Wazazi Wenzangu: Kuna umuhimu (faida) gani kwa baadhi ya watoto kuwa na majina mawili? Jina la shuleni pamoja na lile la nyumbani?

Hii ni mara ya kwanza kusikia mtu ana majina mawili ya kizungu na yanatumika moja nyumbani na lingine kijamii (shuleni).
Nimezoea kusikia majina ya kikabila ya asili yakitumika nyumbani zaidi, na ya kizungu yakitumika shuleni.
Sijui nia hapo ni nini kwa mfano uliotoa, ila kwa mfano wa pili ndio imezoeleka hivyo.
 
Mimi pia nina mawili la kiarabu na kinyumbani...matokeo la kinyumbani ndo limeshika kila mtu hadi kwenye mambo ya kazini ni hilo...wazee walikuwa wanaoneshana umwamba mana ndo "festi boni"
wazee walikuwa wanaoneshana umwamba
 
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa jamiiforums. Mimi mdogo wenu (Last Born) Infantry Soldier nipo mzima kabisa wa afya. Thanks to God the Almighty.

Sio kila muda tunapaswa kusoma na kujadili makala zinazohusiana na masuala ya cold war, jeshi na ujasusi wa KGB, CIA na Mossad. Ngoja leo tujadili kidogo changamoto za maisha katika jamii tunamoishi.

Eti ndugu zangu wamama na wababa wa Tanzania;

Kuna umuhimu (faida) gani kwa baadhi ya watoto kuwa na majina mawili? Jina la shuleni pamoja na lile la nyumbani?

Nimeamua kuuliza hivi kwa maana jana nikiwa ninatoka katika shughuli zangu niliamua kupita katika shule moja ya msingi ya boarding kumsalimia mtoto wa kaka yangu mkubwa. Huyu dogo jina lake ambalo linalijua siku zote tangia akiwa mdogo ni Immanuel na nilipofika kwa academic master nikamuulizia kwa jina hilo hilo sema nikaongeza na jina la kaka yangu (********) ila wao wakasema hawamtambui mtoto huyo. Sasa kwa kujiongeza tu ikanibidi nimpigie tena simu baba yake mzazi ili kuweza kujua huyu ndugu yangu anajulikana kwa jina lipi hapa shuleni ili niweze kumsabahi kisha niendelee na mishe zangu. Ndio hapa baba yake akasema hilo IMMANUEL ni jina lake la nyumbani lakini shuleni anajulikana kwa jina la Alexander (*******). Hapo kwenye mabano ndio jina la baba yake.

Sasa tangia hapa nikawa ninajiuliza, kuna umuhimu/faida gani kwa mzazi kumpa mtoto jina la nyumbani pamoja na shuleni?

Je, na wewe mwana JF ulikuwa na jina la nyumbani pamoja na shuleni pindi unasoma? (Sio lazima ulitaje jina lako ila unaweza ukasema tu NDIO au HAPANA)

OUR MOTTO: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
Mbona nikawaida tuu, la nyumbani ninaitwa Rwechungura, na shule naitwa John. Tembea uone
 
Hii system ipo sana Uhayani kama alivyocomment chief hapo juu. Unakuwa na jina la nyumbani la Kihaya halafu baadae ukibatizwa unakuwa na jina la kizungu. At last, la kubatizwa ndo linakuwa first name, la kilugha la kati halafu la baba linakuwa la mwisho. Mfano Gabriel Rugarabamu Pastory au Christina Kengonzi Salvatory. In this case, Kengonzi na Rugarabamu ni majina ya nyumbani, Gabriel na Christina ya kubatizwa. Na ni kwa sababu hii, wahaya wengi hawana majina ya ukoo maana la tatu linakuwa la baba.
 
Mimi nina majina mawili yanayofahamika sehemu tofauti. Jina la kwanza linafahamika nyumbani nilikozaliwa na hata mama yangu anajulikana kwa jina hilo (mama .......) . Hili la pili linajulikana na wanafamilia, nje ya nyumbani na ndio hilo lipo hata kwenye documents. Siku moja kuna rafiki yangu mmoja alitoka mjini kwenda kuzika mfanyakazi mwenzake karibu na kijijini kwetu. Akanipigia nimuelekeze namna ya kufika hadi nyumbani, maana uelekeo wa kijiji chetu anaujua alishawahi kufika siku za nyuma....mimi sikumuelekeza nilijua anatania maana kutoka pale alipokuwa hadi kwetu ni parefu kidogo. Ye kaona namzingua huyooo kafika mpaka kijijini akijua atauliza tu kwa kina XY. Kiukweli alifika hadi nyumbani ya pili kutoka kwetu ila hakufanikiwa kufika kwetu maana jina alilouliza kule halifamiki kabisa
 
Back
Top Bottom