Wazazi wangu wanataka kuachana, nifanyeje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wazazi wangu wanataka kuachana, nifanyeje?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Felixonfellix, Oct 5, 2011.

 1. Felixonfellix

  Felixonfellix JF-Expert Member

  #1
  Oct 5, 2011
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 1,680
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Tushirikiane kumshauri mtu huyu jamani:


  Naomba ndugu muniombee niko kwenye majaribu makubwa hadi inafika wakati najisikia sina hata nguvu ya kuomba. Mara kwa mara huwa najiuliza kama kweli Mungu yuko karibu nami. Lakini naamini siku moja Mungu atanikumbuka.

  Cha kwanza naomba muniombee, wazazi wangu wanataka ku-divorce, yaani baba yangu alishatuacha nyumbani mimi na wadogo zangu na mama yangu. Sasa wazazi hawasikilizani na wanataka ku-divorce. Mimi nimejaribu kuwaombea muda mrefu na kuwashauri lakini hawanisikii, nami kwa hivyo nimeshachoka na sijui nifanye nini.

  Kingine mnaonaje nikiwashauri wazazi wangu kuachana, kweli nitakuwa nimefanya dhambi? Sijui cha kufanya, lakini neno la Mungu linasema kama kilichounganishwa na Mungu mwanadamu asikitenganishe. Naomba mnisaidie hapo!

  Cha tatu naomba mnisaidie kuomba ili nipate mume mwema kutoka kwa Mungu kwa sababu mara nyingi naogopaga nasema labda sitakuja kuolewa. Sababu ni kuwa mambo ninayoyaona kwa wazazi wangu yananiogopesha sana hadi nakata tamaa, najiuliza hivi nikipata mume ambaye hatusikilizani hali itakuwa ya namna gani?.
  Jamani nawaombeni mnisadie sana kwa maombi na ushauri.
  Naitwa -------------- na nina miaka 25.
  Mungu awabariki sana!
   
 2. c

  c..rella Brains Member

  #2
  Oct 5, 2011
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 66
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  duh kwa hii story! we ni kama dada angu, lakin ye hayupo jeief. . . .au
  ok, ni mapito tu, endelea kusali sana, MUNGU anakusikia na anajua anachofanya! Pia huo mwenendo wa wazaz usikufanye wewe ukate tamaa, kila mtu ana njia yake utapata mume mzuri na mtaelewana. . .!
   
 3. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #3
  Oct 5, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 720
  Trophy Points: 280
  kifulambute toa ushauri kaka...
   
 4. Digna37

  Digna37 JF-Expert Member

  #4
  Oct 5, 2011
  Joined: May 17, 2010
  Messages: 835
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 60
  Pheeewwww! Mambo ya wazazi mdogo wangu ni magumu sana. Yalinitokea mimi miaka michache iliyopita tena wakiwa watu wazima kweli na wajukuu! Baba akasambaratisha mji mama akakimbilia kwaoooo miaka 2. Kila nilipofuatwa nilisema siingilii, hiyo ni ndoa yao kama wameamua kujitesa na kujiaibisha na kufanya nyumbani pasiwe mahali pa sie kufurahia kuwatembelea ni wao. Nilikaa kimya kabisa! Sikuingilia hata kidogo hata mama aliponipigia simu mara moja moja kutoa mashitaka, nilimsikiliza kwa makini kweli but baada ya kukata simu sikufanya lolote zaidi ya kuwaombea tu. Na baba aliponipigia simu kutoa mashitaka kuhusu mama nilimsikiliza kwa makini kweli, lakini baada ya kukata simu nilikaa kimyaaa!

  Walipochoka kutesana na kucheza hiyo sinema yao ya uzeeni mama alirudi kwake na yupo hadi sasa. Siwezi kusema mambo yametengemaa kama zamani lakini wanaelewana na mji upo tena.

  Hizo tabia za baba zetu ni kweli huwa zinatutisha sana kuolewa na mfano mimi, sikuwataka tena watu wa kutoka kwetu. Nilijiambia nafsi yangu, watakuwa kama baba yangu.... (mnisamehe wababa nasema ukweli toka moyoni). Sasa mdogo wangu, wewe muombe Mungu akusaidie, usimuone baba kama ndiye mkosaji sana, sometimes sisi tulifikia mahali tukamuona baba kama ana nafuu kuliko mama, na wakati mwingine tuliona kama baba mkosaji sana. Kwa hivyo, nakushauri kumwomba Mungu akupe mume mzuri atakayekupenda na kukufurahisha maisha yako yote na atakayejali familia, na wewe jiombee uje uwe mke mwema maana tunaomba waume wazuri na wema je, sisi wenyewe tukoje? Omba baraka za Mungu, na utaolewa tu ukikaa mkao wa kuolewa, usijifungie baraka ya ndoa.

  Barikiwa.
   
