Wazee wa Dar wasema Chadema waingepaswa kwenda mahakamani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wazee wa Dar wasema Chadema waingepaswa kwenda mahakamani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zak Malang, Jan 10, 2011.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Jan 10, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  [SIZE="3"Kufuatana na taarifa ya Ch 10 usiku huu, wazee wa Dar (ambao wamesema kuwa wanawasemea wazee wenzao nchi nzima -- yaani wameipora hiyo haki bila ya ridhaa yao) kwamba Chadema wangekwenda mahakamani badala ya kufanya maandamano na kutotii amri halali ya polisi.

  Wazee hao ambao wengi wao walikuwa wamevaa baraghashia na ambao baadhi yao wamekuwa wakionekana katika magwanda ya CCm katika shughuli za chama hicho wamesema mahakama ndiyo njia sahihi kuliko vurugu.

  My take: Hivi hawa wazee mbona hawajawahi kuja na kauli za kuwaponda wazee wa Jumuia ya Afrika ya Mashariki kwa kuporwa haki zao ambao wamekuwa wakiandamana mara kadha kwenye mitaa ya Dar na kufanya vurugu?[/SIZE]
   
 2. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #2
  Jan 10, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Hivi hao Wazee ni wale wa kile kile Chama Cha Mauaji (CCM) Tanzania tawi la Dar es Salaam sio?
   
 3. Polisi

  Polisi JF-Expert Member

  #3
  Jan 10, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 2,087
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Rekebisha heading iwe ' wazee wa kiislam Dar wasema CDM wangekwenda mahakamani'.
   
 4. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #4
  Jan 10, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,274
  Trophy Points: 280
   
 5. Limbani

  Limbani JF-Expert Member

  #5
  Jan 10, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 1,438
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Hao ndio wale wazee waliokuwa wanashangilia wakati kikwete akiita wafanyakazi MBAYUWAYU!!?? Pumbavu hao njaa inawasumbua...
   
 6. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #6
  Jan 10, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Hivi wazee hao wanajua kwamba mahakama ni haki ya Chadema na kuandamana pia ni haki ya Chadema -- vyote hivyo vimewekwa katika Katiba?
   
 7. p

  politiki JF-Expert Member

  #7
  Jan 10, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  ccm inajua wazi kuwa kanuni zilikiukwa kwenye uchaguzi na walikuwa wanajuwa kuwa wakifanya hivyo kitakachotokea ni kwamba chadema itakwenda mahakamani ambapo wao wana control kila kitu kuanzia jaji gani asimamie kesi na kesi hiyo ianze lini kwani wao ndio wanaotoa pesa za kugharamia kesi hizi kumbuka kesi ya mnyika ubungo iliairishwa kwa miaka mitano na haikusikilizwa. Hawa wazee wameuvamia mtego wa ccm ambao chadema imeukwepa. Ogopa mtu anayevunja sheria mchana kweupe ujue wazi kuwa kuna kitu anachokitegemea kinachompa jeuri ya kufanya hivyo.
   
 8. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #8
  Jan 10, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Walinusishwa ugoro hadi sauti zao zilikuwa na mikwazuro kama kengele ya guta.
   
 9. S

  Sumuni Member

  #9
  Jan 10, 2011
  Joined: Feb 19, 2009
  Messages: 59
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naungana nawe matola. Hawana hadhi ya kujadiliwa hapa kwa kuwa ni watu wa kutumwa na wasiojua nini wanachokifanya. Hawaju kuwa ni haki ya chadema kuandamana na kulalamikia ukiukwaji wa haki kama ilivyo haki kwenda mahakamani. Hawajui kama chadema wanajua kuwa baadhi ya mahakimu wamenunuliwa na CCM na watakachokifanya ni kupiga danadana ilihali muda unakwenda. Anyway, hatuhitaji kuwajadili wachovu hao.
   
 10. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #10
  Jan 10, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Wazee wa Dar wako sahihi.

  Kuhusu haki ya wazee wa Afrika Mashariki, aliyewapora haki yao ni Mtakatifu to be Nyerere, au hilo utalipinga.

  Kikwete akalimaliza la hawa wazee, wakasema hawajaridhika wameenda mahakamani, kwa hiyo tungoje sheria ichukuwe mkondo. Kati ya hao wazee wa Dar. uliowaona leo wengine walikuwamo katika jumuiya ya Afrika Mashariki.
   
 11. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #11
  Jan 10, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Hawa pambaffff sana. kama ni watu wenye uchungu wa nchi hii na amani yake kwa nini wasitoe kauli kali ya kupinga ufisadi uliokithiri ndani ya serikali, na hasa kupinga suala la kulipa Dowans?

  Hawajui nchi hii inaelekea kutumbukia katika vita vya wenyewew kwa wenyewe kutokana na utawala mbovu wa CCM, ufisadi, na kutowajibika. sasa hivi baadhi ya viongozi katika CCM na serikali wako kivyao -- serikali na CCM hawana kauli moja kuhusu ufisadi (Dowans), Katiba mpya, vurugu za Arusha etc etc,

  Wazee hawalioni hilo?
   
 12. M-mbabe

  M-mbabe JF-Expert Member

  #12
  Jan 10, 2011
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 4,990
  Likes Received: 3,739
  Trophy Points: 280
  Hapana, Polisi.....hapo nadhani unapotoka kidogo.

  Ukitumia sentiments za udini, unajiondolea sifa ya kuwa-criticize hao wazee kwa vile una-replicate walichokifanya wao!
  By the way mimi ni Mkristo, lakini ni Mtanzania zaidi..
   
 13. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #13
  Jan 10, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Hawako sahihi wametumwa. Madai dhidi ya serikali huwa si ya rais anayehusika, bali serikali iliyopo, kwani marais hupita tu. Wazee wa EAC walilipwa kihuni kama vile serikali ya CCM huwalipa kihuni wanavunjiwa nyumba zao nk.

  Kweli wamekwenda mahakamani -- lakini huko ni uhuni mtupu -- danadana nyingi.

  Halafu hawa wazee (waliotoa kauli dhidi ya Chadema) kwa nini daima huwa hawatazami kiini cha suala, hukimbilia kuangalia matokeo (manifestations) yake? Kiini cha suala la Chadema huko Arusha si linajulikana? hawataki kuliona? Basi si bora tu wangesema tu Meya wa CCM alishinda kihalali?
   
 14. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #14
  Jan 10, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,318
  Likes Received: 438
  Trophy Points: 180
  wajumbe wa nyumba kumi..mabalozi wa sisiem,,shameless oldies
   
 15. m

  matawi JF-Expert Member

  #15
  Jan 10, 2011
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 2,055
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  January akikaa na babaake wakifikiria kitu wanakitoa kwenye vyombo vya habari kwa kisingizio ni tamko la wazee wa Dsm. Mtadanganya hadi mtachoka
   
 16. Monstgala

  Monstgala JF-Expert Member

  #16
  Jan 10, 2011
  Joined: Aug 25, 2009
  Messages: 1,081
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Makubwajinga!
   
 17. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #17
  Jan 10, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Katika mwanzoni mwa miaka ya 90 Mwinyi alifanya kampeni ya 'kuwauzia' wananchi sera yake ya kuwataka wazazi kuchangia elimu ya watoto wao. Katika mkutanommoja wa ndani na wazee wa Mbeya, wazee hao walikuwa wakimpigia makofi na kushangilia kila alipokuwa akimaliza sentensi kuelezea sera hiyo.

  Baadaye watoto wao walikuwa wakifukuzwa Chuo Kikuu kwa kukosa kulipia sehemu ya ada. Nadhani waligundua ujinga wao. Wazee wetu hapa nchini hawana busara yoyote -- laiti wangemuekea ngumu Mwinyi wakati ule, leo hii elimu ingekuwa bure!
   
 18. afroPianist

  afroPianist Member

  #18
  Jan 10, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 86
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sidhani kama ni sahihi kusema "wazee wa kiislamu" kwa kuwa tu wamevaa balaghashia, kwani kofia hizo hupenda kuvaliwa na wazee wengi hasa wa Dar bila kujali dini. Kwa kifupi msinase kwenye mtego wa CCM kugeuza mjadala wowote ambao wao wanaonekana kushindwa kwa sasa kuwa ni "vita takatifu ya kidini" dhidi ya kikwete.

  Kimsingi hao ni wazee wa kitanzania ambao wengi wao ni walalahoi lkn kwa kujua au kujokujua wamekubali kutumiwa kuhalalisha upumbavu na ujuha wa CCM. Kwani ni wapi palipoandikwa kuwa haki hudaiwa mahakamani tu? Na je, ni kweli kuwa mahakama zetu sasa ni "wakala wa Mungu mwenye haki" ambaye anatoa hukumu za haki kikamilifu bila upendeleo wa umri, rika, dini, nasaba n.k? Mara ngapi wananchi wanyonge wameporwa haki zao mahakamani huku wakiona mchana kweupe?(rejea hukumu ya mgombea binafsi,kesi za uchaguzi, kesi za kubambikiwa, kesi za vigogo n.k).

  Hata kama katiba imeipa mamlaka mahakama kutafsiri sheria na kutoa haki, katiba hiyohiyo imetoa uhuru wa kudai haki kwa migomo, maandamano, mikutano ya hadhara n.k na kuulinda uhuru wa kujumuika, uhuru wa maoni na haki nyingine za msingi za raia hivyo isiwe ni lazima kwenda mahakamani wakati njia nyingine halali kisheria na zinaweza kutumika.

  Hao "wazee" walipaswa kwanza kukemea matumizi makubwa ya nguvu zisizo lazima dhidi ya wananchi(ambazo pia zilitumika dhidi ya wazee wenzao wafanyakazi wa EAC) lakini kwabahati mbaya hawawezi kuona mbali zaidi ya matumbo yao!
   
 19. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #19
  Jan 10, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Hivi kuna mtu anakumbuka miaka kumi iliyopita wazee hawa wa Dar waliwahi kutoa kauli ya kuwaponda waandamanaji wa CUF kule Pemba waliouawa na polisi walipokuwa wakiandamana?
   
 20. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #20
  Jan 10, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Fuatilia profile zao! Utapata kinyaa! Hapo sio wazee, wenye njaa waliochoka na kudanganyika ili wakane dhamiri zao!
   
Loading...