Wazazi wenzangu, yule mama jeuri wa Masasi girls amehamishwa.

Ramea

JF-Expert Member
Mar 19, 2015
2,019
2,000
Kwa yeyote mwenye mtoto shule ya wasichana Masasi bila shaka atakuwa anakumbuka vitimbwi vya huyu headmistress jeuri, kiburi, asiye na heshima na kauli chafu kama amemeza choo.

Mama huyu akitoa suspension hata kwa kosa la kumfinya shavu mwanafunzi, aliwahi kuwafukuza watoto zaidi ya 20 wakarudishwa kwa Amri ya R.E.O mkoa wa Mtwara...kwa kikao rasmi cha wazazi, walimu, afsa elim mkoa na wanafunzi.

Headmistress huyu yasemekana hutukana walimu wake hadharani. Hakika hii ni habari njema kwa wanajumuia ya Masasi girls high school, wazazi na wanafunzi bila shaka hata walimu walichoshwa na customer care ya mama huyu.

Asante Magufuli na watendaji wa Elimu mkoa wa Mtwara kwa kuliona hili...kwani shule ile ni kongwe na huchukua vijana toka mikoa yote Tanzania bara. Ni shule ya kihistoria pia kwani hata speaker mstaafu Mama Anne Makinda alipata elimu yake pale.
 
NONIYANG'WAKA

JF-Expert Member
Sep 22, 2013
1,512
2,000
kama wewe ni mzazi na imefurahia huyo mama kuhamishwa kwa sababu anazisimamia sheria haufai.

watoto wenu wanaondoka nyumbani mapema na wanakaa gheto kwa wiki wakigegedwa.

huyo mama huenda ni mkali kwa walimu kwa sababu wakiume wanawatongoza wanafunzi, wakike wanategea kazi na walimu wengi kwa sababu ya mgogoro wa kinafsi na serikali yao wanafanya kazi kwa kinyongo.

nakutakia maisha mema h/m huko ulikohamia.

piga kazi mama
 
Ramea

JF-Expert Member
Mar 19, 2015
2,019
2,000
KWA HIYO HUKO ALIKOHAMIA HAMNA WATU AMA ????
Yasemekana anaenda shule ya kata, ni kama demotion tu. Alituchosha sana wazazi...kututoa mwanza, kigoma kwenda Mtwara kusikiliza uharo wake. Nadhani wanamshusha taratibu mwisho wa siku hata hiyo shule ya kata ikimshinda ataingia darasani
 
Distinction

JF-Expert Member
Sep 20, 2014
659
500
mnasaidiwa kulelewa watoto wenu, afu leo mnamuona huyo mama afai, iv mngekuwa mnajua watoto wenu wanayoyafanya mashuleni laiti usingeshangalia ivo. mi binafsi nawapenda walimu tena wamama wanao kua wakali.

sababu najua faida zake....
 
NONIYANG'WAKA

JF-Expert Member
Sep 22, 2013
1,512
2,000
Yasemekana anaenda shule ya kata, ni kama demotion tu. Alituchosha sana wazazi...kututoa mwanza, kigoma kwenda Mtwara kusikiliza uharo wake. Nadhani wanamshusha taratibu mwisho wa siku hata hiyo shule ya kata ikimshinda ataingia darasani
pole kwa kutotambua umuhimu wa kusimamia sheria
 
Aggayah

Senior Member
Oct 16, 2013
141
225
Yasemekana anaenda shule ya kata, ni kama demotion tu. Alituchosha sana wazazi...kututoa mwanza, kigoma kwenda Mtwara kusikiliza uharo wake. Nadhani wanamshusha taratibu mwisho wa siku hata hiyo shule ya kata ikimshinda ataingia darasani
Hujitambui!
 
Betterhalf

JF-Expert Member
Dec 20, 2016
2,832
2,000
Chuki hujenga sumu mbaya sana.
Sina hakika kama tumethubutu kuangalia pande zote NNE ili kuona tunawezaje kumhukumu(achilia mbali incident ilofikisha maamuzi haya); kwa maana ya Mkuu wa shule,walimu,wazazi na wanafunzi.
Tuunge mkono mazuri yanayofanywa na wakuu/walimu na tushauri au tukemee kwa staha pale wanapoteleza.
Kazi wanayoifanya ni kubwa na siyo ya kuibeza kwa lugha rahisi,Kali,zenye kubeza na zilizojaa dharau.
Pia, tujiridhishe na taarifa tunazozitoa ili tuone tumepatia ama nasi tumekosea.
 
