Wazazi wengine wanashangaza | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wazazi wengine wanashangaza

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Tall, Mar 11, 2010.

 1. T

  Tall JF-Expert Member

  #1
  Mar 11, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 1,431
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  Kuna dada mmoja aliachana na mumewe, sababu alizozitoa ni kuwa mumewe alipata mwanamke mwingine hivyo yeye huyo dada akaamua kumsusa.Hadi ananieleza,alikuwa hamtaki kabisa mumewe hata kumsikia.
  Baada ya kumsikiliza kwa kina nikambadili mawazo. Nilimshauri, afanye fasta fasta warudiane na mumewe. Lakini awe makini kabla ya XXXXX ahakikishe wote wamepima,vipimo vya ukimwi ni muhimu.Leo kaja kanikuta na donyoa donyoa kwenye keybord nikijibu ile thread ya pearl. Chapchap nikamuuliza mambo safii??? Akanijibu kwa huzuni kuwa mambo safi,akaendelea kueleza, ''mume wangu kaniomba msamaha,kaachana na mwanamke wake,tumepima tuko fit, ila ila ila'',duuuuu, akaanza kulia. Nilishangaa sana na kujiuliza kulikoni? baadae alipotulia,akanieleza kuwa wazazi wake WAMEKATAA WASIRUDIANE, nikamuliza kisa?
  akajibu ''wanasema hawamtaki tu''.
  hapo ndipo kaniacha hoi;
  -wazazi wengine jamani vipi?
  -au wanataka wale mahari mara ya pili? maana mtoto mwenyewe analipa kwelikwelli toto languvu?eeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeh naomba
  mumgu anisamehe tunambiwa tusitamani wake za majirani zetu.
  - au hasira za aibu?
  - Kama watu walishasameheana nyie wazazi donge la nini?
  - Si walishawaruhusu wakaoana mwanzoni?
  - Kwa nini hawatoi sababu?
  Kwa kawaida nakuwa na majibu pale pale kila ninapoulizwa jambo, lakini leo nilikwama nikamwomba tuonane kesho.Siku ya leo we acha tu.
  - sijui kesho nimwambie awapuuze tu wazazi? Mungu nae anasema waheshimu baba yako na mama yako.
  - Sijui nimwambie atafute mume mwingine ili aepuke laana ya wazazi?kwa kuishi na mume waliomkataa?
  - Sijui nimwambie wafanye fastafasta wabandikane mimba ili aruhusiwe kurudi kwa mumewe? Ebu semeni waheshimiwa wana JF. JE? arudi au asirudi kwa mumewe?
   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  Mar 11, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  kama analipa kihivyo basi
  nitumie namba zake pm.
  nimsaidie......
   
 3. Mentor

  Mentor JF-Expert Member

  #3
  Mar 11, 2010
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 18,729
  Likes Received: 8,306
  Trophy Points: 280
  Tall for the first time umeandika ujumbe wa maana! Pokea senksi kwanza..
  Ushauri:
  Wazazi wanafanya hivyo kumprotect mwanao..its a natural tendency. usiwalaumu..
  Cha kufaya huyu dada naye achukue muda kwanza kutafakari (huku akiomba, maana haya mambo yanahitaji divine intervention!)ili apate kufahamu kwanini huyu ndugu aachane na aliyekuwa naye-1. kwa sababu amejitambua au 2. labda huyo msichana ndo alimuacha 3. sababu nyingine tusizozifahamu.
  Baada ya hapo anaweza kuongea na wazazi wake kuwaeleza kuwa kweli jamaa kabadilka..Maana sasa hivi kaja kukuomba msamaha unakubali huna uhakika kabadilika kweli ama ameona afadhali zimwi likujualo!??
  Ni hayo tu mkuu..
  Barakaz!
   
