Wazee wa East Africa wazua tafrani jijini Dar

Hii ni nchi yenye AMANI, UTULIVU NA MSHIKAMANO na watu wa nje wanatuangalia kwa jicho la husuda.

Bwahaha aaaaaaa!!! ...jicho la husuda!!! Duh!

Nilikuwa naangalia ile hotuba ya Mlm Nyerere pale Kilimanjaro Hotel; kuna wakati alielezea jinsi tunavyochagua viongozi kutumia pesa; yaani kama alikuwa antabiri, ndo yale yale tunayoyaona sasa katika CCM!! Duh!!
 
You can not solve the problem at the same level it was created. Tatizo limewashinda maana hawana new ideas za kulimaliza. Inawezekana wamekuwa wanalipa hao wastaafu ila hela zinaishia kwa watu wasiokuwa wastaafu halali wa EA.
Hata hivyo kwa upande wa pili, hawa wazee miaka yote hii si wangelifanya kazi nyingine na kupata zaidi ya hela hizo wanazodai?

Hao wazee wanadai haki yao na wala sio huruma kutoka kwa watawala, kwa hiyo hata ikichukua miaka 100 waache wadai tu
 
Ni jambo la kushangaza sana ila cha hajabu wao wao Wazee watakuwa wa kwanza kupigia kura Wagombea kutoka CCM.
 
Eti maisha bora kwa kila mtanzania.....jamani sometimes tufanye mambo kwa kumuogopa Mungu. Umekalia haki zao kwa miaka yote hiyo, then unasema Maisha Bora Kwa Kila Mtanzania. Shut the f%^&#ing hole. Kama unashindwa kulipa HAKI ya mtu, wawezaje kulipa hizo AHADI LULUKI?

3.jpg


1.JPGj.JPG


11.JPG


9.JPG


5.jpg
 

Attachments

  • EAC2.jpg
    EAC2.jpg
    81.9 KB · Views: 22
  • EAC3.jpg
    EAC3.jpg
    73.1 KB · Views: 21
  • EAC.jpg
    EAC.jpg
    31.1 KB · Views: 22
  • EAC4.jpg
    EAC4.jpg
    26.5 KB · Views: 22
  • EAC5.jpg
    EAC5.jpg
    48.8 KB · Views: 23
Wana ndugu nimepita hapo nje ya Mahakama kuu jijini DSM naona kuna polisi wakiwa katika jezi na lundo la wazee wa East Africa wakiwa hapo,huku sura zikiwa zakinyonge,
kama kuna mdau ambaye yuko eneo hilo anaweza kutuelimisha kinacho endelea,tutashukuru(nitashukuru)
asante

Yeye uliyepita hapo ulipaswa kutuelimisha kinachoendelea.
 
Kwa mateso yale niliyoyaona inatia uchungui sana. surprizing enough they will go to vote for the one who humiliate them.
 
Wazeee%281%29.jpg

Mmoja wa wastaafu wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) akiwa amekaa katikati ya Barabara ya Kivukoni Front jijini Dar es Salaam wakati wakipinga kujitoa kwa Jaji wa Mahakama Kuu, Njengafibili Mwaikugile kusikiliza kesi yao kwa kile alichosema kuwa hatatenda haki kwa kuwa ana maslahi nayo.

Wastaafu wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki jana walifunga barabara ya Kivukoni jijini Dar es Salaam, wakishinikiza kusikilizwa kwa kesi yao.

Uamuzi wa wazee hao ambao walikuwa kwa mamia, ulisababisha usumbufu kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam baada ya kukaa katikati ya barabara hiyo mbele ya Mahakama Kuu kwa saa saba.

Wazee hao walichukua uamuzi huo kwa kutoridhishwa na maamuzi ya Jaji Njengafibili Mwaikugile aliyekuwa akisikiliza kesi yao kujitoa kwa maelezo kuwa ana maslahi nayo.


