Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Sio gari inanuka uvundo.

Gari ikinuka uvundo kuna mengi....
1. Umemwaga kitu cha majimaji hivyo ukifunga vioo na mlango baada ya siku moja kutanuka.

2. Ukimwaga mabaki ya chakula yakaangukia chini ya siti au pembeni yakikaa bila kisafisha gari itanuka.

3. Ukinunua vitu sokoni kama nyama samaki nyanya na mbogamboga zinazolegea na kutoa majimaji na ukaacha yalale bila kuosha gari itanuka.

Vumbi pekee haileti uvundo kwenye gari labda tope lililooza...!
 
Easter long weekend Kasie tunaenda wapi?!! Siku tano zote kweli tusipige trip?!

Hapo ndo huwa nakupenda Taibali.

Tupige trip ambayo sio ya kuchosha (isiwe ndefu sana) ili tufurahie mazingira pia. Tukirudi tuna kandana (massage) kuondoa uchovu wa mikono, mabega na shingo.

Kama daraja/barabara ya Saadani Pangani imekamilika, tupange kwenda Tanga ila tunapita Saadani Parks kisha tunatokea geti la kuelekea Pangani hapo tunaenda Tanga tunaambaa na upepo wa bahari kisha tunarudi via wami msata kisha kiotani 😜.

Just the two of us 😉.

BD6D535D-4C51-4AE0-88D7-9728868BCB55.jpeg


Snacks ntakuwa nazo za aina zote 😋😋.
 
Tip zao ile hela wanayopiga! Nitaanza kutoa tip

Yeah hata mia 5 kwao ni nauli tosha.

Ila mie sitatoa, si unajua hela ya mwanamke ilivyo chungu kutoka 😜😜

Ila huwa nawapigisha story ile ya kumtoa mawazo kama yuko kazini, asiwaze amesimama siku nzima labda kapata short au mwenzie anayetakiwa kumpokea shift kachelewa n.k.

Moja ya story naanzaga nazo ni, naweza kuwekewa mafuta ya buku huku nikionesha taswira ya wasiwasi na kushangaa...!

Wengi hucheka kisha nataja idadi ya lita nnazotaka basi maisha yanaenda.

Mmoja wakati anajaza nikamwambia, shoga hivi kama nimesahau pesa kwenye pochi nyumbani nilitoka haraka nanishaniwekea mafuta inakuwaje....

Basi akimaliza kunijibu hapo namwambia asante kwa huduma namtakia shift njema, akirudi nyumbani awakumbatie watu wake wa karibu kwa upendo. Namuacha na tabasamu halafu mie yuleee naendelea na safari yangu 😊.
 
Hapo ndo huwa nakupenda Taibali.

Tupige trip ambayo sio ya kuchosha (isiwe ndefu sana) ili tufurahie mazingira pia. Tukirudi tuna kandana (massage) kuondoa uchovu wa mikono, mabega na shingo.

Kama daraja/barabara ya Saadani Pangani imekamilika, tupange kwenda Tanga ila tunapita Saadani Parks kisha tunatokea geti la kuelekea Pangani hapo tunaenda Tanga tunaambaa na upepo wa bahari kisha tunarudi via wami msata kisha kiotani 😜.

Just the two of us 😉.

View attachment 1718216

Snacks ntakuwa nazo za aina zote 😋😋.
Daraja bado....Twende mlimani
 
Kuna E class zenye hadi 600 hp.

Mfuko wako tu.
600 HP barabarani si hakuna atae kufatia mkuu.. na hawa vijana wenye BMW X1, X3 watakuwa wanaisoma namba na E zilicho chini yake.. pia nimeziona E 63s AMG .. huu ni moto haswa ndio una iyo 600 HP.. ila shekeli ndio mtihani. Kame hela mboba unachukua hata E 450 au yale V12 Biturbo
 
Back
Top Bottom