OMBI: Wastaafu na sisi tunaomba tufikiriwe kwenye tunachopokea

Koryo2

JF-Expert Member
Nov 28, 2016
2,056
2,515
Leo nimesoma kupitia mtandao wa kijamii kuwa Rais ameongeza mshahara kwa watumishi wote wa umma kwa kuongeza 23% kwa kima cha chini.

Ninauliza, Je na sisi Wazee wa pensheni tuko kwenye mfumo huo? Ichukuliwe kuwa maisha yamepanda kwa kila mtu na wengine ile pensheni ya mkupuo tulikwishaimaliza kwa sababu wengi tuna miaka 12 tangu kustaafu.

Kwa sasa tunategemea tu pensheni ya kila mwezi ambayo ni kidogo sana. Mhe. Rais wa awamu ya nne aliwahi kutuongeza kidogo. Mhe. Rais kama na sisi hatukuongezwa basi tunakuomba utufikirie.
 
Leo nimesoma kupitia mtandao wa kijamii kuwa Mhe. Rais ameongeza mshahara kwa watumishi wote wa umma kwa kuongeza 23% kwa kima cha chini. Ninauliza, Je na sisi Wazee wa pensheni tuko kwenye mfumo huo?. Ichukuliwe kuwa maisha yamepanda kwa kila mtu na wengine ile pensheni ya mkupuo tulikwishaimaliza kwa sababu wengi tuna miaka 12 tangu kustaafu. Kwa sasa tunategemea tu pensheni ya kila mwezi ambayo ni kidogo sana. Mhe. Rais wa awamu ya nne aliwahi kutuongeza kidogo. Mhe. Rais kama na sisi hatukuongezwa basi tunakuomba utufikirie.
Pensheni ingekuwa asilimia kadhaa ya mshahara wa mwenye cheo ulichostafia. Kama ilivyo kwa viongozi wakuu.

Amandla...
 
Mhe. Rais tuko Wastaafu wengi tuliostaafu kwa madaraja mbalimbali. Mhe. Rais pensheni yetu kwa kweli ni kidogo kutokana na maisha ya sasa.

Fikiria mtu analipwa Tshs.300,000 kwa mwezi kwa kweli kwa maisha ya sasa ni fedha kidogo hivyo Mhe. Rais na sisi Wastaafu tunaomba utufikirie.

Tumeifanyia makubwa Taifa hili wakati wa utumishi wetu. Nakumbuka kwenye utawala wa Mhe. Kikwete tuliwahi kufikiriwa angalau kidogo.

Tunakuomba sana Mhe. Rais na sisi tufikiriwe tusije tukafa mapema.
 
Back
Top Bottom