Lwasu

JF-Expert Member
May 31, 2015
771
1,000
Anaitwa mama Tesha kabla ya kupewa ile shule kwanza ilikua inaongoza kwa nidham mbovu aliinyosha ile shule, kipindi kile alitufundisha biology Ndanda boy wazee wa Ndabo 2009 tunamjua vizuri huyu mama na utukutu wote wa boys lakini kwa huyu mama ilikua ni break !!!!
 
Mama Tesha alishaondoka Yupo kilakala high school. Huyo mama alikuja baada ya mama Tesha. Anaitwa Mama Sarah, korofi sana huyo mama.
 
kibaravumba

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
6,192
2,000
Watu wengine huwa wanafanya ukorofi kwa nia njema ila wakati mwingine ukorofi huu huweza kuonea wengine.Niliwahi kuombwa kumuwakilisha mzazi katika shule moja Mwanza kwani kulikuwa na mtoto wa kike alifukuzwa shule kisa alitongozwa na makamu mkuu wa shule akakataa.Makamu huyo akamsingizia kuwa amekwepa kumwagia bustani.Binti alibakiza wiki mbili afanye mtihani wa kidato cha nne.
Kesi ilipoenda kwa Head mistress alikataa kata kata kunisikiliza na hata kumsikiliza yule binti.Alitaka aje mzazi wake halisi ambaye hakuwepo karibu kipindi hicho.Nilimshauri tu amuombe arudi kutoka safari.Baadae kesi iliisha lakini yule binti alijisalimisha kwa makamu mkuu wa shule akafanya alichotaka.Kama headmistress angekuwa na hekma na subira,huenda isingefika huko
 
ukaya kutali

Member
Feb 18, 2017
9
45
Mama Tesha huyo, ila alitusaidia sana kwa kweli ,aliinyoosha shule,yani ilikua kama shule ya private,walimu wanafundisha vzur ,chakula safi,mazingira safi ,na unaripoti shule tarehe ya kufungua shule,ukichelewa utarudishwa uje na mzazi wako,alikua hapendi ujinga huyu mama, alikua anaogopeka hatari ,kuanzia,wanafunzi ,walimu mpaka wafanyakaz wasio walimu ,
 
Aug 22, 2015
35
95
mnasaidiwa kulelewa watoto wenu, afu leo mnamuona huyo mama afai, iv mngekuwa mnajua watoto wenu wanayoyafanya mashuleni laiti usingeshangalia ivo. mi binafsi nawapenda walimu tena wamama wanao kua wakali.

sababu najua faida zake....
N watu wachache sana wenye muono kama wewe.N dhahiri wazaz wengi huwavunja moyo Walimu ambao ndio waandalizi wa maisha bora kwa watoto zao,tazama huyu mzaz masikini wa fikra anavyoshangilia kuhamishwa wa mwalimu huyu Shame on you.
 
Aug 22, 2015
35
95
Watu wengine huwa wanafanya ukorofi kwa nia njema ila wakati mwingine ukorofi huu huweza kuonea wengine.Niliwahi kuombwa kumuwakilisha mzazi katika shule moja Mwanza kwani kulikuwa na mtoto wa kike alifukuzwa shule kisa alitongozwa na makamu mkuu wa shule akakataa.Makamu huyo akamsingizia kuwa amekwepa kumwagia bustani.Binti alibakiza wiki mbili afanye mtihani wa kidato cha nne.
Kesi ilipoenda kwa Head mistress alikataa kata kata kunisikiliza na hata kumsikiliza yule binti.Alitaka aje mzazi wake halisi ambaye hakuwepo karibu kipindi hicho.Nilimshauri tu amuombe arudi kutoka safari.Baadae kesi iliisha lakini yule binti alijisalimisha kwa makamu mkuu wa shule akafanya alichotaka.Kama headmistress angekuwa na hekma na subira,huenda isingefika huko
Nahisi % kubwa ya wanao n masikini wa fikra darasani kama ulivyo wewe, hao ndio huwapa walimu shida sana na kuwafanya wasikubalike kwa matendo yao ktk jamii yenye fikra kiza kama zako.Watanzani hatupendi kuwajali na kuwaunga mkono Walimu wetu,kumbuka walimu ndio Daraja au pitio la mafanikio kwa watoto wetu.Hauna hata aibu Kumshangilia kwa mabaya Kiongoz wa Elimu!? Kisa kumtetea mwanao ambaye yawezekaya alikua na fikra za uzinifu.[HASHTAG]#Amka[/HASHTAG]
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom