Tairi bovu
JF-Expert Member
- Sep 28, 2017
- 3,063
- 2,983
Amani iwe kwenu.
Huku wananchi wakiendelea kuaminishwa kuwa elimu ya shule primary hadi Sekondari ni bure. Bure kabisa na kwamba wananchi masikini wanafaidika.
Hali imekuwa tofauti kwa shule nyingi mkoani Dar es salaam. Wazazi wanatakiwa kwenda kuchukua ripoti za matokeo ya watoto wao huku wakiwa na kati ya shilingi 5000- 10,000 tena bila risiti kwa ajili ya ( ujenzi, ulinzi ama maendeleo ya shule) sababu hutofautiana kutegemea na shule.Wazazi wenye watoto wao wanaposhindwa kulipa hawapewi ripoti kabisa.
Watu wanahoji maana ya eelimu bure inayohubiriwa na mamlaka ni ipi? Je sio kweli kwamba serikali inauhadaa umma? Badala ya kutumia mamilion ya walipa kodi kuboresha elimu ya watoto sisi twawahonga wabunge wa upinzani na kubaki tukikenua, wabunge wanaohama ili kuunga mkono hawana budi kujibu kwanza na haya kama ni miongoni mwa juhudi wanazounga mkono au laa.
Waziri wa elimu una chakueleza?
Tujadili