Wazazi walipishwa michango shule za msingi jijini Dar es Salaam

Tairi bovu

JF-Expert Member
Sep 28, 2017
3,063
2,983
Amani iwe kwenu.
Huku wananchi wakiendelea kuaminishwa kuwa elimu ya shule primary hadi Sekondari ni bure. Bure kabisa na kwamba wananchi masikini wanafaidika.

Hali imekuwa tofauti kwa shule nyingi mkoani Dar es salaam. Wazazi wanatakiwa kwenda kuchukua ripoti za matokeo ya watoto wao huku wakiwa na kati ya shilingi 5000- 10,000 tena bila risiti kwa ajili ya ( ujenzi, ulinzi ama maendeleo ya shule) sababu hutofautiana kutegemea na shule.Wazazi wenye watoto wao wanaposhindwa kulipa hawapewi ripoti kabisa.

Watu wanahoji maana ya eelimu bure inayohubiriwa na mamlaka ni ipi? Je sio kweli kwamba serikali inauhadaa umma? Badala ya kutumia mamilion ya walipa kodi kuboresha elimu ya watoto sisi twawahonga wabunge wa upinzani na kubaki tukikenua, wabunge wanaohama ili kuunga mkono hawana budi kujibu kwanza na haya kama ni miongoni mwa juhudi wanazounga mkono au laa.

Waziri wa elimu una chakueleza?

Tujadili
 
Ungetaja jina la shule INGEPENDEZA zaidi. Ila ninachojua kuwa katika baadhi ya shule wazazi wanakubaliana kulipia michango ya ulinzi na hata ujenzi wa mabweni kwani fedha za kugharamia matumizi hayo hazitolewi na serikali
 
Alieyeleta huu uzi ni mchochezi na kibaraka wa majizi,nani aiyejua tupo kwenye vita ya kiuchumi na kati yetu kuna vibaraka kama mleta uzi?
Kamanda mambosasa amesema kama una information kama hizi uzipeleke panapostahili,wizara ya elimu huko
Uzi huu upuuuzwe una lengo la kumkosanisha Rais na kurudisha nyuma juhudi zako za elimu bure
 
Hii ni principle ya bwana mjinga inayosema; huyu bwana ni mgumu na huwa anavuna asipopanda.
Hivi inawezekanaje mtoto wako asome weee mwaka mzima ushindwe kulipa buku tano
Imaskini huathiri afya ya akili

Kabisaaaa na n ujinga wa kiwango cha PhD,nataman Magufuli afute elimu bure,

Wazazi wamekuwa watu wa hovyo sanaaaaa,ikitokea hata dharura ya kuchangia sh 2000 wazaz hawachangii kwa sababu ya elimu bure......

Kiukweli ubora wa elimu umepungua kabisaaaaa....

Mm namshauri Magufuli wazazi wachangie michango ya shule aachane na elimu bure......

Wazazi wengine wameacha kabisa kufuatilia maendeleo ya wanao kwa sabb ya elimu n bora liende tu ili mzazi awe na uchungu lazima achangie michango ya shule
 
Kuna vitu lazima tuvikatae kuanzia level ya individual mpaka taifa. Hivi inawezekana vipi mwanao asome kama kifurushi cha jaza ujazwe cha Tigo? Lipia elimu ya mwanao siasa waachie wana siasa.

Walisema hawatowachagua wapinzani sasa wanawabuy kabisa

Walisema watatoa kumputa na mil. 50 kimya

Walisema ni ile ile loooh ni ile ileee sasa imekuwa ya bwana kheri mpaka wahamiaji haramu nao wa naenda kwa sababu ya bwana yule.

Bora elimu ichangiwe watu wasome buku tano per year?
Tuwe serious jaman
 
Wananchi wajiongeze waache ujingaaaaa
 
Kabisaaaa na n ujinga wa kiwango cha PhD,nataman Magufuli afute elimu bure,

Wazazi wamekuwa watu wa hovyo sanaaaaa,ikitokea hata dharura ya kuchangia sh 2000 wazaz hawachangii kwa sababu ya elimu bure......

Kiukweli ubora wa elimu umepungua kabisaaaaa....

Mm namshauri Magufuli wazazi wachangie michango ya shule aachane na elimu bure......

Wazazi wengine wameacha kabisa kufuatilia maendeleo ya wanao kwa sabb ya elimu n bora liende tu ili mzazi awe na uchungu lazima achangie michango ya shule
Wewe unakurupuka kuwalaumu wazazi bure tu, sasa kabla ya mahubiri ya elimu bure waliwahi kukulilia kwamba wameshindwa kuwasomesha watoto wao? Wanakosa gani kuhoji kuhusu malipo hayo kwa kuwa wao wameaminishwa ni elimu bure? UVCCM bwana!
 
Wazazi wajiongeze waache siasa.....
 
Amani iwe kwenu.
Huku wananchi wakiendelea kuaminishwa kuwa elimu ya shule primary hadi secondari ni bure. Bure kabisa na kwamba wananchi masikini wanafaidika. Hali imekuwa tofauti kwa shule nyingi mkoani dar es salaam. Wazazi wanatakiwa kwenda kuchukua ripori za matokeo ya watoto wao huku aakiwa na kati ya shilingi 5000- 10000 tena bila risiti kwa ajili ya ( ujenzi, ulinzi ama maendeleo ya shule) sababu hutofautiana kutegemea na shule.

Wazazi wenye watoto wao wanaposhindwa kulipa hawapewi ripoti kabisa. Watu wanahoji maana ya eelimu bure inayohubiriwa na mamlaka ni ipi? Je sio kweli kwamba serikali inauhadaa umma? Badala ya kutumia mamilion ya walipa kodi kuboresha elimu ya watoto sisi twawahonga wabunge wa upinzani na kubaki tukikenua, wabunge wanaohama ili kuunga mkono hawana budi kujibu kwanza na haya kama ni miongoni mwa juhudi wanazounga mkono au laa.

Wazir wa elimu una chakueleza?

Tujadili
Katika watu ambao thinking capacity yao ni sifuri ni huyu aliye leta huu uzi, yaani unazaa ili watu wengi wakulelee? Mhs Rais ameonesha pa kuanzia sio kila kitu yeye fikili tena tafadhali
 
michango inaruhusiwa au hairuhusiw?i Raisi alishasema ni bure unaelewa maaana ya bure? Halafu mnamshambulia mtoa maada jibuni hoja zake, Au na nyie ni waalim maslahi yenu yameguswa?
 
Jamani watu Kama watoa uzi msitafsiri elimu bure kwa namna isiyofaa. Wazazi watimize wajibu wao. Serikali ni pamoja na jamii.
 
Mara kadhaa nimemsikia waziri akielezea vizuri tu maana ya elimu bure, we mleta uzi acha upoyoyo,uzae mitoto yako ushindwe kulipa 5000 kwa mwaka?
 
Back
Top Bottom