Wazee wadai Mkukuta haujawasaidia

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,172
Wazee wadai Mkukuta haujawasaidia
Thursday, 16 December 2010 21:03

Brandy Nelson, Morogoro
MPANGO wa Kukuza Uchumi na Kuondoa Umasikini Tanzania (Mkukuta) awamu ya kwanza umedaiwa kutowasaidia wazee kutokana na Serikali kushindwa kuteleza mambo yaliyomo kuhusu Wazee.

Madai hayo yalitolewa juz na baadhi ya wazee mkoani Morogoro walipokuwa wakizungumza na waandishi wahabari kuhusu mipango iliyowekwa na serikali kwa ajili ya kukabiliana na umasikini wa wazee.

“Mipango ya Serikali kwa ajili ya kuwasaidia wazee kukabiliana na umasikini ipo, lakini tatizo kubwa hayatekelezeki kwani hata katika Mkukuta awamu ya kwanza una mambo mengi yanayohusu wazee, lakini Serikali haijatekeleza na sasa tayari kuna Mkukuta awamu ya pili,”alisema. Mwenyekiti wa wazee, Kata ya Bigwa mkoani Mororogoro, Godlight Lyimo
alisema kwa ujumla serikali imeshindwa kutekeleza sera ya wazee hasa katika kipengele kilichomo katika Mkukuta awamu ya kwanza.

Alisema kwa msingi huo, wazee wengi hawaoni sababu au faida ya kuwepo kwa Mkukuta awamu ya pili .

Naye Evelady Wilson alisema kuwa wazee ni watu ambao wamesahauliwa na Serikali kutokana na kutotekelezwa kwa sera ya wazee kwani hadi sasa kauli ya matibabu bure kwa wazee imebakia midomoni mwa viongozi wa kisiasa na si vitendo.
Alisema hadi sasa ni wazee wachache pekee ambao wamepewa vitambulisho kwa ajili ya kutibiwa bure katika vituo vya kutoa huduma za afya kwani huduma za hospitali za sasa ni za kulipia.
Kwa upande wa mratibu wa kituo cha habari cha Wazee, Kata ya Kihonda Michael Kihonda, alisema kuwa viongozi wa serikali wako mbali na vituo hivyo kwani hawaoni umuhimu kushirikisha vituo vya wazee katika shughuli za huduma kiafya.

“Mkukuta unaeleza kuwa wazee wanatakiwa wapewe pensheni, lakini hicho kitu hakuna kabisa ,kwani hadi leo tunalipishwa majengo pamoja na kuwa maeneo mengine hawalipishi hivyo tunachokiona hapa ni urasimu unaofanywa na baadhi ya watendaji wa Serikali”alisema

Alisema kuwa Urasimu wa baadhi ya watendaji wa kata ndiyo unaosababisha kukwamisha utekelezaji wa sera ya wazee katika suala la msamaha wa kodi ya majengo kwa wazee.
 
"Mipango ya Serikali kwa ajili ya kuwasaidia wazee kukabiliana na umasikini ipo, lakini tatizo kubwa hayatekelezeki kwani hata katika Mkukuta awamu ya kwanza una mambo mengi yanayohusu wazee, lakini Serikali haijatekeleza na sasa tayari kuna Mkukuta awamu ya pili,"alisema. Mwenyekiti wa wazee, Kata ya Bigwa mkoani Mororogoro, Godlight Lyimo
alisema kwa ujumla serikali imeshindwa kutekeleza sera ya wazee hasa katika kipengele kilichomo katika Mkukuta awamu ya kwanza.

Nilichojifunza kwenye mipango ya maendeleo ya serikali ni mipango ya viongozi ili waonekane na jamii kuwa wananawajali lakini ukweli ni mipango ya kujipatia madaraka na umaarufu wa bei poa..........................

Tukijiuliza hivi Mkukuta uliandaliwa na nani na kwa manufaa ya nani..........majibu hapo ni mepesi sana ya kuwa mpango huu kama ilivyo mipango mingine ni viongozi tu ambao wanananufaika............................lakini siyo raia walengwa hata kidogo............
 
Back
Top Bottom