Wazazi wanapoingilia penzi

the dose

New Member
Aug 24, 2010
4
0
habari zenu wana jamiii
nimekua nikiobserve mara nyingi inapofikia hatua ya watu kufunga ndoa wazazi huingilia kati either kumshauri mwanao aachane na mchumba wake au asifanye mambo kwa pupa....
swali linaloniumiza ni kwamba kama ww ni kijana na umeshazoeana na mtu wako ukaridhika nae wazazi wanapokwambia umwache au hafai je utachukua uamuzi gani....keep in mind to establish another new relationship takes time and energy:thinking:

...nakweli aisee...Inakuwaje mambo haya?

Achilia wazazi, hata mashoga, ndugu jamaa na marafiki atatokea mmoja wapo aanze kuwa influence wengine
mpaka 'bunge' zima linaanza kukushawishi uachane nae kwa sababu hata zisizoingi akilini, mfano;
• kwa kabila lake
• kwa imani yake ya dini
• kwa elimu yake
• kwa uzuri wake nk...
Kwani mtu hawezi jitambua mwenyewe bila watu kumlazimisha abadili maamuzi?
Mw'mungu aniongoze hivihivi, siku wanangu wanaleta mkwe nawapa support 100%..

Dear the dose na Mbu, ninaelewa jinsi inavyouma na kuchanganya. Ni kweli sometimes huwa na sababu ambazo yaani wewe huzielewi kabiisaaa but not all teh time wazazi wanakuwa hawana sababu ya msingi. Sometimes ni kama vile huwa wanaoteshwa au the instinct that they have huwa ni kali kama nyoka aisikiavyo harufu ya binadamu kutokea mbali. Ni mara nyingi tumesikia habari za watu walio'aswa' na wazazi wao juu ya kumwuoa/olewa flan na flani na mbeleni kukumbana na vimbwanga vya maisha ikisha kuishia kuambiwa.........si tulikwambia?'

Kuhusu taking time kuanzisha mahusiano mengine mwe.....sijui itakuwa sahihi kuanza kum'fahamisha' mtarajiwa wako mapema (hata kwa kivuli cha rafiki) kabla hujaamua kuwa ndiye au siye, ili kuwapa muda mzuri wazee wako kum'assess' na kumjua vema!! ingawa akiamua kuyaficha atayaficha tu

• Thanks
Reactions: Mbu

Mwj1 unajua tatizo nilionalo mimi li wapi?
Wao kinachowapelekea maamuzi yao hayo ni kutokana na experiences zao.

Mimi nadhani kila mtu ana haki kutahadharishwa, sio kukatazwa asioe/asiolewe na fulani.
Kila mtu ataubeba msalaba wake. Hata hapa JF utasikia wanawake wa Kimachame hatari, mara Ooh
Kabila fulani halifai... it's all MYTH!

Kama mke wangu mtarajiwa ni mvivu, hajui kupika, nk...yapo nilompendea mimi,
Mie ndie namjua mazuri yake mengine yanayofunika udhaifu wake huo.
Au nimekosea Mwj1?

Kuendekeza fulani kasema, ndio kiushikiwa akili kwenyewe huko.

Inawezekana wazazi wana nia njema.
Watu huweza kusoma tabia za watu. Mzazi anaweza kuhisi mkwe aliyeletewa si sahihi kuishi na mwanae kutokana na tabia alizoziobserve kutoka kwa huyo mkwewe. Hisia hizo zinaweza kuwa sahihi au lah.
Simaanishi kuwa nakubaliana na wazazi wanachokifanya ila nashauri inapotokea hvyo jaribu kuchunguza ndio ufanye maamuzi kuliko kuwapa lawama wazazi moja kwa moja.
Wapo watu walioolewa/oa ingawa walikatazwa na wazazi wao aina ya wake/wanaume wao waliokuwa nao na mwisho wa siku hujuta na kutamani wangesikiliza ushauri wa wazazi.
Hili suala ni la kuliangalia pande mbili ingawa kwa sababu za kiutandawazi (globalization) tunaona ni jambo lililopitwa na wakati.

