Wazee wa "road trip" safari yako ilikuaje 2021/22?

Hahahha niliovertake gari iliyobeba afisa usalama Tanzania nzima sehemu isiyo sahihi sasa nadhani kutaka kuonekana kazi inafanyika mbele ya mkuu ikabidi niwekwe kwanza ndani
Duh,mahabusu tena?we utakuwa Mtata sana mutu ya tarime
 
Yangu/yetu ilikuwa poa sana.

1. Ilianzia 07 Dec 21 alafajiri sana kwa kutoka Namanga via Arusha, Kilimanjaro, Pwani to DSM (was so smooth)
2. Baada ya wiki hivi asbh saa nne j2 fulani baada ya chai nikaenda Dodoma via Chalinze/Moro (hii inilipa kero kutoboa Moro maana malori mengi,buses,mara misafara ya viongozi )
3. Baada ya siku mbili nikanyoosha goti kwenda Tarime kutokea Dom,Via Singida Nzega, Shy-Mwigumbi, Maswa, Bariadi, Lamadi then Tarime (was smooth ride,niliianza sa tisa hivi usiku maana ni safari ndefu,almost kms 800,ukimaliza unaskilizia tako,kiuno na mikono)
4. Then baada ya xmas,nikaingia Musoma mjini kwa siku mbili tatu( haka katrip kapo soft)
5. Then nikaenda Mwanza kutoka Msm (soft trip) na nilala Bunda usiku mmoja.
6. Nikamalizia Mwanza (baada ya kupokea mwaka na kukaa wiki hivi) to Arusha via Shy,Singida,Babati ( Hii trip nzito niliianza alfajiri sana,ila muda karibu wote wa asbh uliliwa na ukungu mzito hivyo kutembea kama bibi harusi, na kipande cha road Mwz - Shy nikibovu,usipokua makini unavunja miguu)

All in all safari kama alivyoshaauri Rrondo katika uzi wake ambao nimeunakili title
1. Uwe na gari zuri lenye uwezo (langu no B lkn bado linauwezo mzuri na comfo ya kutosha, cc 2000 vvti)
2. Kampani nzuri nzuri (nlikuwa na familia,mke na watoto wadogo wanne,jenga picha hapo safari ilikuwaje)
3. Mfuko lzm uwe vzr kwa kweli ( kama 3 mil hivi imekata,tutatafuta ingine)
4. Jumla ya Kms nilizokata kwa mzunguko wote ni 3,506....nyingi ni kwenye lami na kama kms 100 zilikuwa ni rough road)

Ushauri zaidi kama unataka trip yako iwe nzuri,ongeza haya
1. Kwa safari ndefu, lala mapema na uanze safari asbh sana...tisa,kumi sio mbaya kwa mwili unakua na nguvu. Mpk jua linatoka uko mbali. Usinywe pombe kabla ya kulala na wakati wa safari.
2. Weka vituo vya kupumzika hasa wakati wa kunywa chai,lunch,kuchimba dawa,kupiga picha etc. Kama ukiset vzr,utatumia muda huo kuonana/salimiana na ndugu na jamaa kama wapo ktk miji utakayopita, ni kitu kizuri sana. Hakuna haja ya mpera mpera mwanzo mwisho kama umepanda bus,relux furahia safari kama vipi lala kabisa katika miji midogo. Pia unaweza kupiga kamoja,safiii..
3. Usishindane mbio na madereva wengine, tena wasaidie wakuovatake,haina maana kabisa...nimeshuhudia ajali 2,moja nissan wingroad na IST ,Mungu jalia hapakua na vifo ila gari zimeharibika vibaya na safari inakuwa ishakufa hapo. Kuwa na speed muafaka,binafsi nilikuwa sizidi 120 na umakini wa hali ya juu
4.Fuata alama za barabarani,zinasaidia mnooo maisha yako hasa kwa barabara ngeni na kuepusha migongano na askari wetu. Aidha Askari wa barabarani wengine sio wa baya kama tujuavyo,kikubwa ni kuomba radhi pale penye makosa. Na ukiwa na familia wanakuelewa haraka sana hivyo faini huzipati.
5. Service muhimu sana kila baada ya kms kadhaa hasa unapomaliza trip fulani, mbali ya kufungua boneti na kuangalia ya humo, ingiza gari shimoni kagua hata kama husikii shida yoyote...trust me gari inapotembea some nuts,bolts hufunguka,vitu kukatika nk..... Kagua sana tairi, studs na hasa upepo (nashauri kila baada ya km 300).....upepo huongezeka kutokana na msuguano na kupelekea tairi kupasuka na kusababisha majanga makubwa .
6. Be suspicious, jua harufu, sauti na kila kitu cha gari lako, itakusaidia kuepusha hatari nyingi na uharibifu wa chombo. (Kuna wkt kuanzia speed 100 hivi, nikifunga break, naskia sauti ngeni. Kumbe tairi moja ya mbele wkt nafanya service fulani walitoa tairi,katika kurudishia ni stud mbili 2 tu ndio zilifunga na kubana vzr,3 walilazimisha kufunga kumbe hazijakaa ktk njia zake, hvyo licha ya wao kufunga na kuona zimetaiti kumbe hazikufika mwisho:rolleyes:)
7. All in all,muombe sana Mungu kabla ya safari na mjikabithi kwake mda wote, hili la kuzingatia sana.

