Wazee wa CHADEMA wamvaa Mzee Mwinyi, wamtaka Rais kukemea kampeni ya 'urais wa maisha'

Tumaini Makene

JF-Expert Member
Jan 6, 2012
2,642
6,071
CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)

BARAZA LA WAZEE WA CHADEMA

TAMKO LA KULAANI KAULI AU MAPENDEKEZO YA MZEE ALI HASSAN MWINYI YA KUTAKA KUVUNJWA KWA KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

Ndugu waandishi wa habari

Sisi, Baraza la Wazee wa CHADEMA tumeomba kukutana nanyi leo kwa ajili ya kutoa tamko letu hili la kulaani kauli iliyotolewa na Mzee Ali Hassan Mwinyi (Rais Mstaafu) ambayo ilikuwa na lengo la kushawishi kuvunjwa kwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Rais Mstaafu, Mzee Ali Hassan Mwinyi, alipokuwa kwenye swala ya Eid El Fitr iliyofanyika kimkoa katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam alinukuliwa akisema;

"Kama si matakwa ya Katiba ya nchi, uongozi wa Rais John Magufuli ulipaswa kuendelea kuwapo miaka yote…laiti ingelikuwa Katiba iliyopo haikufupisha muda wa uongozi wa rais, ningeshauri Rais Dkt. Magufuli awe Rais wa Tanzania wa siku zote”.

Kauli hii imetusikitisha sana hasa baada ya kusikia na kuona imetolewa na Mzee tena aliyewahi kuwa kiongozi Mkuu wa Nchi yetu kwa miaka 10, ambaye anapaswa kupima madhara ya kila neno analolitamka kwani “imani uja kwa kusikia.”

Ndugu Waandishi wa Habari

Tumeona tunao wajibu wa kuwakumbusha Watanzania kuwa viongozi kama Pierre Nkurunzinza, Robert Mugabe, Joseph Kabila na wengine wa namna hiyo ambao kwa namna mbalimbali na nyakati tofauti wamejaribu au wamefanikiwa kuvunja au kubadili Katiba za nchi zao ili wakidhi matakwa ya kujiongezea muda wa kukaa madarakani, walianza kwa kupata watu walioanza kuwachochea na kuwapigia kampeni na kuwasifia kuwa ni watawala wazuri hivyo wanapaswa kuendelea kuwepo madarakani. Walipofuata ushauri huo, sote tunafahamu matokeo yake kwa yale yanayoendelea katika nchi zao.

Kwa kutambua madhara ya kauli hizo, Wazee wa CHADEMA tumeamua tusikae kimya.

Sisi kama wazee tulijipa muda wa siku kadhaa tukiamini kuwa labda mzee mwenzetu aliteleza ulimi na angeweza kuirekebisha kauli yake ile au Chama chake kingelitoa kauli ya kuweka marekebisho. Lakini hakufanya hivyo na wala Chama chake hakikufanya hivyo na mbaya zaidi Rais Magufuli mwenyewe naye pia amenyamaza kimya kuhusiana na kauli hii.

Kwahiyo tukajua wazi kuwa huu ni mkakati rasmi wa kuliandaa taifa kisaikolojia kuwa na “Mfalme au Sultani” (yaani Rais wa siku zote kama kama alivyopendekeza kwenye kauli yake).

Hivyo sisi wazee wa CHADEMA tunaulaani mkakati huu ovu unaoweza kulitumbukiza taifa letu katika machafuko kama ambavyo imetokea kwa nchi jirani zilizopuuzia kampeni za uchochezi kama huu wa kuvunja Katiba ya nchi ili kukidhi matakwa au matamanio ya mtu au kikundi cha watu wachache wanaotaka kuwa madarakani siku zote.

Mwalimu Nyerere aliwahi kumkemea Mzee Mwinyi kwa swala hili
Sisi wazee bado tunakumbuka vyema, namna Mzee Mwinyi akiwa bado madarakani, wakati anaelekea mwishoni mwa utawala wake yeye na wapambe wake walipenyeza pendekezo hili la hatari la kutaka kuibadili Katiba, ili Rais Mwinyi (wakati huo) aweze kuongoza bila kikomo, lakini Mwwalimu Nyerere akalizima jaribio hilo kwa kukulikemea vikali tena wazi wazi na alikwenda mbali zaidi na kulizungumzia ndani ya kitabu chake cha “Uongozi Wetu na Hatma ya Tanzania” alichokiandika mwaka 1994 ili vizazi vinavyokuja visifanye kosa hilo na akaonya kwa kuonesha madhara yake.

Tutanukuu baadhi ya vifungu katika kitabu hicho:

“Mapema mwezi Disemba 1992, Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM ilikutana Dodoma kwa ajili ya kuzungumzia suala la utaratibu wa kuchagua Makamu wa Rais na mambo mengine mengine. Mimi (Mwalimu Nyerere) nilialikwa nitoe maoni yangu."

"Katika kikao cha faragha cha viongozi wakuu wote wa Chama na Serikali, na wengine wa nyongeza. Rais (Mwinyi) alieleza kuwa mbali ya agenda zilizokuwa zimeandaliwa walikuwa (yaani Mwinyi na wenzake) wamezungumza pia suala la muda wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwepo madarakani. Alieleza kuwa pamoja na kwamba ilikuwa imekubalika muda wa Rais kuwepo madarakani uanishwe lakini ni muda gani akae ulikuwa haujaamuliwaa…”

“Nilishtuka sana kusikia jambo ili linaibuliwa tena ili lijadiliwe upya kwani uamuzi wa vipindi vya Rais kuwa madarakani ulikwishafanyika.”

“Lakini kabla ya hapo baadhi ya viongozi wa chama walikuwa wameanza kampeni za kutaka Rais Mwinyi aongezewe vipindi vya muda wa kuwa Rais zaidi ya ule muda wa vipindi viwili uliokuwa umekubalika. Niliposikia hizo kampeni nilikwenda moja kwa moja kwa Rais na kumsihi azizime kampeni hizo; na viongozi wahusika nilitafuta nafasi nao nikawaomba wasilifufue jambo hili kwani lilikwisha fanyiwa maamuzi na kulifufua upya kungeleta athari kubwa.”

“Sababu ya kuweka ukomo wa muda wa Rais kuwa madarakani utamkwe na uwe ni sehemu ya Katiba, ilikuwa ni kuondoa uamuzi huo mikononi mwa Rais mwenyewe au kikundi chochote cha Chama au Dola…”

“Watawala wetu ni wanasiasa wa kawaida ambao wanapenda sana kutawala hata kama hawana uwezo wa kutawala; na ambao wako tayari hata kuhonga ili wachaguliwe kuwa Watawala, na wakishakuchaguliwa hawatoki bila kulazimishwa. Kwa hiyo ni jambo la busara kabisa uamuzi wa muda wa kuwa Rais ufanywe mara moja, na ukishakufanywa uwe ni sehemu ya Katiba ya Nchi na Uheshimiwe!” Mwisho wa kunukuu.

Sisi, wazee wa CHADEMA tumeamua kunukuu maneno haya ya Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere ili;

Kwanza; kumkumbusha Mzee Mwinyi kuhusu jambo hili kwani tunaona kuwa kiu yake ya tangu mwaka 1992 ya kutaka kuondoa ukomo wa muda wa kutawala kwa Rais bado anayo mpaka leo pamoja na kukemewa na Mwalimu Nyerere.

Pili; tunawakumbusha Watanzania kuwa hatari aliyoiona Mwalimu Nyerere miaka hiyo bado iko pale pale kwani wote tumeshuhudia watawala wengi Afrika ambao wana mawazo ya kidkteta wakiwa wanajiandaa kutawala milele na hatimaye kuziingiza nchi zao katika machafuko ya kisiasa kwa sababu tu ya uchu wa madaraka, hatutaki nchi yetu ielekee huko na kamwe sisi wazee hatutakuwa tayari kuona jambo hili likitokea katika Taifa letu.

Tatu; tunataka kuwakumbusha wazee wenzetu ambao bado wako CCM na huwa kila mara wanajinasibu kuwa wanafuata misingi na miongozo ya Mwalimu Nyerere wakumbuke maneno hayo na wajitokeze hadharani wazi wazi kukemea kauli za Mzee Mwinyi na wamtake aheshimu misingi ya Katiba yetu kama alivyofanya Mwalimu Nyerere kama kweli bado wanamuenzi Mwalimu.

Nne; tunawataka Wazee wa CCM waungane nasi (Wazee wa CHADEMA) kumtaka Rais Magufuli ajitokeze hadharani waziwazi na kukemea kampeni hizi ambazo zinaratibiwa na Mzee Mwinyi na Rais Magufuli aweke wazi kuwa yuko upande gani.

Tano; tunatoa wito kwa Watanzania wote wenye mapenzi mema na wazalendo wa kweli kwa nchi yetu kuupinga kwa nguvu zote utaratibu wa kutaka kuturudisha nyuma. Ni lazima Katiba iliyopo iheshimiwe na hasa katika kipindi hiki cha kutaka Katiba mpya na asiwepo yeyote miongoni mwetu anayetaka kuharibu misingi tuliyokwisha kujiwekea kama taifa kwa kipindi kirefu.

HITIMISHO

Sisi Wazee wa CHADEMA tunaona uwepo wa mwenendo na jitihada za wazi wazi kabisa za kuvunjwa kwa Katiba yetu huku pia tukishuhudia ukimya wa viongozi waandamizi ndani ya nchi wakiwemo wazee wenzetu Marais Wastaafu na waliowahi kuwa makamu wao, na wale wanaopata fursa ya kusema ndio hawa aina ya Mzee Mwinyi ambao wanachochea kuvunjwa kwa Katiba ya nchi yetu.

Katika mwenendo huo, tumeshuhudia Watanzania wakibaguliwa kwa misingi ya itikadi za kisiasa huku vyama vya siasa vikinyimwa kutekeleza wajibu wake kwa mujibu wa Katiba ya nchi.

Tunapenda kuwakumbusha Watanzania kuwa kitendo cha kuvunja Katiba ya nchi yetu ni kosa la uhaini.

Hima wazee tusimame imara katika kipindi hiki na tumuenzi Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere kwa vitendo, hasa kwa kumkemea mtu yeyote yule ambaye anashawishi au anataka kufanya kampeni za kuvunjwa kwa misingi ya Katiba yetu na heshima kubwa ambayo tumejiwekea kama taifa.

Imetolewa leo tarehe 29 Juni, 2017

Roderick Lutembeka

Katibu Mkuu Baraza la Wazee CHADEMA Taifa
 
Hawa wazee wa Chadema kwa hakika wamechanganyikiwa, na wameonesha dhahili walivyo wanafiki, Nilitegemea Wazee hawa Waanze na kulaani Ufisadi wa Wazee walioko Chadema, akina Frederick Sumaye,Kingunge Ngombare Mwiru aliyefisadi Ubungo, Edward Lowasa (Fisadi papa), Mtei fisadi na hujumu Uchumi hadi Nyerere alimtimua kwenye uongozi, Mbowe mporaji na mkwepaji wa kodi hadi bilion Bil.1.6, Mchafuzi wa vyanzo vya maji. Haya ndiyo ambayo Wazee wa Chadema wanapaswa kuyakemea badala ya kuhangaika na Rais Mstaafu Mwinyi, kitendo ambacho ni kumkosea heshima. Ikumbukwe anao Uhuru wa kuongea maoni yake, na maoni yake ni huru. Na Rais wa awamu ya Tano anafanya kazi nzuri sana na atafaa kuongoza hata miaka 50 ijayo. Watz tunamuhitaji sana. Nyinyi Ma-Chadema ni Wasaliti wakubwa, mmenunuliwa na Wazungu (Wezi).
 
Hivi Chagadema ina Baraza la Wazee? Makubwa
 
Mbowe alibadili katiba ya chadema ili aendelee kupiga hela kwa kisingizio cha kukopesha chama. Tumaini Makene na wazee wake hawalioni kama ni issue ili mradi nao wanaambulia makombo.

Kama huwezi kuaminika katika madogo huwezi kuaminiwa katika makubwa.
 
makene, hao wazee walitakiwa kwanza wamvae mwenyekiti, wamwambie ni vizuri kubadilishana vijiti badala ya uenyekiti wa maisha.
 
Kweli nyani haoni kundule. Hawa wazee wakati Mbowe anabadili katiba na kujipa uenyekiti wa kudumu hawakuwa wanamuona? Au walikuwa bado hawajazeeka.
 
Hawa wazee wa Chadema kwa hakika wamechanganyikiwa, na wameonesha dhahili walivyo wanafiki, Nilitegemea Wazee hawa Waanze na kulaani Ufisadi wa Wazee walioko Chadema, akina Frederick Sumaye,Kingunge Ngombare Mwiru aliyefisadi Ubungo, Edward Lowasa (Fisadi papa), Mtei fisadi na hujumu Uchumi hadi Nyerere alimtimua kwenye uongozi, Mbowe mporaji na mkwepaji wa kodi hadi bilion Bil.1.6, Mchafuzi wa vyanzo vya maji. Haya ndiyo ambayo Wazee wa Chadema wanapaswa kuyakemea badala ya kuhangaika na Rais Mstaafu Mwinyi, kitendo ambacho ni kumkosea heshima. Ikumbukwe anao Uhuru wa kuongea maoni yake, na maoni yake ni huru. Na Rais wa awamu ya Tano anafanya kazi nzuri sana na atafaa kuongoza hata miaka 50 ijayo. Watz tunamuhitaji sana. Nyinyi Ma-Chadema ni Wasaliti wakubwa, mmenunuliwa na Wazungu (Wezi).

Nmekosa tusi la kukupa, najua ni madhara ya cc emu so siyo kosa lako. Mnyime elimu bora , mfanye masikini na umpe buku 7 basi uwezo wake wote wa kifikiri utakuwa unamuamulia wew.
 
Hivi Chagadema ina Baraza la Wazee? Makubwa

Uko vizuri kweli kichwani? Una quote uzi wote na kila siku tunapinga hili lakini akili yako ngumu kuelewa kabisa. Ina maana mtu akiwa cc emu ndyo anakuwa na akili kama zako ?
 
Ni kweli kabisa. Hayo nimambo ya msingi ambayo Nyerere aliyasimamia. Kauli kama za Mzee Mwinyi hazina nafasi
 
Nmekosa tusi la kukupa, najua ni madhara ya cc emu so siyo kosa lako. Mnyime elimu bora , mfanye masikini na umpe buku 7 basi uwezo wake wote wa kifikiri utakuwa unamuamulia wew.
umefanya vizuri mkuu kutomtukana kwani mambo haya hayataki hasira bali majibu ya kina tu, yenye kueleweka.

kwa heshima na taadhima, naomba ujaribu kuijibu hoja yake aliyoigusia angalau kidogo ili na wengine akili na mishangao itukae sawa,..ahsante sana!!!
 
Back
Top Bottom