Wazee Arusha wampinga mbunge Mrisho Gambo

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Wazee wa Jimbo la Arusha Mjini Wamedai kuwa kauli ya Mbunge wao Mrisho Gambo kuwa Wamachinga Wanyanyaswa na Mgambo wa Jiji ina lengo la kuchonganisha Wafanyabiashara hao na Serikali kwani zoezi la kuhamisha wamachinga lilishirikisha pande zote wakiwemo viongozi wao.


Gambo alidai mbele ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa ,Abdullahaman Kinana kuwa Mgambo wa Jiji wanawanyanyasa Machinga kwa kuwakamatia Biashara zao kwa kudai ya kufanyabiashara kinyume na utaratibu.


Kauli hiyo ilipingwa vikali na Wazee hao wakiongozwa na Shekh Saidi Rashid kwa kueleza kuwa Mbunge huyo afuate taratibu katika kuwasilisha hoja zake na sio kukimbilia kwa viongozi wa ngazi za juu wa Chama.


Mzee Rashid alisema Mbunge Gambo kila wakati amekuwa akikinzana na maamuzi wa watendaji wa Jiji wakiongozwa na Mkurugenzi DktJohn Pima na kueleza kuwa malalamiko ya Mbunge huyo ni ya uchonganishi na yenye hila kwa viongozi wa Jiji dhidi ya Wananchi hatua ambayo ni mbaya kama kiongozi.


Dkt Pima amekuwa akifanya mambo mengi ya Mandeleo katika Jiji la Arusha ikiwemo kuongeza Pato la Ukusanyaji wa Mapato tofauti na Awali lakini hilo halipongezwi na Gambo na amekuwa mtu wa kumchonganisha Mkurugenzi huyo na viongozi wa Juu wa Nchi hatua ambayo sio sahihi.


"Tunamwambia Gambo acha mara moja fitina,Majungu na Uchonganishi kwani Arusha ni salama na mambo yote yako sawa ikiwa ni pamoja na machinga kuwa na vibanda vya kufanyia biashara na vingine viko wazi baada ya kutosheka'' Alisema Shekh Rashid

Wazee hao wametishia kumnyima kura iwapo ataendelea na tabia yake ya kujali maslahi yake na kushindwa kushirikiana na viongozi wenzake .
 
Hawa si ndio wale wabunge walio saidiwa kuiba kura na JPM??
Mungu atusaidie, wote walohusika kt ule wizi awape mapigo yao hapahapa duniani tukiona.
Mastermind wa wizi i.e mkuu wa wizi huo bw JPM kwa sasa kadudu kake kawe kameungua km mshiKaki uku akigumia kwa maumivu makali
Hivi Arusha mjini kuna mbunge au kuna mwimba taarabu?
 
Huko kanda ya kaskazini inaelekea kuna fukuto la kisiasa, mara wazee wa Arusha watamnyima kura Mrisho Gambo huku kule Kilimanjaro madiwani 41 hawamtaki mkurugenzi ....




21 April 2022

Madiwani 41 mkoani Kilimanjaro waandika barua ya kumkataa mkurugenzi




Madiwani 41wa Halmashauri ya Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro, wameandika barua ya kumkataa mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Kastory Msigala wakimtuhumu kutumia maamizi binafsi kupitisha baadhi ya miradi ya maendeleo katika Halmashauri hiyo. Madiwani hao ambao waliandamana hadi ofisi ya Mkuu wa Mkoa kuwasilisha barua yao, wanalalamikia ukusanyaji wa mapato hafifu kutokana na utendaji usio shirikishi wa Mkurugenzi huyo pamoja, utolewaji wa maamuzi ya utekelezaji wa miradi bila kushirikisha kamati ya fedha na baraza la madiwani.
 
Back
Top Bottom