So far, The trip was sooooo gud...seeing nature when traveling is amaizing....na jana tarehe 05 Jan 22 ndio nimeingia Ar...Naamini kuna jambo utajifunza na litakusaidia. Ofkoz,mimi husafiri mara kwa kwa mara kwani ni kitu nachokipenda hasa self drive. Asanteni Mwanza kwa kuupokelea mwaka mpya hapo, Mwz kutamu sana kwa kweli.

Trip yako ilikuaje?Kms ngapi umemaliza?ulienda wapi na wapi?Please,share nasi tujifunze hata kama ulipata majanga, pole lknsisi tutapata somo,
Asanteni

NB. Kuwa na plan ya trip yako na anza maandalizi mapema, make money kdg kdg naamini utafanikiwa.
View attachment 2069357
Kusafiri na family n Risk sana aiseeee..huwa napenda kupiga road trip alone ..
 
Dec nilisafiri from Dodoma to Chato, nilitoka Dom saa tisa alfajiri then nikaingia Chato saa nane mchana via kahama. Gari ilikua IST, speed ilikua ni 120km/hr na mara chache nilifika 140km/hr japo ile njia ya Singida polisi wengi sana barabarani hadi kero
 
Dec nilisafiri from Dodoma to Chato, nilitoka Dom saa tisa alfajiri then nikaingia Chato saa nane mchana via kahama. Gari ilikua IST, speed ilikua ni 120km/hr na mara chache nilifika 140km/hr japo ile njia ya Singida polisi wengi sana barabarani hadi kero

Safi sana. Lkn sbb ulitoka asbh bila Shaka wengi Walikuwa Hawapo vituoni
 
Umenikumbusha trip nilizokua napiga 2013-15...

Dar-Iringa-Makambako-Mbeya-Sumbawanga-Mpanda then nageuka mpaka Njombe with the same route halafu songea-mbinga-mbamba bay narudia Litui songea then namtumbo-napita milima ile nakamata Tunduru mtamba swala nafika masasi then naibukia tandahimba then mtwara naanza kugeuka mnazi mmoja to Dar es salaam... Total of 5600 km for 2 weeks....

Most of the roads zilikua rough kwa kipindi hicho.

Ingawa mara nyingi nilikua kazini ila nilienjoy
 
Umenikumbusha trip nilizokua napiga 2013-15...

Dar-Iringa-Makambako-Mbeya-Sumbawanga-Mpanda then nageuka mpaka Njombe with the same route halafu songea-mbinga-mbamba bay narudia Litui songea then namtumbo-napita milima ile nakamata Tunduru mtamba swala nafika masasi then naibukia tandahimba then mtwara naanza kugeuka mnazi mmoja to Dar es salaam... Total of 5600 km for 2 weeks....

Most of the roads zilikua rough kwa kipindi hicho.

Ingawa mara nyingi nilikua kazini ila nilienjoy
Duh. Mziki huyo ulikuwa si wakitoto
 
wakuu Nataka nisafiri kutoka Arusha leo jioni mida ya saa kumi na mbili (usiku) naweza pata usafiri hata gari binafsi
 
Back
Top Bottom