Mgodo visa
JF-Expert Member
- Nov 1, 2016
- 3,562
- 3,558
Kama uzi unavyo jieleza hapo juu.
Ni masikitiko yangu (huu sasa ni mwaka wa pili) pamoja wa wazazi wengine.
Kumekuwa/Umeibuka mtindo ama utaratibu kutoka Wizara inayohusika na mambo ya Taaluma, kuwaelekeza Maafisa Elimu (W) kuhakikisha karibu 100% ya Wanafunzi wote kutoka Shule za watu binafsi ama taasisi za Kidini, walio hitimu na kufaulu mitihani yao Elimu ya Msingi, wanapelekwa (wanachaguliwa) katika Shule za Kata (Saint Kayumba)
Naandika haya, nikiwa kama mzazi na Muhanga wa maamuzi haya.
Fikiria pale Mzazi/Mlezi unapojinyima na kujipinda (kwa kulipa Mamilioni) kuhakisha mtoto (mwanafunzi) wako anapata Elimu bora na katika Shule yenye Mazingira bora, anafaulu mitihani yake kwa Alama nzuri tu (A ama B) kisha anachaguliwa kwenda katika Sekondari za Kata, kwa kweli inauma sana...!
Wanasema huu ni mpango wa makusudi kuwafanya watoto wetu (wa-kishua) waishi kama "Mashetani".
Wanasema kama Mzazi/Mlezi wake aliweza kulipa Mamilioni Miaka saba ya Msingi, atashindwa vipi kulipa Mamilioni kwa miaka minne inayofuata...!
Kumbuka Mzazi, mtoto wako anahitimu kutoka katika Shule aliyofunzwa maadili Mema (Mazuri) sasa unalazimishwa umpeleke "CHANGANYIKENI" katika Shule ambazo 90% ya wanafunzi wake wana ndoto ya kuwa kama Diamond, Manfongo, Giggy au Shilole, naomba niseme "this is unfair"..
Inapo tokea Wazazi/Walezi kuhoji utaratibu huu kwa Wakuu wa Shule, wanatupa majibu kuwa, ni lengo na matarajio ya Serikali kuwa, kujaza wanafunzi walio faulu kutoka Mashule binafsi, kutaleta mabadiriko kitaaluma, hivyo kuleta tafsiri (tumaini) kwa wananchi kuwa, sasa Shule za kata nazo ziko vizuri kushindana na Mashule binafsi kitaaluma...!
NB: Wizara inasahau kuwa huko hakuna Waalimu bora, vitendea kazi vya kutosha pia Maabara za kufundishia kwa vitendo.
Matokeo tunakwenda kuua ndoto na matarajio ya watoto wetu.
Wilaya ya TEMEKE ni Wahanga wakubwa katika hili.