Wazee wa yanga wakataa kuingiza team uwanjani tarehe 3 july vs simba

njaakalihatari

JF-Expert Member
Feb 12, 2019
4,084
8,661
Wazee wa klabu namba 74 kwa ubora barani africa yanga sc wamekataa kuingiza team tarehe 3 july.Team hiyo ya mitaa ya twiga na jangwani ambayo kwa mujibu wa shirikisho la soka afrika ni ya tatu kwa ubora nchini nyuma ya simba na namungo kikawaida huwa ina utaratibu wa jadi na wa kihistoria wa kusikiliza busara za kamati hiyo ya wazee

Nilichokipenda ni jinsi wazee hao walivyofanya press hiyo huku nyuma kukiwa na official banners za sponsors,ama kwa hakika yanga ni team kubwa inayoendeshwa kiuweledi bila janjajanja
 
Yanga wanastress kila pahala.
Wasipoingiza timu iyo tarehe July 3 wakatwe points wawe nafasi ya tau huko.
 
Yanga wanastress kila pahala.
Wasipoingiza timu iyo tarehe July 3 wakatwe points wawe nafasi ya tau huko.
adhabu ni kushushwa madaraja mawili inashangaza kwamba wanadhani simba alisogeza mechi kumbe ni mwanachama mwenzao waziri bashungwa
Ila hii mechi ni wazi utopolo wanaiogopa sana unajua hili tamko limetolewa officially kuna banners kabisa nyuma za wadhamini
Hawa wanatangulizwa tu ila uongozi uko nyuma ya hii issue
 
Wazee wapo mbele ya banners za Club maana yake wana baraka za uongozi na mfadhili wao.

Jiulize kama ni malalamiko kwa TFF kwa nini wakatae mechi ya Simba Sc na sio mechi zote zilizobaki

Hivi hawa watu wanaosajiliwa Yanga wanafanya uchambuzi kujua going concern na stability ya hii club?
 
Wazee wa Simba kina Hans Pope na Magori wanaleta vyuma hatari.Wazee wa Simba kina Kova wananyoosha kina Mkude wawe na nidhamu. Hii ndio tofauti
 
Hawa wazee wangekua na akili wangeomba kugawana point na sio kupewa point zote 3. Vinginevyo waeleze kosa la simba ni lipi kiasi kwamba wao wasipate point.
 
mwneyekiti wa yanga akiwashukuru wazee wa yanga baada ya tamko lao ambalo litasaidia kumuepusha na kipigo cha bao 8 hapo july 3..tusiwacheke uto BORA LAWAMA KULIKO FEDHEHA
Capture.PNG
 
Utopolo bhana hata hayafikiri. Kuendelea kugoma kucheza hiyo mechi ni kuigomea serikali maana tangazo la TFF lilisema kuahilisha mechi ilitokana na maagizo kutoka wizara ya michezo.

Bila serikali utopolo sio timu ya mpira bali riadha maana serikali ikiagiza viwanja vyake kuanzia vya mashuleni visiguswe utopolo mtafanyia wapi mazoezi au ligi mtachezea wapi? Kwa nini kuwa rigid wakati huna chochote cha maana unachomiliki?
 
Wakati mwingine tuwaheshimu wazee wetu tuwaache wapumzike kuliko kuwaingiza kwenye mambo kama haya. Na wa kulaumiwa ni viongozi wa Yanga kwani hii "move" ilianzishwa na Bumbuli "script" ikawa imekosewa. Sasa wamekosea zaidi baada ya kuwatumia wazee ambao kwa watu wenye uelewa wanaona kabisa wamelishwa maneno matokeo yake wanajichanganya katika maelezo yao. Yanga kuna ombwe kubwa la uongozi kiasi najiuliza kila siku hivi ilikuwaje watu wa mpira kama wakina Tiboroha, Mkwasa, Sekilojo, Mayay, Mziba, Bin Kleb, Seif Magari, Binda, Chanji na wengineo wakakaa mbali kiasi wakaiacha timu kubwa kama Yanga yenye historia kubwa Tanzania na Afrika ikaingia mikononi kuongozwa na watu ambao leo "wanajustify" kukimbia mechi kwa sababu za hovyo za kuaihirishwa mechi. Na ndio sababu watu wachache waliopo sasa wenye weledi kama wakili msomi Simon wanapigwa vita kila leo. Kwa mtu anayezifahamu Simba na Yanga zikikutana hata timu mojawapo iwe dhaifu kiasi gani sio kigezo cha kushindwa na mara kibao timu inayoonekana dhaifu ndio hupata matokeo. Sasa hawa viongozi wa Yanga wa sasa hivi wao wameamua kula kona kimtindo huku wakipiga kelele "kanuni" " kanuni".

Hivi walioandaa huo mkutano wangeruhusu hao wazee waulizwe tu maswali je yangepata majibu sahihi au ndio ingeonekana kuwa waandishi wanawaonea hao wazee kwa kuwauliza maswali magumu:-
1. Hivi hao wazee wanamjua aliyeiagiza TFF itoe taarifa mechi iaihirishwe? Je wanajua kazi/mamlaka/cheo chake? Je wanajua ni mwanachama na shabiki kindaki ndaki wa timu gani ukiacha kazi/cheo chake? Je wanajua ni kwa sababu aliahirisha hiyo mechi?
2. Je hao viongozi wanajua kuwa chama cha mpira hakiwatambui wao bali kinawatambua viongozi wa Yanga? Je wanajua kwa mantiki hiyo walipaswa wawasilishe malalamiko yao kwa uongozi wa Yanga ili uongozi uwasilishe TFF kwa niaba yao tena kwa maandishi?
3. Je hao wazee wanajua tarehe ya hiyo mechi ilipangwa baada ya viongozi wa Smba na Yanga kukaa na mamlaka za serikali na kukubaliana kwa pamoja? Na kama jibu ni ndiyo kwa nini wailaumu TFF badala ya kuwalaumu viongozi wao walioshiriki huo mkutano na kukubaliana na maamuzi hayo ya mechi kuchezwa tarehe 3 July?
4. Je hao wazee wanajua ni kwa kiasi gani wanaharibu saikolojia ya wachezaji wa Yanga na kuinua saikolojia na morali ya wachezaji wa Simba ambao kuna uwezekano mkubwa tu Yanga wakaikimbia Simba kwenye mechi ya ligi halafu wakakutana nao kwenye Azama Federation Cup.
5. Je hao wazee wanajua kuwa kuna mechi mbili zilisogezwa muda mbele na Yanga walikubali na wakacheza bila malalamiko ypyote?
6. Na kwakuwa malalamiko yao hayaonyeshi kuwa kuna taarifa rasmi ya maandishi kwenda TFF je wanategemea TFF iwajibu kwa njia gani iwapo TFF inataka kuwajibu.

Yanga sasa hivi ina mdhamini na pesa zipo lakini iwapo haitafanya mabadiliko kwenye uongozi na kupata watu weledi wenye kuujua mpira na siasa zake basi itakuwa ngumu sana kupiga hatua. Na muda wa kufanya mabadiliko ya uongozi na kuweka viongozi imara ni kipindi hiki Yanga inapokwenda kwenye mabadiliko ya mfumo. Wanachama wa Yanga wanapaswa wawe makini sana wakati wa mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wa timu wachague viongozi ambao ni watu wa mpira haswa na si kuchagua kwa mihemuko au ushabiki.
 
Mtu anaweza akajiuliza ni kwa nini Yanga tu ndio wanakataa kucheza hiyo mechi, kwa nini Simba wenyewe wako tayari kucheza?

Je, Yanga wakicheza wataathirika nini. Kitendo chao cha kutaka kususia hiyo mechi kinafanya wengi waamini kwamba wanaogopa matokeo ya mechi hiyo inaweza kuwa aibu kubwa kwao.
 

Similar Discussions

6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom