi wa mkoa.akiguswa hugusiki.Mathayo hafai kwa sasa watu wamechoka sana
 
Pamoja kamanda
nimeipenda juhudi yako kaka, hata mwenyekiti wa bavicha katika kufungua tawi la CDM chuo cha st. john dar alitudokezea kuwa sisi vijana tunakiwa kukisaidia chama maake vijiji vya tanzania ni vingi mno vyapata kama 20,000. Let's keep on creating awareness on the issue
 
Back
Top Bottom