 5. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #5
  Oct 5, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Hapo kwenye Bold nyekundu sijaelewa kabisa......... hata sijui muandishi alikuwa na maana gani
   
 6. Felixonfellix

  Felixonfellix JF-Expert Member

  #6
  Oct 5, 2011
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 1,680
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Noted and edited mkuu


   
 7. TEMPOLALE

  TEMPOLALE JF-Expert Member

  #7
  Oct 5, 2011
  Joined: Aug 18, 2011
  Messages: 303
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Well said penye red, Mungu anasikiliza maombi. Mimi binafsi nimepewa mwanamke wa ndoto zangu baada ya maombi ninaye kwa miaka minane sasa. Nikisafiri au yeye akisafiri kwa siku chache tuu maisha yangu huwa magumu sana, sembuse kuachana!!!!!!!!!!!
   
 8. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #8
  Oct 5, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180
  Pole, endelea kuwaombea wayaelewana tu!
   
 9. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #9
  Oct 5, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,081
  Likes Received: 6,544
  Trophy Points: 280
  baba kwa muda huu anapuyanga nje, mama naye anapuyanga nje, mwisho wote wataleta maradhi ndani. kama ni makosa ya kusameheana na wafanye hivyo kama ni magumu wewe waache si kila mtu ana akili zake.

  kuhusu wewe wala usijali MUNGU alishakupangia maisha yako toka dunia inaumbwa ni wewe kumkumbusha tu kwa njia ya maombi.
   
 10. roby2006

  roby2006 JF-Expert Member

  #10
  Oct 5, 2011
  Joined: Sep 30, 2011
  Messages: 399
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Ugomvi wa baba na mama achana nao usiuingilie kabisa hujui baba yako alicho mfanyia mama yako na wala haujui mama alichomfanyia baba na wala uctake kujua kwasababu unaweza usitamani hata kuingia kwenye ndoa
   
 11. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #11
  Oct 5, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  Jitahidi uwe kiungo kipatanishi kati ya baba na mama. Piga magoti ukasali, ikiwezeka ufunge kwa ajili ya hilo.
   
 12. Rose1980

  Rose1980 JF-Expert Member

  #12
  Oct 5, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 5,701
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  pga goti ndugu
   
 13. Tulizo

  Tulizo JF-Expert Member

  #13
  Oct 5, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 849
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Wengi tumepitia kwa hayo maisha.. Hakuna anayependa..kuona wazazi wakigombana ..lakini hakuna jinsi kwani wao ni wanadamu....

  Ushauri wangu.. Uchukua worse scenario (yaani wazazi wanaachana) na uifanyie kazi..Yaani nyinyi watoto mtayumba vipi kiuchumi, masomo etc.. (hasa kama binafsi bado hujaanza kujitegemea) Washirikishe wakubwa na kuhakikisha mnapata haki zenu kama watoto ..hasa matunzo..

  Siri ya mafanikio yako 1. "usijihusishe kabisa wala kushiriki ugomvi wa wazazi".. 2. Kwa sababu wewe ni binti..kumbuka wanaume wote sio kama yule usiyempenda.
   
 14. feis buku

  feis buku JF-Expert Member

  #14
  Oct 5, 2011
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 2,371
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  mmh! unahisi itasaidia au sijakuelewa?!
   
 15. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #15
  Oct 5, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Ushauri ulompa ni mzuri kazi kwake kuufuata ili siku moja ujetimiza malengo yako yakuunganisha wazazi wako pamoja na kupata mume mwema. Pia na wewe jitahidi uwe mwema sio ukute mambo yako sio alafu unataka mume mwema. God bless u na akuongoze ktk kukabiliana na mtihani huu mgumu
   
 16. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #16
  Oct 5, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  hiyo ni comfusition kidogo nadhani alikuwa akimaanisha ALICHOUNGANISHA MUNGU MWANADAMU HAWEZI TENGANISHA
   
 17. Shostito

  Shostito Member

  #17
  Oct 5, 2011
  Joined: May 25, 2010
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pole mwaya.
   
 18. kikahe

  kikahe JF-Expert Member

  #18
  Oct 5, 2011
  Joined: May 23, 2009
  Messages: 1,273
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Mungu akutie nguvu ili uweze kuendelea kuwaombea wazazi. Hizo ni hila za shetani kusambaratisha ndoa ili na familia nzima isambaratike. Pia epuka kujinenea mabaya (Mf. Hivi nitakuja kuoelwa kweli?) Kumbuka kinywa huumba. Mungu akutie nguvu.
   
 19. u

  utantambua JF-Expert Member

  #19
  Oct 5, 2011
  Joined: Aug 1, 2011
  Messages: 1,373
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kuna ndoa moja ilikua na mgogoro wa miaka nenda miaka rudi Mungu anisamehe walipoachana nilishukuru sababu hiyo ndio ilikuwa wish yangu. Nilikua na wasiwasi huenda mmoja wao anaweza muua mwenzake siku moja kwa hasira/wivu wa kimapenzi ama mmoja wapo anaweza kujiua kwa frustration. Wameachana lakini sasa roho inaniuma jinsi kila mmoja wao anavoishi maisha ya upweke na kuhangaika. But naona hii ni afadhali kuliko kipindi walipokua wakiwa pamoja
   
 20. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #20
  Oct 5, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Ktk hili kumtegemea Mungu ndio tegemeo pekee
   
Loading...