Wazazi wanachangia sana kuua future za watoto wao. Elimu sio kila kitu

MURUSI

JF-Expert Member
Jun 25, 2013
4,468
8,685
Vuta picha mkiwa Primary school au Secondary enzi hizo. Kuna watu walikuwa ni wakiambiaji balaa leo hii wangekuwa wanashindana na wakina Bolt wa Jamaica, Ila where are they? Wazazi waliaminisha kwenye kusoma na leo hii wengine labda ni madereva na wengine hawana hata future tena.

Vuta picha kwenye soka, shule ya Msingi na Secondary kuna vijana walikuwa wanacheza mpira wewe acha kabisa yaani kwa kiwango kile leo hii angekuwa hata anakipiga Hispania au Ufaransa. Ila walikomaliwa wasome na leo hii si chochote tena.

Vuta picha kwenye sanaa kama kuchora picha kuna wanafunzi walikuwa ni hodari mno kwa kuchora picha je wako wapi leo?

Vuta picha kwenye kuimba wapo walio kuwa hodari mno na wana sauti kama za wakina Whitney Houston ila kwa sasa inaweza kukuta walishaolewa wako tu.

Elimu sio kila kitu kwenye life.

Diamond angekomaliwa kusoma leo hii angekuwa bwana shamba labda. Ali Kiba labda angekuwa kondakta wa daladala za Mbagala huko.

Wakina Ronaldo De Lima sidhani kama walisoma ila walitingisha dunia na dunia ilisimama. Wakina Messi vipi wazazi wao wangewaambia wasome tu leo hii angekuwa wapi?

Wakina Michael Jackson hawakuwa na elimu kubwa ila walisimamisha dunia na vipi kama wazazi wa Michael wangemwambia Michael akazane na elimu je leo hii angekuwa wapi?

Elimu ni muhimu ila elimu sio kila kitu kwenye maisha. Unawesa usiwe na elimu na ukatingisha dunia na unaweza kuwa na eliimu pia ukatingisha dunia.

Unaweza kuwa na elimu na ukawa na maisha magumu sana na unaweza kuwa na elimu ukawa na maisha mazuri pia unaweza usiwe na elimu na ukawa biilionaire na unaweza usiwe na elimu na ukawa maskini.

Watoto waachwe wa implement vipaji vyao acheni kuwashindilia tuition na kwenda kukaririshwa mito. Mtoto anakaririshwa mito ya Tanzania itamsaidia nini kwenye maisha?


=====
MAWAZO YA WACHANGIAJI

Pamoja na maneno mengi usitake kuwatupia lawama wazazi! Hakuna mzazi asiyependa mtoto wake asifanikiwe kimaisha. Mzazi anajitahidi kumpa kile ambacho anadhani kitamsaidia wakati huohuo mtoto naye sio kama robotic kukubali kila kitu kutoka kwa wazazi.

Mtoto kama anakipaji, hicho kipaji kinakuwa ndani ya damu na hakijifichi na kitamuwinda hata akiwa shuleni. Mbona akina Billgate, Steve job, yule tajiri wa amazon n.k walipelekwa shule na wazazi wakakataa na kuingia mitaani vipaji vikawatoa. Ukiwa na kipaji na unaelimu uwezekano wa kudumu katika hivyo vipaji ni mkubwa kuliko yule ambaye hana elimu. Mfano Michael Tyson anakipaji lakini kukosa elimu uenda imechangia kuwa masikini na ombaomba kama alivyo sasa.

Wako wengi wanavipaji mitaani lakini kwa kukosa elimu wanakosa exposure na uwezekano wa kuviendeleza. Tushukuru siku hizi watoto wanasoma wakiwa wadogo angalau mtoto akianza darasa la kwanza na miaka 5 atamaliza kidato cha 4 na miaka 15 umri ambao kama anakipaji anakuwa na maamuzi ya kufuata cha mzazi au kipaji chake! Wazazi tutaendelea kuwasisitiza elimu kuwa na uwanja mpana wa kuwasaidia vijana wetu kuliko blahblah za motivational speakers! Narudia! Kama ni kipaji kitakuwinda huwezu kukikwepa na hakuna wa kukuzuia. Utaenda nacho hivyo hivyo shuleni walimu watakiona mtaani wazazi na kila mtu ataona by the time unamaliza form four at least bilashaka maamuzi yanakuwa sahihi
 
Ulichokisema kina ukweli hasa kwenye hii elimu yetu ya kusoma ili uajiriwe. Sasa hivi mtaani wasomi waliokosa kuajiriwa wanafanya kazi za watu ambao hawakusom. kuuza uji, mitumba, miamala ya pesa, kufuga kuku nk. Hapo mtu Kesha poteza muda, nguvu na pesa.
 
Kuna mambo ambayo hayaitaji madesa, mfano kuelewa kilichoandikwa hapo juu. Huyo jamaa anafikiri kila ki2 ni madesa Mada inahusu maisha yeye anawaza geography
 
Ngoja sasa nijikite kwenye mada, Elimu ni muhimu sema tu ni muhimu pia mtoto mwenye kipaji fulani mfano kuimba,mpira n.k.Ni vyema mtoto akionekana na kipaji cha kuimba kumsaidia katika kufika katika ndoto zake za uimbaji mfano kumuandikisha kwenye leçons za music. Anaependa kusoma pia awezeshwe kusoma.

Mfano De Lima alikuwa kilaza sana darasani na alikuwa anapenda mpira. Mama yake alikuwa anapenda kucheza kamari ili siku moja ashinde ma milion kumbe mamilion alikuwa nayo ndani(Ronaldo de Lima)
 
Ngoja sasa nijikite kwenye maada,Elimu ni muhimu sema tu ni muhimu pia mtoto mwenye kipaji flani mfano kuimba,mpira n.k.Ni vyema mtoto akionekana na kipaji cha kuimba kumsaidia katika kufika katika ndoto zake za uimbaji mfano kumuandikisha kwenye leçons za music.Anaependa kusoma pia awezeshwe kusoma.

mfano De lima alikuwa kilaza sana darasani na alikuwa anapenda mpira.Mama yake alikuwa anapenda kucheza kamari ili siku moja ashinde ma milion kumbe mamilion alikuwa nayo ndani(Ronaldo de Lima)

Ahaa alikuwa anaacha dhahabu anaokota mawe?
 
Wengi wa Watanzania hawatofahamu ujumbe wako, hawajui wengi wa mabilionea Dunia ni watu waliokuwa hawakumaliza elimu ya juu
Nani kakwambia kila mtu anataka kuwa bilionea? kuna watu wamezaliwa kutoa huduma kwa wengine, kuna wengine mafanikio kwao ni elimu na maisha ya kawaida tu.
 
Ulichokisema kina ukweli hasa kwenye hii elimu yetu ya kusoma ili uajiriwe. Sasa hivi mtaani wasomi waliokosa kuajiriwa wanafanya kazi za watu ambao hawakusom. kuuza uji, mitumba, miamala ya pesa, kufuga kuku nk. Hapo mtu Kesha poteza muda, nguvu na pesa.
Na wewe unarudi mulemule hakuna kazi za wasiosoma cha msingi ni focus.
 
Umeongea vizuri sema unachanganya kati ya shule( formal education) na elimu.

Elimu ni kila kitu ila shule sio kila kitu, elimu ni jumla ya maarifa, stadi/ ujuzi na muelekeo alionao/ apatao mtu. Shule ni sehem moja wapo ya kupata hiyo elimu yenyewe.

Tafuta types of education utaelewa zaidi .

By the way, uko sahihi kabisa, school kill creativity
 
Back
Top Bottom