Wazazi wote haya sio malezi mazuri kwa watoto.

Ngareroo

JF-Expert Member
Aug 11, 2019
2,049
2,249
Habarini za wakati huu wadau..Hopefully ni nzuri kabisa..

Bas leo nna jambo muhimu la kuwaasa wale wote wenye watoto,mimi bado mdogo ila na sina familia ila kwa hiki nilichokishuhudia ata nikiwa na familia yangu siwezi ishi hivi...Hivyo bas sitatumia Lugha ya NGAREROO SLANGS ili wote tuelewane au vipi bhana eeh.?!



Kweli mtoto umleavyo ndivyo akuavyo!!
Leo baada ya kutoka pindi nilimtembelea chaliangu ambae tumesoma wote O level..Anakaa mitaa ya Mianzini apa Arusha,Maisha yake si haba huwezi mfananisha nasisi wa Ngarenaro kwa wang'ata lami uku..



Chalii hakuendelea na A level alipiga mishe zake tu na anabiashara zake,anaishi na mkewe na wana katoto kadogo ka miaka mi5 au 6ivi..

Katoto kanaitwa ka Junior sijui junya ivo ivo yaani..kanasoma izi shule za Nursery sijui English Medium izi..In short mwana anaishi maisha ya kwenye TV na familia yake..


Yaani tangie nimeingia mule ndani haka katoto. hakajui kusema Mama wala Baba,kanasema Dadi na Mami tu!Bas jamaa anajiona mjanjaaaa!!


Bas haka katoto hakakaripiwi wala kukatazwa chochote..


Nilipofika tu nilishitushwa na mwenendo wa hako kabwana mdogo,dada wakazi ambae nilimletaga mimi mwaka juzi akaanza kunishangaa na kusema haya kanayofanya ni cha mtoto sana..



Kuna siku kalimvua Baba ake taulo alipokua anatoka bafuni tena mbele za watu,jamaa akaishia tu kusema"Noo junya this is bad"alaf eti anasema"tatizo uyu mtoto ana akili za kikubwa"Doooh hii story kutoka kwa House girl iliniacha mdomo wazi..Ghafla katoto kakaja na mpira sebuleni kisha kakaupiga mbele yetu,Kanaangusha vitu mala kanatupiga usoni..Jamaa anaishia tu kusema"Hahah please dont do that junyaa"lakini hata hakasikii ndo kwanza kanapanda juu ya meza mala kabatini yaani kero tupu..


Chalii na mkewe utafikiri wamelongwa,mala kakanipaparukia kakataka kunivuta miwani yangu na ndevu zangu za mzuzu,Kwa ustaarabu wa nyumba ile nikatoa kauli ya kinafiki"No Junya No,this is bad"muda huo kwenye TV kulikua na Wasafi Festival ya Dar marudio ana'perform TID na Domo kaya,eti kikang'ang'ania kiweke Katuni,jamaa akakiwekea bas bora ata kingeangalia,muda wote kinataka kupakatana tu hadi kikachafua T-Shirt yangu nyeupe iliyoandikwa 'Arusha Boy'..



Baada ya dakika kadhaa hivi kupita mama Junya akaingia jikoni,Baba ake nae akaenda chumbani kidogo..


Sebuleni tukabaki mimi na hiki kidude kisichokua na chembe ya aibu..Si kikaanza vimaswali vya maudhi...!Eti"Leo umekuja kula kwetu","Mna TV kama hii yetu?",,Baba ako anakuleteaga chokoleti kama mimi?"..Si kikaanza mchezo wa kunitemea mate alaf kinacheka..


Mwanzo nilijua labda kitaacha,kadri nnavojifuta yale mate ndivyo kinaona kama ni mchezo flani wa kuburudisha..Mama ake jikoni akaskika"Junya plizi donti du that tu yuwa anko!".."Junya yua veri badi"chenyewe kinajibu"Noo mamii"..Kilipojichanganya ni pale kiliponipanda kichwani na kunivuta nywele zangu Afro ndefu kama za Shimateo wa Ayo&Teo au za DJ Tee wa shujaaz alaf nyeusi..Nikaona hii sasa ni dharau nikakishika mkono wake kwa nguvu nikakitolea macho nikakifinya vizuri mashavu yake..



Hakikuamini kilichokiona,nadhani kiliifananisha mikono yangu na ile ya King kong..kilijaribu kujitoa lakini wapi?nilikikaza sawa sawa..kikaniangalia usoni uku kikiwa hakiamini kama kimefinywa na binadamu alie hai.nikakiambia kwa sauti ya chini chini yenye kitisho uku nimekaza macho yangu mekundu"Ukinisogelea tena nakukata masikio"nikakiachia kiondoke..



Ebwana wee kilitoka marathon pale sebuleni uku mkojo unakitiririka,kilienda jikoni kwa mama ake,nilitegemea kitalia kwa nguvu but kikawa kimyaa,mama ake akakiuliza"Umefanyaje Baba?What happened junya?"kikawa kimya..




Mama ake akaja nacho sebuleni uku chenyewe kikiwa nyuma kimejificha kwenye gauni la mama ake..Mama ake akauliza"Shemu uyu kafanyaje?".nikajibu kwa sauti ya mtu asiye na dhambi kabisa"Shemeji ata sijui katimka tu hapa mbio kaja uko",,Baada ya hapo kukawa na Displini mle ndani,tukala bila fujo na kuzungumza vizuri tu bila fujo..



Baba ake akakauliza"A yu siki?"kalinicheki mimi. bila kujibu kitu,nadhani ile kauli ya kukatwa masikio ilimkaa..mpaka naondoka nyumba ilijaa ustaarabu..
Wengine maisha ya Kwenye Tv hatufungamani nayo kabisa.



@NgarenaroBoy.
 
Mi sipendi watoto watundu.
Mi nakupiga mbele ya mzazi wako
 

Attachments

  • zngua.JPG
    zngua.JPG
    13.3 KB · Views: 2
Back
Top Bottom