Wazee wa porini nipe ushauri

Willard Jonnes

JF-Expert Member
Apr 26, 2020
361
750
Wakuu kuna project ambayo ninaenda kuifanya na itaniweke remotely yani maeneo ya vijiji mbalimbali ndani ya nchi sasa nina option mbili za mtandao wa simu Halotel na Airtel, sasa nichague upi interm of coverage ya kawaida tu sio inshu za internet nataka coverage ya kupiga na kupokea simu na Sms.

Nataka ku officialize namba moja kati ya hizo mbili airtel na halotel je mtandao upi ni stable na coverage yake ni kubwa hapa nchini?
 
Tumia Halotel ndio mtandao uliopo zaidi vijijini by the way vijijini ndani kabisa hakunaga mitandao mpaka uende sehemu Fulani....mfano nilikua kijiji cha Namhanga wilaya ya Malinyi mkoani Morogoro. Eneo hilo la karibu na ofisi za kijiji hamna mtandao wowote unaopatikana wala Huduma sijui M-PESA hakuna. Inakulazimu kwenda umbali fulani kutafuta mtandao wa Airtel mingine haipatikani.

Mara nyingi porini hamnaga mtandao mawasiliano ya uhakika huwa ni radio call.. Ama simu zinazotumia satellite badala ya minara... Rediocall hutumika zaidi na vyombo vya ulinzi kama polisi kwa ajili ya kuhakikisha mawasiliano, ukienda mt.Kilimanjaro, Meru , mbugani nk. Kazi za namna hii nazipenda sana mkuu nipe connection
 
Nunua kitochi line mbili jibu utalipata huko porin yafaa nini kutuchosha akili na maswali yako
 
Back
Top Bottom