Wazee wa Private, IT na malori tukutane hapa

b4theg

JF-Expert Member
May 31, 2011
347
1,184
Habari za leo wapendwa wasomaji, poleni kwa mihangaiko ya hapa na pale na haswa poleni kwa mapambano ya Covid 19.

Mimi ni mmoja kati ya waatumiaji wa usafiri usio rasmi kwa safati za mikoani nikimaanisha malori , gari za IT na gari za watu private, mashirika na hata serikali.

Nimekuwa najikuta natumia usafiri huo tajwa kutokana na muda ninaotaka kuanza safari mabasi yanakuwa yamesha pita yote au nauli pia haija kamilika.

Tabia hii imefanya hata kama nauli imekamilika na mabasi yapo najikuta natamini tu kupanda IT, Private au hata lori.

Nawakaribisha hapa watu wote kila mkoa tuambiane maeneo ya kupandia usafiri wetu huo kwa mkoa ulioko.

Pia tupeane changamoto zinazotokea katika safari za kutumia usafiri huo wa IT, Private na maroli nk.

Naomba kuwasilisha.

Karibuni.

20200626_112828.jpg
 
Kweli mkuu, huwa unasaidia sana hasa ukiwa umebanwa na muda, hivi hata Jumapili hii nimepanga kuondoka DSM saa Moja jioni kwenda Arusha, Hivi gari (Usiku) za Arusha wanapandia sehem gani kwa Morogoro road?
 
Mataa ya kwanza kutokea Ubungo kama unaenda moro hapo utakua watu wanangoja usafiri na madalali. Kikubwa usijikabidhi kwa dalali pambana mwenyewe.
 
Kwa morogoro rd nenda kibo. Japo gari za kaskazini nyingi zinapita bagamoyo rd. Ukikaa bunju au Tegeta kibaoni unapata gari.
Kweli mkuu, huwa unasaidia sana hasa ukiwa umebanwa na muda, hivi hata Jumapili hii nimepanga kuondoka dsm saa Moja jioni kwenda Arusha, Hivi gari (Usiku) za Arusha wanapandia sehem gani kwa Morogoro road?
 
Back
Top Bottom