Wazee wa Mtama washindwa kuzuia hisia zao kwa Rais Magufuli

Egnecious

JF-Expert Member
Jul 8, 2015
875
960
WAZEE WA MTAMA WASHINDWA KUZUIA HISIA ZAO KWA RAIS MAGUFULI

22 Februari, 2020

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Dkt. Bashiru Ally akiendelea na ziara yake Mkoani Mtwara kuelekea jimbo la Ndanda kupitia jimbo la Mtama, wazee wameshindwa kuzuia hisia zao kwa Rais Magufuli kwa kuonesha nia ya kutaka kumchangia gharama za fomu za Urais mwaka 2020.

Akieleza kwa niaba ya wazee hao, Mbunge wa jimbo la Mtama Ndg. Nape Mosses Nnaye, ameleeza kuwa wazee wapo tayari na wamejipanga kumchangia gharama za fomu za Urais ili kuonesha mapenzi yao kwake kutokana na namna anavyowajali wazee na wananchi kwa ujumla, hivyo wanasubiri kibali kwa Katibu Mkuu.

Wameyasema hayo asubuhi ya leo tarehe 22 Februari, 2020 katika ufunguzi wa shina la Wakereketwa la Kambarage jimboni Mtama.

Katibu Mkuu pamoja na mambo mengine, akifafanua uamuzi huo wa wazee, ameeleza kuwa, nia yao ni njema na imekuwa matamanio ya wazee wengi kufanya hivyo kama wao wa Mtama, amepokea nia yao njema lakini kikubwa wao waendelee kumuombea Mhe. Rais afya njema ili awatumikie zaidi bila kuchoka.

Katibu Mkuu yupo Mkoani Mtwara kwa ziara ya kikazi ya siku tatu, yenye lengo la kuendelea kukirejesha Chama kwa wanachama

Imetolelewa na;
Said Said Nguya
Afisa Habari
Ofisi ya Katibu Mkuu
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aisee kiongozi wetu ni Malaika!....yani watu wote ambao wapo katika mkusanyiko au wakutanapo na viongozi wa chama wanamuunga mkono asilimia mia moja point zero!

Tanzania tumebarikiwa!
 
Wazee gani wa Mtama ambao wanataka kuchangia hela? Mbona karibia wazee wote maarufu walihamia Chadema na Suleiman Methew Luwongo mwaka 2015? Wazee pekee ambao walibakia CCM ni Mzee Nyale na Kibwana na sasa hivi amebaki mzee Kibwana baada ya Mzee Nyale kufariki.

Nape aache maigizo yasiyo ya msingi na kujipendekeza, ingekuwa wa Chadema sawa, lakin hata hao hawawezi kufanya huo ujinga kwani wanadai fedha zao za Korosho tangu mwaka juzi.

Nape na CCM wenzake wangeshughulikia kwanza hili tatizo pale Likolombe
Screenshot_20200221-222222_Instagram.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizi drama zitatufikisha kwenye korongo ambalo kamwe hatutaweza kuchomoka.

Kati ya majimbo ambayo watu wake wana haki ngumu ya maisha ni pamoja na jimbo la Mtama.

Nimewahi kufanya kazi kwenye halmashauri ya wilaya ya Lindi ambako jimbo hili lipo. Wananchi ni maskini wa kutupwa. Wanaishi kwa kutegemea mlo mmoja kwa siku, wanawezaje kuchangia Meko pesa kwa ajili ya kuchukua fomu ya ugombea?

Nimetembea vijiji lukuki vya jimbo hili ikiwa ni pamoja na Mtama, Nyangao, Nyangamara, Linoha, Ruhokwe, Kiwalala, Mahumbika, Mnolela, Mtumbya, Nyundo I, Chiuta na vijiji vingine kibao.

Acheni siasa za kuongopa nyie maCCM.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siasa ya Tanzania tamu sana

2015 Wazee wa Bagamoyo walikusanywa wakaletwa Dar es salaam wakalipwa posho ya 1 million kila mmoja lakin wakatakiwa katika hizo 1 Million zao ni laki 4 tu na zile sita kila mmoja kapewa ili akifika Dodoma wamuombe Mzee mmoja Maarufu sana wakati huo akagombee Urais

Zikakodiwa Coster pale Biafra Kinondon zikawapeleka Dom

Kule Dom nako yakaandaliwa Mpaka mahema na Ambulance ya dharura ili wakati anaombwa Mzee Akagombee wengine wajidondoshe japo la kujidondosha halikitokea

2011 kule Mkoani Tabora kuna Mbunge aliita Wapiga kura wake bila ya kuwapa Agenda, na walipofika akatangaza kujiuzulu Ubunge, basi kuna Watu wakadondoka na kuzimia kwa huzuni na wengine pale pale wakanyanyua Mabango kuomba asijiuzulu


Siasa ya Tz raha sana , Wakazi wa Mtama Mkoani Lindi wanajitokeza kumnunulia fomu ya kugombea Rais wakati wala Keki ya Taifa kule Masaki na Ostybay hawana fedha hizo za kumnunulia fomu Rais

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huko kusini yaani Chadema imepukutika kabisa .
Mifisiem inazunguka nchi nzima kufanya siasa wakati imewafunga midomo vyama vingine halafu bado inajivunia kwamba vyama vingine vimepukutika.Hebu waache na vyama vingine vifanye siasa ili tuweze kupima!
 
Egnecious,
Maigizo ya kijinga kabisa yameanza. Kilio chote cha korosho eti leo ndio wamchangie pesa za kuchukua form? Acheni kuwatumia wananchi masikini kwaajili ya kujikweza kisiasa.
 
Back
Top Bottom