Wazee nchini Afrika Kusini watumia mipira ya kiume maharafu kama condoms kujitibu maradhi ya baridi

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,315
33,111
Wazee nchini Afrika Kusini watumia mipira ya kiume maharafu kama condoms kujitibu maradhi ya baridi yabisi


000_Par7375013_0_0.jpg


Desmond Tutu na Graca Mandela mke wa rais Mandela



Na Ali Bilali
Watu wa makamo nchini Afrika Kusini wamebuni mbinu mpya ya kutumia mafuta ya kwenye mipira ya kiume maarufu kama condoms kwa ajili ya kujitibu maradhi ya baridi yabisi ambayo yamekuwa yakiwasumbua wengi na wamekuwa wakipanga kwenye maungio ya viungo.

Wagonjwa wengi wanaokabiliwa na maradhi ya baridi yabisi wameacha kutumia videngo ambavyo amekuwa wakipewa Hospital na badala yameanza kutumia mafuta hayo kupanga sehemu za maungio ya mwili na wamekuwa wakipata ahueni ya haraka.

Watu wengi wa makamo wamekuwa vinara wa kuchukua condoms ambazo zinasambazwa bure nchini Afrika Kusini kutokana na nchi hiyo kuwa na maambukizi makubwa lakini matumizi yake yamekuwa si ya kuzuia kusambaa kwa ugonjwa huo tena.


Utafiti uliofanyika huko Soweto umethibitsha watu wengi wa makamo wanatumia zaidi mafuta hayo katika kupambana na maumivu yanayochangiwa na baridi yabisi ambayo imekuwa ikiwasumbua mno watu wenye umri mkubwa.


Wazee wengi wamesema kutokana na kupatikana kwa urahisi kwa condoms kwao imekuwa ni kitu cha faraja kwa sababu wameweza kupata tiba mbadala ya kupata sehemu za maungio badala ya kuendelea kunywa dawa kila siku.



TAGS: AFRIKA KUSINI


 
Back
Top Bottom