 4. ChaMtuMavi

  ChaMtuMavi JF-Expert Member

  #4
  Mar 11, 2010
  Joined: Oct 15, 2008
  Messages: 333
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mbuzi kaenda kuomba ushauri kwa chui, duuh
   
 5. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #5
  Mar 11, 2010
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135
  ..........Huyo mdada naye kweli hamnazo, mwanaume huyo alishawahi kumcheat wa nini tena? Wazazi hapo wapo right kumkatalia kurudi kwa mumewe kwa sababu wameshamuona mwanaume hajui kufunga zipu yake, anapenda kufungua zipu kwa kila mwanamke.

  Hivyo kama akiamua kurudi awe tayari kutengana na mwanaume tena, maana inaonyesha mwanaume utulivu zero.
   
 6. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #6
  Mar 11, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,197
  Trophy Points: 280
  Ahhahahahahahaha,

  You made me say "Oh my god, these people are shameless" even though I don't believe in god.

  Ur funny dude.

  Mtu yeyote aliyezidi miaka 18 anayewaachia wazazi wake wampangie maisha yake deserves whatever comes to him/ her indeed.

  I mean in this age watu badala ya kuwatunza na kuwaelimisha wazazi maswala ya dunia ya leo yanavyokwenda, kuna watu bado wanawaachia wazazi wao wawapangie maisha?

  Solution ya matatizo haya ni kutokuoa/ kutokuolewa, kwa sababu ndoa inevitably zinaenda kuwa intrinsically zina matatizo haya.Penda usipende.Nine ten out of ten kuna mtu ata cheat or some shyt like that, sasa kwa nini ujidanganye at all?
   
 7. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #7
  Mar 11, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,197
  Trophy Points: 280
  Wanaume 9 kati ya 10 ndiyo zao, wewe unayemkandia huyu mdada kama unaye wako, at the risk of betraying the gender, kama hujamshtukia basi atakuwa Askofu Desmond Tutu or some Gandhi like that, au wewe mwenyewe utakuwa slow.

  Wanaume 9 katika 10 wamecheza rough somewhere in their relationships, it is not like they want to hurt anybody, sometimes mbongo huwa hazifanyi kazi, badala ya kufikiri na ubongo tunafikiri na uboooo-ngo.

  Our institutions and moralities are far evolved compared to our biologies.Uliangalia interview ya MoNique katika awards za juzi alivyokuwa anaongelea kumsamehe mwanamme na Barbara Walters? Almost like anaongelea open marriage.

  And that's just the men, kinamama walioolewa wanavyojirahisisha mtu wako akipiga suti za Calvin Klein na viatu vya Joseph Abboud tu, never mind anything else, utashangaa mwenyewe.Sasa najiuliza, hawa wake za watu wanatoa namba zao fasta dfasta hivi, ukibeep tu kazi kwisha, na mimi nataka kuopa kweli? Ila mie sio zangu bahati yao.

  Mimi ndiyo maana kuoa ngumu, najua nikioa siwezi kujizuia na mwanamama mmoja sasa kwa nini nimpe mtu uchungu?
   
 8. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #8
  Mar 12, 2010
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,122
  Likes Received: 617
  Trophy Points: 280
  Mbona mimi naona wewe ndo unampa huyo dada ushauri mbovu? Bora waachane now wakati hakuna watoto. Au kuna kitu namiss?
   
 9. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #9
  Mar 12, 2010
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,773
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Mchango mzuri kama avatar yako:cool:
   
 10. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #10
  Mar 12, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,856
  Likes Received: 2,017
  Trophy Points: 280
  Blue=huyu ndie Kiranga namfahamu au?
  Red=hata kama lakini kwa hapo kwenye blue tu umepiga hatua ndugu yangu. BWANA apewe sifa. Amen
   
 11. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #11
  Mar 12, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,856
  Likes Received: 2,017
  Trophy Points: 280
  Kuhusu mada mimi naona wazazi wameplay role yao ya kumlinda binti yao kama binti anaona kuna ushawishi unaoweza kubadilisha mawazo ya wazazi wake basi atafute njia sahihi za kuwaeleza lakini.............................................!!!!????
   
