Wazee wa fursa nini kinaendelea kwenye matikiti?

Alvajumaa

JF-Expert Member
Jul 5, 2018
4,951
6,065
Wakuu
Juzi kati hapa narudi kutoka kibaruani nikaamua nichukue matunda kidogo,
Nilistaajabu sana bei ya tikiti moja ni Tsh 10,000/-, hivyo kutokana na ukata nikachukua ya elfu 2 tuu ila vilitoka vipande viwili tena vikubwa tuu,
Nipo kwenye daladala nikajiuliza kama tikiti moja ni Tsh 10,000/- sokoni hivyo shambani itakua si chini ya elfu 5 ,
Binafsi nina shamba lakini nalima mazao mengine kabisa si matikiti, je wazee wa fursa hii imekaaje kwenu?
Kwanini matikiti yamepanda sana bei?
 
Ni ulanguzi unaofanywa na madalali masokoni...hustle na taabu anayoipata mkulima wa tikiti ( hata na mazao mengine perishable) na bei anayolipwa shamba unaweza jikuta unalaani..yataka uvumilivu wa kiwango cha juu kama Hayati Madiba alipokuwa gerezani.
 
Kilimo cha matikiti hustawi sana wakati wa kiangazi ukanda wa kaskazini Kilimanjaro na tanga huhitaji maji ya kunyesha kwa kisima hustawi zaidi mbegu unanunua gram 100 zinatosha kwa heka inategemea na mbegu nazujua mm zinauzwa 175,000 ni Edeni f1 unatoa tani za kutosha maana kama umekodisha hadi kuvuna unaweza tumia mil 1 hvi
 
Eden c mbegu ya nyanya
 
Kwa sasa tikiti ni adimu ndo maana bei ipo juu kidogo, kufika mwezi wa tisa na wa kumi tikiti itakuwa nyingi mtaani
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom