Wazazi wapigwa marufuku tabia ya kuwakatisha wanafunzi masomo kwa ajili ya kuwapeleka mijini kufanya kazi za ndani

AUGUSTINO CHIWINGA

JF-Expert Member
Apr 23, 2017
220
689
Afisa Mtendaji wa Kata ya Rutamba Ndg.Augustino Chiwinga amepiga marufuku tabia ya baadhi ya wazazi kuwaachisha masomo wanafunzi hususani wa kike na kuwapeleka mijini hususani Jijini Dar Es Salaam kwa ajili ya kufanya kazi za ndani.

Ameyasema hayo wakati wa kikao kilichowashirikisha wazazi,walimu na wanafunzi wanaosoma katika Shule ya Msingi Rutamba .

Ndg.Chiwinga alisema hatokubali tabia hiyo iendelee katika kata yake kwani ni kinyume na sheria ya elimu na ya mtoto na endapo mzazi yoyote atakmkiuka basi atachukuliwa hatua kali za kisheria mara moja.

Alisema tabia hiyo ni ukatili ma dhuluma kwa watoto na yeye kwa mamlaka yake atasimama kidete katika kuhakikisha kila mtoto kwenye Kata hiyo anapata haki ya kupata elimu pasipo kukatishwa kwa makusudi,mimba na ndoa za utotoni.

Aidha aliwasisitiza wazazi kuwaandikisha kwa wingi watoto wa darasa la Kwanza katika muhula ujao wa masomo wa mwezi Januari ili waweze kunufaika na sera ya elimu bure inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya 5 chini Rais Mh Dr John Pombe Joseph Magufuli.
 
Back
Top Bottom