WAZEE WA CHAMA CHA CHADEMA WATOA ONYO KALI KWA SERIKALI YA MAGUFULI NA JESHI

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,285
24,161
30 September 2020
WAZEE WA CHAMA CHA CHADEMA WATOA ONYO KALI KWA SERIKALI YA MAGUFULI NA JESHI

Huu wa Uchaguzi Mkuu 2020 vyama vimeamua kusimama kidete na kusema basi dhidi ya chama-dola cha CCM Mpya kinachotumia Tume ya Uchaguzi, Wasimamizi wa Uchaguzi na vyombo vingine vya dola kujaribu kuviburuza.

Wazee hawa wamuasa Magufuli kuwa bado ana muda wa kutosha kurekebisha upotovu wa serikali yake, Tume aliyoiteua na vyombo vya usalama ili kurejesha imani ya waTanzania na Jumuiya ya Kimataifa kuwa mchakato mzima wa Uchaguzi Mkuu 2020 utakuwa Huru na wa Haki.
 
Wazee wamekubaliana kuwa yale mazoea ya CCM kupeana miaka kumi kumi mwaka huu basi. CCM Mpya ikubaliane na matakwa ya wananchi Tanzania nzima, kuwa awamu hii ya CCM Mpya miaka yao mitano inatosha na wafunge virago vyao waondoke.
 
Hivi Siro kilugha sio ndio Ziro kizungu?

Hakuna mahali popote Duniani polisi wakatuliza wananchia walioamua! Kama hawezi kutumia akili hata kidogo hafai hata kuwa mgambo!
 
MaCCM yakichezaea Uchaguzi huu, lazima tupasuane matumbo tulane maini wenyewe kwa wenyewe.
#sasabasi
 
Wazee wa baraza hili la Taifa la CHADEMA wameibua mengi katika tamko lao kuhusu utawala huu wa CCM Mpya kushindwa kupiga vita ufisadi, matumizi mabaya ya kodi za waTanzania, kukosekana uhuru na haki katika mchakato mzima wa Uchaguzi Mkuu na hivi vyote vinapingana na kauli ya Rais Magufuli kuwa uchaguzi Mkuu utakuwa Huru na wa Haki.
 
Toka Maktaba
21 January 2020

"TUMEJIPANGA UCHAGUZI 2020 UTAKUWA HURU NA HAKI" MAGUFULI AKIONGEA NA MABALOZI

Hapo mapema mwezi Januari tarehe 21 mwaka huu 2020, mgombea wa CCM akiongea na mabalozi wa nchi za kigeni nchini Tanzania kwa kutumia lugha ya ushawishi kuwa waje kuwekeza Tanzania kwa kuwa kuna mazingira ya uhuru na haki kwa wawekezaji wa nje hata wakiingia ubia na wawekezaji wa ndani ili kujiletea Maendeleo kupitia kipato, Ajira, kodi zitakazolindwa na utawala wa sheria unaoheshimu mikataba
 
IMG_7125.JPG

Dah....mi naona kuna tatizo mahali....
 
Tayari Jumuiya ya Kimataifa inayohusisha wawekezaji, wanadiplomasia, watetezi wa Haki za Binadamu, watalii, Mabenki ya Kimataifa n.k inatilia mashaka hali ya kisiasa na demokrasia nchini Tanzania kama ilivyo pia shaka ya wazee wetu hawa juu ya muenendo na matendo halisi ya serikali ya Magufuli kusimamia kauli za matamko yake ya kulinda uhuru na haki.
 
Wazee wamekubaliana kuwa yale mazoea ya CCM kupeana miaka kumi kumi mwaka huu basi. CCM Mpya ikubaliane na matakwa ya wananchi Tanzania nzima, kuwa awamu hii ya CCM Mpya miaka yao mitano inatosha na wafunge virago vyao waondoke.
Unaona anavyomwita kwa heshima Mh. Rais Magufuli. Halafu anaonekana hana taarifa kabisa eti bajeti ya ununuzi wa ndege haukupitishwa na bunge. Mwambie akasome Fungu la 2006 tangu mwaka wa fedha wa 2016/2017 ataona bajeti ipo ilijadiriwa na bunge!
 
Tayari Jumuiya ya Kimataifa inatilia mashaka hali ya kisiasa na demokrasia nchini Tanzania kama ilivyo pia shaka ya wazee wetu hawa juu ya muenendo na matendo halisi ya serikali ya Magufuli kusimamia kauli za matamko yake ya kulinda uhuru na haki.
Mtanyooka tu nyinyi. Nilifikiri mnategemea watz kumbe wakina Robert Amsterdam?!
 
30 September 2020
WAZEE WA CHAMA CHA CHADEMA WATOA ONYO KALI KWA SERIKALI YA MAGUFULI NA JESHI

Huu wa Uchaguzi Mkuu 2020 vyama vimeamua kusimama kidete na kusema basi dhidi ya chama-dola cha CCM Mpya kinachotumia Tume ya Uchaguzi, Wasimamizi wa Uchaguzi na vyombo vingine vya dola kujaribu kuviburuza.

Wazee hawa wamuasa Magufuli kuwa bado ana muda wa kutosha kurekebisha upotovu wa serikali yake, Tume aliyoiteua na vyombo vya usalama ili kurejesha imani ya waTanzania na Jumuiya ya Kimataifa kuwa mchakato mzima wa Uchaguzi Mkuu 2020 utakuwa Huru na wa Haki.
 
Wakati chakula ukiwa nacho, waweza kulala bila kula na kumshaangaa anayelalamika kulala bila kula kwa kukosa chakula! Hii show ndivyo ilivyo!
 
Back
Top Bottom