Wazee tupatieni dunia yetu, ama tujitwalie kwa nguvu?

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,987
20,271
Naiangalia rika ya ujana wa juzi na ujana wa leo, huu ni ujana mikingamo katika dunia tenge. Agharabu binadamu amepewa na kujaaliwa vichwa viwili vya kufikiria, kichwa cha juu chenye macho ya nyama, mdomo na pua, Pia kichwa cha chini kinachoundwa na via vya uzazi, hiki kinafikiria na kujituma katika ngono na uzazi tu.

Nguvu ya utumizi wa vichwa hivyo huzidiana katika msongo rika wa binadamu, vijana wengi wanatajwa kutilia mkazo utumizi wa vichwa vya chini katika tafakuri zao, na hili limepelekea kuwa na dunia tenge. Wengi wa vijana hawa ni wanaopatikana bara la upwa la karne hii ya 21.

Karne ya 20 ndio karne inayotajwa kuwa na kizazi cha mwisho cha uwepo wa binadamu wenye utumizi mkubwa wa vichwa vya juu. Ni karne hiyo ndio yenye machipuzi madhubuti na thabiti ya kifikra.

Leo taifa limekumbatia mzigo wa vijana wenye utumizi mkubwa wa vichwa vya chini, fikra zao ni mfu na zinazingatia kiwango cha njaa ya tumbo iliyohamia kichwani na ngono zembe, ni kundi la ufuasi zaidi kuliko utendaji zaidi. Katika picha ni vijana majabali ambao pengine ukiwa mgeni unaweza kusema hawa si kizazi hiki cha nyoka, kwakuwa miimo yao, akili zao na vinywa vyao si vya kizazi hiki.

Hawa vijana katika picha wamebalehe na kuvunja nyungo zote, hawa hawalambi viatu, si wafuasi wa ndio. Hawa wanasimama na kusimamisha. Lakini wazee wamebana, hawa vijana wako kati ya umri wa miaka 30 na 40, lakini hawa hawaonji hata ujumbe wa nyumba kumi, achilia mbali uwaziri. Zaidi zaidi vijana hawa wamenasibishwa na wazee kuwa makazi yao yakustahili yatakuwa central ana Kisutu na segerea, wakizingua wabapotezwa kama vile ipoteavyo sindano au pini.

Unaweza kuvuta fikra, Vijana wa kizazi cha karne ya 20 waliwezaje kuwa vijana kwaajili ya taifa lao kuliko hawa wa karne ya ishirini na moja vijana ambao ni mzigo kwa taifa?

Fikiria katika umri lijari wa moto kabisa kwa vijana kama Julius Nyerere miaka 39 tu akawa Rais, Oscar Kambona mika 33 tu akawa Waziri Mambo ya Nje, Amir Jamali miaka 40 tu akawa Waziri wa Fedha, Solomon Eliufoo miaka 40 akawa Waziri wa Elimu, Rashidi Kawawa akiwa na miaka 37 tu akawa Waziri mkuu, Nsilo Swai akiwa na miaka 35 tu akawa Waziri wa Viwanda, Bhoke Munanka akiwa na miaka 34 akawa Waziri Ofisi ya raisi, Usalama wa Taifa,
Job Lusinde akiwa na miaka 31 tu akawa Waziri Wizara Mambo ya Ndani,
George Kahama akiwa na miaka 32 tu akawa Waziri wa Ushirika na maendeleo, huku
Fundikira akiwa na miaka 40 tu akawa Waziri wa Sheria.

Ni kigezo gani kilitumika kuweka umri wa kuwa na sifa ya kugombea urais? Tukubali ilitafutwa hekima ya kiuongozi kwa kizazu kipya na ndipo kuweka sifa ya mgonbea urais iwe kuanzia miaka 40. Hoja inakuja je kwa miaka 40 ya leo vijana wanakuwa wametoka kamasi kweli na kuweza kusimama wao wenyewe?

Mfano serikali kwa namna moja ama nyingine, kwa miaka mingi imekuwa ikiundwa na rika la uzee zaidi, Rais miaka 60 na kuendelea, Makamu miaka 61 na kuendele,
Waziri Mkuu miaka 58 na kuendelea, Haya njoo kwa viongozi wa dini ambao jamii imeaminishwa kuwa wanamiliki hekima ya duniani, wote umezaliwa umewakuta...na bado wapo utazeeka utawacha.

Ukisoma Kitabu chenye mkusanyiko wa machapisho ya simulizi mbalimbali za enzi za Rumi ambacho leo kinaitwa Biblia inayoaminiwa na waamini wa Ukristo, katika moja ya andiko la jamaa anayeitwa Daniel 1:3 nainukuu, "Mfalme akamwambia Ashpenazi, mkuu wa matowashi wake, awalete baadhi ya wana wa Israeli, wa uzao wa kifalme, na wa uzao wa kiungwana"; Mstari wa 4; unasema, "vijana wasio na mawaa, wazuri wa uso, wajuzi wa hekima, werevu kwa sababu ya maarifa yao, wenye kufahamu elimu, watakaoweza kusimama katika jumba la mfalme"; mwisho wa kunukuu.

Ukisoma mbele zaidi, Bwana Daniel anakazia kwakusema awafundishe elimu ya Wakaldayo, na lugha yao. Kwa Tanzania hakuna mpango madhubuti wa kuwarithisha vijana makuzi, elimu na ujuzi wa wazee zaidi ya kutengeneza "wafuasi" wao, walambanyayo, na kuwatumia vijana hao katika kutekeleza maono ya wazee hawa. Kazi ipo, wazee wanauishi muda wa vijana huku vijana wanakufa na maono yao, mtawazika sana.

Enyi wazee hebu acheni kukaza tupatieni dunia yetu!

Endelea kupata kitabu cha Ujasusi kwa OFA ya #CORONA kwa 25,000/= badala ya bei halisi ya 80,000/=,

Lipia 25,000 kwa 0715865544 au 0755865544 (Yericko Nyerere) tuma majina yako na mahali ulipo.

Nje ya Dar nauli ni 8,000/=
IMG_20200527_101311_467.jpg
 
Wewe ndiyo yupi sasa kwenye hiyo picha? Anyway, hongera kwa Bandiko zuri dhidi ya hawa Wazee Ving'ang'anizi wa madaraka kutoka vyama vyote vya siasa.

Inakera kuona hawa viumbe wakirithishana madaraka kutoka Baba/Mama kwenda kwa mtoto, mjukuu, nk huku wenye hivyo vipaji kama mtoa mada, mkiishia tu kulima matikiti huko Kigamboni.
 
Back
Top Bottom