Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,597
- 215,272
Ninakumbuka miaka ya 1980 enzi zile Afrika ya Kusini siasa za ubaguzi wa rangi zimetamalaki. Nchi nyingi zilijitenga na Afrika ya Kusini, passport ya Tanzania iliandikwa kabisa hairuhusu mmiliki kuingia nchi hiyo
Jirani yetu Baba yao alifanikiwa kupata kazi Afrika ya Kusini kwenye migodi ya madini. Yule mzee alirudi kwa kujificha na alikaa wiki si zaidi ya wiki mbili. Aliondoka usiku
Familia yake waliweza kujenga nyumba yenye hadhi. Watoto walivaa raba mtoni na ada za shule walipata. Lakini kukua bila malezi ya baba nayo ni changamoto
wazazi wakisha pata watoto, wanajitoa sana kuhakikisha watoto wanapata mahitaji yao, ikiwemo kutengana na familia kwa muda mrefu