FaizaFoxy
Platinum Member
- Apr 13, 2011
- 92,881
- 109,191
Leo nimezikuta habari za Mzee wa Madrassatul Abraar ambae pia ni member wa JF kwenye group la kuwezeshana ujenzi zilizonifurahisha sana na nikajiuliza, hawa wazee wa Madrassa wamempiku hatua moja Mama Samia Suluhu?
Mama Samia Suluhu juzi alipokuwa akiwaapisha Makatibu Tawala alisema "asilimia 46" ya aliowaapisha ni wanawake. Mama alinifurahisha sana sana kuona kuwa hatutupi wanawake wenzake.
Kilichonifurahisha zaidi ni habari iliyotumwa leo kwenye group la whatsapp na telegram kuwa wazee wa madrassatul Abraar ni muda sasa wameanzisha mpango wa kuwawezesha wanawake kabla ya Mama Samia Suluhu. Wanawawezesha kwa kuwwfundisha fani na taaluma mbali mbali za kazi kwa vitendo, hata mtaa wao unaitwa Vitendo.
Ya leo waliotuma ilikuwa ni kina mama waliojifunza ujenzi kuanzia hapo hapo Madrassatul Abraar, msimamizi wao (Mke wa Mzee wa Madrassa) yeye pia kajifunza usimamizi wa ujenzi hapo hapo Madrassa na mteja wa nyumba wanaoijenga ni mwanamke pia.
Mwenye nyumba hiyo pia nampongeza sana kwa kujitolea kuwakabidhi ajengewe nyumba yake kwa roho nyeupe kina mama hao ambao bado wanapata uzoefu wa ujenzi. Chini ntapandisha video clip.
Hongereni sana wazee wa Madrassatul Abraar, Hongera Bi Samira uliejitolea ujengewe bila hofu ili kina mama wenzio wapate uzoefu,
Jioneeni team ya kina mama ikiwa kazini...
Waandishi wa habari mko wapi mambo mema kama haya yanafanywa na wazee wa madrassa hamyatangazi? Hawa Madrassatul Abraar nimepitia hapa JF nimeona wamebuni mpango wa kuwezeshana wanaouita Nyumba kwa Wote ambao wanatamba kuwa haujawahi kutokea duniani, cha kushangaza si wanasiasa si waandishi wa habari wanaokwenda kuona mipango hii ambayo wangewawezesha hawa wazee ingefanywa kitaifa kabisa tena kwa ufanisi mkubwa kabisa.