Sawa kabisa Mbu nimekuelewa concern yako.but hebu tujiulize mbona wazee wetu walikuwa wanatafutiwa/shurutishwa kuolewa na fulani/kumwuoa flani? naamini hizi choices pia zilibase kwenye decisions za wazee na si za wahusika au? why inakuwa ngumu now??

Sawa kanbisa Hus, ingawa ni sawa na anachosema Mbu kuwa wakutahadharishe yes but not kukukataza. Wakuonye yes lakini si kukuzuia kwa kutumia cheo chao cha uzazi......mie namkumbuka dada mmoja alipeleka mchumba wake kwao...Mama yake akamwuliza mwanangu, wa huko (Mkoa) utamuweza kweli? hawafai hao (hakutoa sababu) ikawa kama laana vile, ndoa ilivinjika baada ya miezi 7. !! So soetimes maneno nayo yanaumba sijui ndo laana zenyewe!?

Lawama naamini hazikosekani pande zote.
Yawezekana ukakataliwa usimuoe/usiolewe na fulani ukaishia maisha yako yote
huna raha na furaha kwenye ndoa yako, na hata mapenzi kwa mkeo/mumeo na wazazi yako yakaathirika
kwa kiwango kikubwa sana.

Nadhani wakati umetusaidia kujichungua zaidi na kufahamu lipi wenza wetu wanataka, tofauti na miaka ile
ambako kigezo kikuu cha Mke/Mume kilikuwa Kabila lake, na tabia za kwao. Siku hizi si ajabu tena
Mmanyema wa Pwani kumuoa Mchaga wa Tanga. Ukabila si hoja tena.

Ni vizuri sana kuwasikiliza wazazi (si marafiki!) kwani hakuna mzazi anayemtakia baya mwanae. Mdogo wangu alimleta jamaa yake home; mama hakumpenda na hata baba hakumpenda pia wakati baba na mama hawakai pamoja kila mmoja alimponda kwa muda wake. Mdogo wangu aliumia sana mimi nikawa nampa moyo but deep inside na mimi nikawa naona kama wazazi hawaja approve ni bora wahachane. Ila kwa kuwa alikuwa amechanganyikiwa na anahitaji comfort nikamwambia wape muda wazazi watalainika wenyewe. Mimi sababu walizosema wazazi sikuona kama ni za msingi. Kwanza walikuwa hawamjuhi kabisa kijana. Ila baba yeye alisema hilo kabila la jamaa wanaume hawana heshima ya familia; eti kulala nje na kuwa na nyumba ndogo ni sifa na akatoa mifano kadhaa including ya majirani zetu. Mama yeye akasema analijua lile kabila ni washirikina kupitiliza na mume akifa utanyang'anywa kila kitu akatoa mifano ya rafiki zake. Mdogo wangu hakumwacha jamaa yake na wazazi wala hawakusema wanamlazimisha ila wamemwambia fact ili aamue akiwa anajua future itakuwaje. Huwezi amini hata mwaka haukuisha mdogo wangu akampiga chini jamaa kwa sababu nyingine kabisa ila naona moyoni tayari alikuwa influenced na maneno ya wazazi. Sababu zilisomfanya ampige chini ni kuwa jamaa anaringa sana na anawasikiliza sana dada zake kiasi kwamba ni kama vile hata kuwa na yeye ni approval ya dada zake. Sasa hivi kaolewa na jamaa ambaye wazazi hawakutia neno?

Nina mifano mingi ya waliosikiliza wazazi na waliodharau maneno ya wazazi. Ushauri wangu wazazi wakisema kitu inakuwa sijuhi kama laana maisha lazima yataenda ndivyo sivyo ukipuuzia. Sijuhi wana maono kama mdau alivyosema hapo juu.

Sawa kabisa Mbu nimekuelewa concern yako.but hebu tujiulize mbona wazee wetu walikuwa wanatafutiwa/shurutishwa kuolewa na fulani/kumwuoa flani? naamini hizi choices pia zilibase kwenye decisions za wazee na si za wahusika au? why inakuwa ngumu now??

Sawa kanbisa Hus, ingawa ni sawa na anachosema Mbu kuwa wakutahadharishe yes but not kukukataza. Wakuonye yes lakini si kukuzuia kwa kutumia cheo chao cha uzazi......mie namkumbuka dada mmoja alipeleka mchumba wake kwao...Mama yake akamwuliza mwanangu, wa huko (Mkoa) utamuweza kweli? hawafai hao (hakutoa sababu) ikawa kama laana vile, ndoa ilivinjika baada ya miezi 7. !! So soetimes maneno nayo yanaumba sijui ndo laana zenyewe!?

...kama nilivyojibu awali,....
wazee wa zamani naamini hisia zao zilijengwa kutokana na imani potofu.
Mbona nishasikia mara nyingi eti sie wamanyema tuliogopewa sababu eti tunakula watu?
Yale yale ya wanawake wa kimachame mpaka sasa eti wanaogopewa kwa kuua waume zao.

Ni imani potofu tu zilizopelekea jamii kukimbia hayo.
Ni sawa na sifa kuu za Wapare kuuza Ng'ombe kupatia pesa za kuendesha kesi ya kuku!
Vikwazo vya miaka ile vilienga zaidi na imani potofu...
Imagine, hata kuzaliwa watoto mapacha ilikuwa ni NUKSI!...

Hilo la laana, nadhani nisubiri wengine waje wadodose hilo..
Nakimbilia kuchangia pato la taifa mida hii..

• Thanks
Reactions: BAK
Lawama naamini hazikosekani pande zote.
Yawezekana ukakataliwa usimuoe/usiolewe na fulani ukaishia maisha yako yote
huna raha na furaha kwenye ndoa yako, na hata mapenzi kwa mkeo/mumeo na wazazi yako yakaathirika
kwa kiwango kikubwa sana.

Nadhani wakati umetusaidia kujichungua zaidi na kufahamu lipi wenza wetu wanataka, tofauti na miaka ile
ambako kigezo kikuu cha Mke/Mume kilikuwa Kabila lake, na tabia za kwao. Siku hizi si ajabu tena
Mmanyema wa Pwani kumuoa
Mchaga wa Tanga. Ukabila si hoja tena.

Hah Mchaga wa Tanga tena .....ndo kabila gani hili we Mbu? LOL

Ni kweli so haya mabadiliko tunayoyaexperience kizazi cha leo ni wazi hayaeleweki hata kidogo kwa kizazi cha kale. Ingawa sometimes naona kidooogo wazee wetu wanaelewa hawakazii kiviiile kuwa usioe/olewe na flani.

But nadhani bado tuna changamoyo kwenye ku'itikia' miito ya hisia za mapenzi yetu kwa tunaowachagua......Imagine umefaal kwa mwanamke/mume ambaye alishakuwa na ndoa akaacha/achwa/ mwenye watoto wakubwa hata kama mmekutana ukubwani sometimes kuna kipingamizi hasa kwa upande wa mume kuwa ...utaoaje huyu aloachika/achwa au mwenye watoto kwa mwanaume/wanaume wengine?......hii bado ni changamoto unless muamue tu ku-elope.

Ni vizuri sana kuwasikiliza wazazi (si marafiki!) kwani hakuna mzazi anayemtakia baya mwanae. Mdogo wangu alimleta jamaa yake home; mama hakumpenda na hata baba hakumpenda pia wakati baba na mama hawakai pamoja kila mmoja alimponda kwa muda wake. Mdogo wangu aliumia sana mimi nikawa nampa moyo but deep inside na mimi nikawa naona kama wazazi hawaja approve ni bora wahachane. Ila kwa kuwa alikuwa amechanganyikiwa na anahitaji comfort nikamwambia wape muda wazazi watalainika wenyewe. Mimi sababu walizosema wazazi sikuona kama ni za msingi. Kwanza walikuwa hawamjuhi kabisa kijana. Ila baba yeye alisema hilo kabila la jamaa wanaume hawana heshima ya familia; eti kulala nje na kuwa na nyumba ndogo ni sifa na akatoa mifano kadhaa including ya majirani zetu. Mama yeye akasema analijua lile kabila ni washirikina kupitiliza na mume akifa utanyang'anywa kila kitu akatoa mifano ya rafiki zake. Mdogo wangu hakumwacha jamaa yake na wazazi wala hawakusema wanamlazimisha ila wamemwambia fact ili aamue akiwa anajua future itakuwaje. Huwezi amini hata mwaka haukuisha mdogo wangu akampiga chini jamaa kwa sababu nyingine kabisa ila naona moyoni tayari alikuwa influenced na maneno ya wazazi. Sababu zilisomfanya ampige chini ni kuwa jamaa anaringa sana na anawasikiliza sana dada zake kiasi kwamba ni kama vile hata kuwa na yeye ni approval ya dada zake. Sasa hivi kaolewa na jamaa ambaye wazazi hawakutia neno.

Nina mifano mingi ya waliosikiliza wazazi na waliodharau maneno ya wazazi. Ushauri wangu wazazi wakisema kitu inakuwa sijuhi kama laana maisha lazima yataenda ndivyo sivyo ukipuuzia. Sijuhi wana maono kama mdau alivyosema hapo juu.

dahhh, ndio kusema mama/baba akisema sitaki uoe/uolewe na fulani ndoa ndio imekwisha hiyo?
lahhh...inauma sana iwapo mlipendana kiukweli.
Sababu za maana mfano, Ulevi, Uzinzi, Uvivu wa kazi, Maradhi ya kurithi, nk kidogo zinaingia akilini...
lakini si kwasababu ya kabila lake, dini yake, nk...

Sawa kanbisa Hus, ingawa ni sawa na anachosema Mbu kuwa wakutahadharishe yes but not kukukataza. Wakuonye yes lakini si kukuzuia kwa kutumia cheo chao cha uzazi......mie namkumbuka dada mmoja alipeleka mchumba wake kwao...Mama yake akamwuliza mwanangu, wa huko (Mkoa) utamuweza kweli? hawafai hao (hakutoa sababu) ikawa kama laana vile, ndoa ilivinjika baada ya miezi 7. !! So soetimes maneno nayo yanaumba sijui ndo laana zenyewe!?

kupewa tahadhari ni jambo la maana kuliko kukatazwa ila nafikiri sisi watoto ambao hatujaolewa/hatujaoa huwa mara nyingine hatuwapi fursa wazazi za kutupa tahadhari.
Mzazi anapokukataza ni vizuri kuongea nae kujua tatizo lipo wapi kwa mkwewe. Unapozungumza nae ni rahisi kubadilisha msimamo wake wa kukukataza na kuwa msimamo wa tahadhari.
Tatizo vijana sisi tunapokatazwa tunaanza kuwafikiria vibaya wazazi wetu, tunaanza kutangaza, tunapanic na kukosa raha.
Kwahiyo ni muhimu kutoa fursa kwa mzazi kujadili hilo suala inapotokea hvyo maana inawezekana mzazi alifikisha ujumbe kwa hasira hvyo kuonekana kama anakukataza wakati alikuwa na nia ya kukupa tahadhari.

• Thanks
Reactions: Mbu
Inawezekana wazazi wana nia njema.
Watu huweza kusoma tabia za watu. Mzazi anaweza kuhisi mkwe aliyeletewa si sahihi kuishi na mwanae kutokana na tabia alizoziobserve kutoka kwa huyo mkwewe. Hisia hizo zinaweza kuwa sahihi au lah.
Simaanishi kuwa nakubaliana na wazazi wanachokifanya ila nashauri inapotokea hvyo jaribu kuchunguza ndio ufanye maamuzi kuliko kuwapa lawama wazazi moja kwa moja.
Wapo watu walioolewa/oa ingawa walikatazwa na wazazi wao aina ya wake/wanaume wao waliokuwa nao na mwisho wa siku hujuta na kutamani wangesikiliza ushauri wa wazazi.
Hili suala ni la kuliangalia pande mbili ingawa kwa sababu za kiutandawazi (globalization) tunaona ni jambo lililopitwa na wakati.

Ni kweli Husninyo, Wazazi wana nia njema na mtoto wao, lakini wakati huo huo mara nyingi hawataki kutafuta muda wa kumfahamu muhusika kama anastahili kupewa baraka zao za kumuoa/kuolewa na kijana wao. Siku hizi watoto wengi ni vichwa ngumu mara nyingi Wazazi wanapoweka vikwazo mtoto huamua kusonga mbele bila baraka zao. Na mara nyingi wapenzi hawa huweka extra efforts katika ndoa yao ili kuwaonyesha Wazazi kwamba walikosea walipoweka pingamizi bila hata ya kutafuta muda wa kumfahamu mkwe wao vizuri. Na ndoa ikifanikiwa basi wanakuwa hawana jinsi bali kuikubali ndoa ile. Wazazi wengine wanakuwa wastaarabu na kukubali makosa yao kwa wanandoa hao na wengine wanaminya tu.

• Thanks
Reactions: Mbu

...kama nilivyojibu awali,....
wazee wa zamani naamini hisia zao zilijengwa kutokana na imani potofu.
Mbona nishasikia mara nyingi eti sie wamanyema tuliogopewa sababu eti tunakula watu?
Yale yale ya wanawake wa kimachame mpaka sasa eti wanaogopewa kwa kuua waume zao.

Ni imani potofu tu zilizopelekea jamii kukimbia hayo.
Ni sawa na sifa kuu za Wapare kuuza Ng'ombe kupatia pesa za kuendesha kesi ya kuku!
Vikwazo vya miaka ile vilienga zaidi na imani potofu...
Imagine, hata kuzaliwa watoto mapacha ilikuwa ni NUKSI!...

Hilo la laana, nadhani nisubiri wengine waje wadodose hilo..
Nakimbilia kuchangia pato la taifa mida hii..

We nae na shift zako za Usiku ah!! aksante kwa mchango nway.

Hapo kwenye imani potofu mh nachelea kukukubalia 100% kwa sababu sometimes haya waliyokuwa namasema/hofia yalikuwa yanatokea kweli!! I mean why waseme wamachame wanaua waume zao (Sio kwa kuwa kuna matukia yaliyokuwa ya kweli enzi hizo?- mimi sijui kwa sababu ni 'mtoto' sana katika mila na desturi na mambo ya huko) ?

Wamanyema kwa nini walikuwa wanahisiwa wanakula watu?? Carnibalism ndo mnaitaga hiyo tabia??

• Thanks
Reactions: Mbu
Kama una amini kuwa kuheshimu wazazi kunaongeza baraka pale wanapokupinga au kukushauri chukua muda kufanyia kazi ushauri wao. Ndoa ni mapenzi moto moto mwanzo kuna ups and downs baadae. Sasa kama ulioa/olewa kwa mbwembwe na jeuri ndio wale mtu ananyanyasika lakini anakomaa kwani anahisi akiwambia wazazi na ndugu watamcheka kuwa walimwambia akawaona machizi.

Raha sana ukioa/olewa na mtu ambaye wazazi wamemkubali. Wakipinga vuta muda utaanza kuona wanayosema kama umevuta muda na bado waona he/she is the one oa/olewa. Mimi nina mpaka marafiki zangu wanakiri kuwa waliambiwa na wazazi wasiolewe na waume walionao. Sasa hivi wanaliona joto la jiwe na hawathubutu kushare na ndugu zao matatizo walonayo.

dahhh, ndio kusema mama/baba akisema sitaki uoe/uolewe na fulani ndoa ndio imekwisha hiyo?
lahhh...inauma sana iwapo mlipendana kiukweli.
Sababu za maana mfano, Ulevi, Uzinzi, Uvivu wa kazi, Maradhi ya kurithi, nk kidogo zinaingia akilini...
lakini si kwasababu ya kabila lake, dini yake, nk...

habari zenu wana jamiii

nimekua nikiobserve mara nyingi inapofikia hatua ya watu kufunga ndoa wazazi huingilia kati either kumshauri mwanao aachane na mchumba wake au asifanye mambo kwa pupa....

swali linaloniumiza ni kwamba kama ww ni kijana na umeshazoeana na mtu wako ukaridhika nae wazazi wanapokwambia umwache au hafai je utachukua uamuzi gani....keep in mind to establish another new relationship takes time and energy

sometimes ushauri wa wazazi ni muhimu, huwezi jua ni kwa nini wanafanya hivyo
1. Huenda ni kutokana na historia ya wazazi wake! Kumbuka siku zote maji hufuata mkondo.
2. Siku yatakapokuharibikia utakwenda kwa mzazi gani endapo hutamsikiliza yeye?
3. Usisahau pia mara nyingi vijana chini ya miaka 25 hupenda kwa kusukumwa na tamaa zaidi, hivyo mzazi anakushauri kwa nia ya kukuweka katika mapenzi sahihi

NB, si lazima kumsikiliza mzazi wako kama unaona uko sahihi.

• Thanks
Reactions: Mbu
Lawama naamini hazikosekani pande zote.

Yawezekana ukakataliwa usimuoe/usiolewe na fulani ukaishia maisha yako yote

huna raha na furaha kwenye ndoa yako, na hata mapenzi kwa mkeo/mumeo na wazazi yako yakaathirika

kwa kiwango kikubwa sana.

Nadhani wakati umetusaidia kujichungua zaidi na kufahamu lipi wenza wetu wanataka, tofauti na miaka ile

ambako kigezo kikuu cha Mke/Mume kilikuwa Kabila lake, na tabia za kwao. Siku hizi si ajabu tena

Mmanyema wa Pwani kumuoa Mchaga wa Tanga. Ukabila si hoja tena.

ni kweli mbu ila huyo mchaga wa tanga nayo kali. Ila mimi nasisitiza tuwape fursa wazazi ya kusikiliza sababu zao. Ikibidi tujitahidi kubadilisha fikra/hisia/misimamo yao ili tupate baraka zao.

• Thanks
Reactions: Mbu
Kama una amini kuwa kuheshimu wazazi kunaongeza baraka pale wanapokupinga au kukushauri chukua muda kufanyia kazi ushauri wao. Ndoa ni mapenzi moto moto mwanzo kuna ups and downs baadae. Sasa kama ulioa/olewa kwa mbwembwe na jeuri ndio wale mtu ananyanyasika lakini anakomaa kwani anahisi akiwambia wazazi na ndugu watamcheka kuwa walimwambia akawaona machizi.

Raha sana ukioa/olewa na mtu ambaye wazazi wamemkubali. Wakipinga vuta muda utaanza kuona wanayosema kama umevuta muda na bado waona he/she is the one oa/olewa. Mimi nina mpaka marafiki zangu wanakiri kuwa waliambiwa na wazazi wasiolewe na waume walionao. Sasa hivi wanaliona joto la jiwe na hawathubutu kushare na ndugu zao matatizo walonayo.

Aksante nyumba kubwa umeiweka vizuri sana....... watakuasa juu ya mwenza wako kisha weye utake time kuyachunguza uloasiwa!! usiichukulie juu juu tu. Mbu amesema ataelewa iwapo makatazo hayo yanahusu magonjwa ya kurithi na vitu kama hivyo lakini si kwa kabila au dini.....nadhani ni sawa tabu ni kuwa siku hizi mpaka tunafikishana kwa wazee inakuwa tushamaliza kila kitu.yaani tunakuwa tushainvest mali mpaka hisia sasa unapokujaambiwa HAPANA lazima uwe mbishi..............ndio maana tuna cases nyingi za waliojiua kwa kukatazwa kuolewa na flani.
Afu kitu kingine ambacho wengine tunakosea ni kule, umeaswa hafu nawe mbio wendamweleza mwenzio plainly.........Baba/Mama wamenikataza eti wewe uko hivi, na vile...bila kutambua kuwa tunajenga ufa katika mahusiano ya mwenza na m/wakwe zake kungali mapema

• Thanks
Reactions: Mbu

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom