Wazee wa yanga wakataa kuingiza team uwanjani tarehe 3 july vs simba

SImba wasikae kimya inaonekana utopolo wanafanya makusudi kuwanyima mapato Simba sababu mechi ya kwanza utopolo alikuwa mwenyeji na mapato yote akachukua lakini kwa sababu mechi hii utopolo hapati kitu anaanza kuleta mind game za kipumbavu.
Mzigo uko kwenye account tangia trh 8
 
Kama nilivyotanabaisha hapo juu mmechangia kihisia zaidi na ni ukweli usiofichika wengi wenu vilaza! Case closed
 
Wakati mwingine tuwaheshimu wazee wetu tuwaache wapumzike kuliko kuwaingiza kwenye mambo kama haya. Na wa kulaumiwa ni viongozi wa Yanga kwani hii "move" ilianzishwa na Bumbuli "script" ikawa imekosewa. Sasa wamekosea zaidi baada ya kuwatumia wazee ambao kwa watu wenye uelewa wanaona kabisa wamelishwa maneno matokeo yake wanajichanganya katika maelezo yao. Yanga kuna ombwe kubwa la uongozi kiasi najiuliza kila siku hivi ilikuwaje watu wa mpira kama wakina Tiboroha, Mkwasa, Sekilojo, Mayay, Mziba, Bin Kleb, Seif Magari, Binda, Chanji na wengineo wakakaa mbali kiasi wakaiacha timu kubwa kama Yanga yenye historia kubwa Tanzania na Afrika ikaingia mikononi kuongozwa na watu ambao leo "wanajustify" kukimbia mechi kwa sababu za hovyo za kuaihirishwa mechi. Na ndio sababu watu wachache waliopo sasa wenye weledi kama wakili msomi Simon wanapigwa vita kila leo. Kwa mtu anayezifahamu Simba na Yanga zikikutana hata timu mojawapo iwe dhaifu kiasi gani sio kigezo cha kushindwa na mara kibao timu inayoonekana dhaifu ndio hupata matokeo. Sasa hawa viongozi wa Yanga wa sasa hivi wao wameamua kula kona kimtindo huku wakipiga kelele "kanuni" " kanuni".

Hivi walioandaa huo mkutano wangeruhusu hao wazee waulizwe tu maswali je yangepata majibu sahihi au ndio ingeonekana kuwa waandishi wanawaonea hao wazee kwa kuwauliza maswali magumu:-
1. Hivi hao wazee wanamjua aliyeiagiza TFF itoe taarifa mechi iaihirishwe? Je wanajua kazi/mamlaka/cheo chake? Je wanajua ni mwanachama na shabiki kindaki ndaki wa timu gani ukiacha kazi/cheo chake? Je wanajua ni kwa sababu aliahirisha hiyo mechi?
2. Je hao viongozi wanajua kuwa chama cha mpira hakiwatambui wao bali kinawatambua viongozi wa Yanga? Je wanajua kwa mantiki hiyo walipaswa wawasilishe malalamiko yao kwa uongozi wa Yanga ili uongozi uwasilishe TFF kwa niaba yao tena kwa maandishi?
3. Je hao wazee wanajua tarehe ya hiyo mechi ilipangwa baada ya viongozi wa Smba na Yanga kukaa na mamlaka za serikali na kukubaliana kwa pamoja? Na kama jibu ni ndiyo kwa nini wailaumu TFF badala ya kuwalaumu viongozi wao walioshiriki huo mkutano na kukubaliana na maamuzi hayo ya mechi kuchezwa tarehe 3 July?
4. Je hao wazee wanajua ni kwa kiasi gani wanaharibu saikolojia ya wachezaji wa Yanga na kuinua saikolojia na morali ya wachezaji wa Simba ambao kuna uwezekano mkubwa tu Yanga wakaikimbia Simba kwenye mechi ya ligi halafu wakakutana nao kwenye Azama Federation Cup.
5. Je hao wazee wanajua kuwa kuna mechi mbili zilisogezwa muda mbele na Yanga walikubali na wakacheza bila malalamiko ypyote?
6. Na kwakuwa malalamiko yao hayaonyeshi kuwa kuna taarifa rasmi ya maandishi kwenda TFF je wanategemea TFF iwajibu kwa njia gani iwapo TFF inataka kuwajibu.

Yanga sasa hivi ina mdhamini na pesa zipo lakini iwapo haitafanya mabadiliko kwenye uongozi na kupata watu weledi wenye kuujua mpira na siasa zake basi itakuwa ngumu sana kupiga hatua. Na muda wa kufanya mabadiliko ya uongozi na kuweka viongozi imara ni kipindi hiki Yanga inapokwenda kwenye mabadiliko ya mfumo. Wanachama wa Yanga wanapaswa wawe makini sana wakati wa mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wa timu wachague viongozi ambao ni watu wa mpira haswa na si kuchagua kwa mihemuko au ushabiki.
Mkuu nimesoma post yako mpaka nimejisahahu nikadhani ni uzi ..
 
Back
Top Bottom