 12. T

  Tall JF-Expert Member

  #12
  Mar 12, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 1,431
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  Ngoja nitakupa akija, nafikiri yupo tigo, jana alisema kuwa wanapendana sana na mumewe kiasi kuwa kila mmoja wao ame divert mawasiliano yote ya simu kwa mwenzie
   
 13. T

  Tall JF-Expert Member

  #13
  Mar 12, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 1,431
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  Kama ulikuwepo, baada ya kutengana tu mkewe kapata bonge ya kazi,ni afisa kwenye kampuni moja ya kimataifa, labda ndio maana jamaa kakubali kutubu.
   
 14. JS

  JS JF-Expert Member

  #14
  Mar 12, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 2,065
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  ;)

  Kumbe wewe mwanaume??? Lovely stuff.......[​IMG][​IMG];)

  Kuhusu sredi: Cheating is everywhere hiyo si kitu mpya kwa wanandoa. Alichemsha pale alivyoachana naye at first. Mwambie she has to learn living with vitu kama hivyo in relationships hata kama ni kwenye ndoa.

  Saa zingine wazazi wants best for their kids so is huyo mdada na wazazi wake. Wanamuogopea mwanao asije pata matatizo lakini zaidi. But wazazi should have limits especially kwenye ndoa na mahusiano. Tunaongelea furaha ya mtu hapa maishani. kama mtu mzima she should judge on her own kwa sababu ni maisha yake na ndoa ni yake.
   
 15. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #15
  Mar 12, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 543
  Trophy Points: 280
  wazazi wa Binti wanakataa kwa sababu ambazo binti yao atakuwa aliwaeleza mwanzo na kama wazazi wenye mapenzi na mtoto wao wanamuhurumia ..
  kama binti yao asingeongea mabaya yote na tabia chafu za mmewe wao wangejua wapi?
  Sidhani kama kuna haja ya kuwalaumu zaidi ni kukaa chini na kutafuta muafaka na wazazi.
  Sina uhakika kama jamaa kaacha kweli mambo yake ya kuchovyachovya..
   
 16. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #16
  Mar 12, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
   
 17. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #17
  Mar 12, 2010
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Nooooo! Wazazi wanayo haki juu ya binti yao, lakini mapatano ya wanandoa yana haki ya kimsingi. Wazazi kwa kawaida ya kimila za wabantu wengi, kuna washenga wanaolink pande mbili. Waliogombana waende kwa washenga wao ambao ndio watakaozungumza na wazazi ili kutulisha boll chini. Lazima wazazi washituke. Hawakusema sababu zao kwa binti yao kuepusha mabishano, hakuna mzazi anayetaka binti yake akae na huzuni. Furaha ya mwano ndio amani yako mzazi.

  Wasiwe na pupa vijana hao. Wasipatane wenyewe na kuishia hapo kwa sababu mambo yenyewe yalishafika nje mbali kabisa. Kwa hiyo wanapaswa kuwashirikisha watu wa mbali ili angalau kujihakikishia ufinyu wa varangati hilo kurudia tena karibuni. Inasaidia mume akikiri kwa wazee kwamba alipitiwa tu lakini hatarudia tena kosa hilo, mkewe naye amani na furaha angalau vitapanda. Vinginevyo akirudi kinyemela anawapa nafasi mume na kimada waendelee kutesa naye akifagia sebule tu.
   
 18. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #18
  Mar 12, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Mkuu ni ajabu, kweli Life is a box of emoticons
   
 19. o

  omwana Member

  #19
  Mar 12, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 46
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Wanapendana nini wakati mume alisham-cheat. Na kama wanapendana mbona mume ameweza kuwasiliana na huyu mwanamke mwingine mpaka kufikia hatua ya kutengana au upendo umekuja ghafla baada ya kuludiana na mbona bado hawajaludiana kwa sababu wazazi wa mke hawamtaki mume. Au una-mbania tu huyu aliyekuomba namba
   
 20. T

  Tall JF-Expert Member

  #20
  Mar 12, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 1,431
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  Wana mtoto mmoja.
   
Loading...