Pia, wastaafu hao mbali na kufunga barabara, waliwateremsha abiria katika mabasi yote yaliyokuwa yakitoka Posta kwenda Kivukoni pamoja kuzuia magari binafsi yaliyokuwa yanapita kando kando ya eneo hilo huku wakiimba "tunataka haki yetu" na wakati mwingine wakisema "bora tufe."

Hali hiyo ililazamisha magari yaliokuwa wakielekea Kivukoni, Ikulu, Posta ya Zamani na kwingineko, kutumia njia zisizo rasmi.

Pamoja na wazee hao kuifunga barabara, askari wa usalama barabarani waliingilia kati na kuyaelekeza magari hivyo kuepusha uwepo wa msongamano.

Wastaafu hao walitaharuki na kuchukua hatua hiyo baada ya Jaji Mwaikugile kujitoa kusikiliza kesi hiyo ambayo ilifikishwa mahakamani hapo kwa ajili ya kutajwa.


Jaji Mwaikugile alisema anajitoa kusikiliza kesi hiyo kwa kuwa ana maslahi nayo na kwamba akiendelea kusikiliza haki haitatendeka.

"Kwa mujibu wa taratibu, hakimu au jaji andapo akiona kesi anayosikiliza ana maslahi nayo ili haki itendeke analazimika kujitoa… mimi najitoa kusikiliza kesi hii baada ya kusikiliza kwa muda mrefu na kwa uadilifu mkubwa na bila matatizo kwa kuwa nina maslahi nayo, naona sitatenda haki," alisema kabla ya kuahirisha kesi hiyo saa 3:25, jana asubuhi.

Aliongeza: "Kesi imekuwa mbele yangu kwa muda mrefu, nimeiendesha kwa nia njema bila maslahi yoyote," alisema na kuongeza: "Ikionyesha jaji ana maslahi yoyote katika kesi anayoisikiliza, inampasa ajitoe mwenyewe, asisubiri kutolewa… leo natangaza kesi hii nina maslahi nayo na hivyo najitoa."

Baada ya uamuzi huo wawakilishi wa wastaafu hao walioingia mahakamani akiwemo wakili wao Jotham Lukwaro, walitoka nje na kuwapa taarifa wastaafu wengine waliokuwa nje ya mahakama na ndipo vurugu zilipoanza na kutanda barabarani wakipiga kelele.

Ilipofika 3:30 hali ilibadilika gafla baada ya wastaafu hao kumiminika barabarani ambapo walizungusha mawe makubwa yaliyokuwa pembeni ya viunga vya mahakama hiyo kwa ajili ya kuweka uzio wa kuzuia magari yasipite eneo hilo.

Wastaafu hao waliendelea kulalamika huku wakimuomba Rais Jakaya Kikwete kufika katika eneo hilo kuwatatulia tatizo la kulipwa mafao yao ambalo limedumu kwa muda wa zaidi ya miaka 30 sasa.

Ilipofia saa 7:13 mchana, baadhi yao wenye imani ya dini ya Kiislamu walianza kuswali katikati ya barabara hiyo huku wengine wakiwa wanasisitiza kuwa hadi Kikwete afike kuwasikiliza la sivyo wasingeondoka kwa kuwa Kikwete ndiye mwenye uamuzi wa mwisho.


Wakati hayo yote yakiendelea, polisi walizagaa maeneo hayo kuhakikisha amani inakuwepo.

Mwandishi wa NIPASHE aliyekuwa eneo hilo, ilishuhudia ofisa mmoja wa jeshi hilo ambaye alifahamika kwa jina moja la Mutafungwa, akijaribu kuwasihi wastaafu hao, lakini hakuna aliyemsikiliza badala yake walisikika wakisema "tunataka hela zetu, hatuelewi mtu hapa."


Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Amiri Msumi, aliwambia waandishi kwamba mvutano huo hauna sababu kwa kuwa ulitokana na wastaafu hao kutokuelewa amri iliyotolewa na mahakama.

Msumi alisema kesi yao ilishakwisha na kwamba iko katika hatua ya utekelezaji kwa kuwa amri ilitoka ikitaka walipwe madai yao.

Alisema lakini wao wenyewe wamegawanyika na kwamba kuna mvutano kati ya makundi mawili tofauti.


Alisema Julai 27, mwaka huu, Jaji Mwaikugile alielekeza wawasilishe maombi ya pamoja kuhusiana na tofauti zilizoko kati yao.

Alisema Septemba 27, mwaka huu, jaji alikuwa na udhuru na mawakili wao waliomba muda wa nyongeza kwa ajili ya kuandaa maombi hayo.

"Kwa kuwa shauri niliahirisha mimi sikuwa na mamlaka ya kusikiliza maombi yao zaidi ya kupanga tarehe… nilipanga kesi ije leo (jana), lakini kabla jaji hajasikiliza maombi yao, alijitoa kusikiliza kesi hiyo na kurejesha jalada kwa Jaji Mfawidhi ili ampangie jaji mwingine wa kusikiliza," alisema Msumi.

Ilipofika saa 7:45 mchana, Msajili wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Francis Mutungi, akifuatana na Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Charles Kenyella, na Mkuu wa Upelelezi (RCO), Duwani Nyanda walizungumza na wastaafu hao, lakini juhudi zao hazikuwashawishi wazee hao kuondoka barabarani.

Hata hivyo, jalada la kesi hiyo lilipangwa kusikilizwa na Jaji John Utamwa ambaye aliiahirisha hadi kesho ambapo atasikiliza maombi yao.

Kufuatia hatua hiyo, wakili Charles Semigalawe wa wastaafu hao akiwa amefuatana na Kamanda Kenyella, aliwasihi na kuwajulisha wateja wake hatua iliyofikia kwenye shauri lao, baada ya jaji wa kwanza kujitoa kusikiliza kesi hiyo.

"Jamani kama hamuwezi kuniamini mimi mnadhani nani atawasaidia, naomba tuondoke hadi keshokutwa (kesho) ambapo kesi yenu itasikilizwa na Jaji Utamwa," alisema Semigalawe.

Hata hivyo, walisikika wakisisitiza kwamba watalala katika eneo hilo hadi watakapolipwa fedha zao.


"Naombeni tuondoke mahali hapa kama wakili wenu alivyowaeleza hatua mliyofikia ni nzuri… sisi polisi tuko hapa tangu asubuhi kuhakikisha amani inaendelea hatuna ugomvi na mtu nawapeni dakika 15 mtawanyike ili magari yaweze kupita," alisema Kenyella.

Wakati Kenyella akitoa amri hiyo ilikuwa saa 9:57 alasiri na ilipofika saa 10:06 wastaafu hao walifungua barabara na kuruhusu magari kupita kama kawaida.


CHANZO:
NIPASHE
 
Jioni hii wazee jumuiya walioamua kulala mahakamani wanatimuliwa na wanapigwa virungu na vijana wa Afande tossi (FFU) walio mjini ni mshikemshike
 
Wazee hawa wamemwagiwa maji yenye pilipili na wametawanyika muda si mrefu.

Sijui hii amri ya kuwamwagia maji imetolewa na nani.
 
Wazee hawa wamemwagiwa maji yenye pilipili na wametawanyika muda si mrefu.

Sijui hii amri ya kuwamwagia maji imetolewa na nani.

wanasubiri giza liingie maana mchana ni aibu kuwamwagia maji ya upupu wazee wa watu. Hawa ndio waliosafirisha barua zetu kwa wazazi na kuomba kazi vyo na shule, ndio waliotupakia kwenye treni meli basi ( tukienda shule ) na ndege, ndio waliopeleka pamba katani kahawa na chai yetu nje ya nchi leo tunawapiga virungu sio laana hii?????
 
Wamewamwagia maji ya kuwasha usiku huu hata ITV kwenye news za saa mbili usiku wameonyesha kikojozi (gari la kumwanga maji ya kuwasha) kikiwashughulikia kikamilifu hao wazee
 
WANAJF

Nimeona kwenye taarifa ya Habari kuwa Wazee wa EAC walikuwa wameziba barabara karibia na mahakam kuu.

FFU mida ya saa moja wametawanywa kwa kumwagiwa maji ya kuwashwa

Mwenye habari zaidi jamani

source :ITV news

mytake

serikali inajitafutia rahaana huu sio uungwana
 
Nilikuwa narejea home napiga moja moja. nilipokuwa nakatiza ofisi ya Haki za binadamu Opp. na ukuta wa ikulu nilishihudia defender tatu zizizosheheni wajukuu wa hawa wazee wakiwa wamejiandaa kikamilifu pamoja na kikojozi (gari washawasha). Sikujua kama kule kivukoni front kuna wazee wamezinga njia.

Nilipofika ofisi za takwimu nilishuhudia kweli wazee wameketi chini wamefunga barabara na hakukuwa na vurugu yeyote. Ila ile taswira ya wale wajukuu kule pembezoni mwa ikulu nikahisi kuwa wanaandaliwa mtego mbaya. Nilijaribu kuwasogelea na kupata mawasiliano na mmoja wa viongozi wao ambaye nilimpigia akanieleza kuwa wanapigwa danadana kwani leo wamepewa Jaji mpya ambaye amesema analisoma file ili waje tare 29 kwa P. H (Pre Hearing) na kesi itaanza tarehe moja oktoba. wazee wakagoma kuelewa wakaamua kuzinga njia mpaka kieleweke. wazee wanadai chao since miaka 32 iliyopita.


Niliamua kuvuta subira na kupanda sehemu ndefu kuangalia kinachoendelea. walah sikuamini macho yangu, kwani muda wa saa moja kasoro jioni lile gari la kikojozi lilikunja kona kali na kuanza kuwashambulia wazee kwa maji washa na wakifuatiwa na difenda wakipiga bomu za chozi. Masikini wazee wa watu walihamanika wakaanza kutawanyika to posta ya zamani wengine to ferry. lakini kote huko kikojozi liliwafata na kuwabaruza na maji ya kuwasha. ilikuwa giza giza sikuweza kuona casualties. Nilimpigia mzee kiongozi wao anieleze kama kuna taarifa yeyote ya member wao kuumizwa, hakuweza kuongea bali alikuwa analia na kusema kwamba hawa vijana wameamua kutudhulumu haki yetu na wanatupiga danadana mahakamani. wanasema kwamba uvumilivu wao ndio umewafikisha hapo, hawakuwa na silaha wala nia ya kihalifu bali kushinikiza wapate stahiki zao.


MY TAKE

Kama kusanyiko la wazee hawa lilikuwa ni jinai basi kwa nini wasikamatwe na kufunguliwa mashtaka?
Nahisi kwamba polisi hawakutaka kuwatenda vile, lazima kuna amri imetoka mahala kwamba washughulikiwe ili kusafisha njia.
Watanzania tuweke serikali inayojali watu wake hapo oktoba 31. dhuluma na hujuma zimezidi sasa
 
Kwenye kile kikao cha changanya na zako ohh mbayuwayu si walikua wazee hawa hawa au wako wengine? changanya na zako:A S thumbs_up:
 
Watumie nguvu yao ya Kidemokrasia kuwanyima kura hao Jamaa ifikapo Jumapili ya Oktoba 31.Kila Mtanzania ana haki ya kusikilizwa na kupewa haki ya kusikilizwa...Hiyo ni haki yake ya kikatiba!.
 
Back
Top Bottom