Wazazi walipishwa michango shule za msingi jijini Dar es Salaam

Naona huu uzi walimu wamekuja resi wanatoaje povu la kufa mtu hahahhaaaa

Unapoambiwa BURE maana yake nini
Acheni mambo zenu bure maana yake hakuna gharama sasa michango ya nini alafu kwanini asipate ripoti mpaka atoe hela hizo n tamaa

Ooh wazazi wazazii mlaumu waliosema bure sisi tunafyatua tu tunaleta BUREEE
Bro vifurushi vya bure kule mitandaoni huwa havilipiwi?
Eleweni lugha bure haijawahi maanisha kuwa haulipi.
Utakulazimu ununue simu yenyewe, line, vocha na charger n.k.
Lipeni jamani siasa waachieni wanasiasa
 
Sasa mabegi unapendekeza walindiww na nani?
Pili, kwenye vikao vya wazazi huwa mnajadili nini?
Yaani michango shuleni toeni tu msihoji sana hela za brashi tu hizo 'in kheri's voice'
Mlinzi wa serikali analinda nini? Na hayo mabegi yanalindwa ikiwa wanafunzi wako wapi?

Ungeuliza hivyo nafikiri ungepata maana halisi ya michango isiyo na maana!
 
Ngoswe Mimi naomba akili zetu zinyumbuke, hivi inawezekana vipi mzazi aambiwe atoe 10,000/= kwaajili ya riport ya mwaka ya mwanae anajilizaa weeeee.

Ifikie mahali tutofautishe bure na hailipiwi au haiuzwi.

Inawezekana ikawa bure kwenye kukalia dawati la shule husika ukalazimika kulipa kila additional service.
 
Kabisaaaa na n ujinga wa kiwango cha PhD,nataman Magufuli afute elimu bure,

Wazazi wamekuwa watu wa hovyo sanaaaaa,ikitokea hata dharura ya kuchangia sh 2000 wazaz hawachangii kwa sababu ya elimu bure......

Kiukweli ubora wa elimu umepungua kabisaaaaa....

Mm namshauri Magufuli wazazi wachangie michango ya shule aachane na elimu bure......

Wazazi wengine wameacha kabisa kufuatilia maendeleo ya wanao kwa sabb ya elimu n bora liende tu ili mzazi awe na uchungu lazima achangie michango ya shule
Hakuna sababu ya kuwatolea matusi wazazi na kuwaona hawajitambui, ahadi ni kitu cha kuheshimiwa sana, na bahati mbaya inarudiwa kila nafasi inapopatikana. Nashauri itangazwe tu ulikuwa ni utaratibu wa muda, ni serikali ilisitisha na si wazazi, ktk shule za serikali tulishazoea kuchangia, leo unapomwambia achangie hata sh 50/= acha 5000 lazima kama wazazi tuhoji, maana ya elimu bure inaeleweka tena vizuri tu
 
Amani iwe kwenu.
Huku wananchi wakiendelea kuaminishwa kuwa elimu ya shule primary hadi Sekondari ni bure. Bure kabisa na kwamba wananchi masikini wanafaidika.

Hali imekuwa tofauti kwa shule nyingi mkoani Dar es salaam. Wazazi wanatakiwa kwenda kuchukua ripoti za matokeo ya watoto wao huku wakiwa na kati ya shilingi 5000- 10,000 tena bila risiti kwa ajili ya ( ujenzi, ulinzi ama maendeleo ya shule) sababu hutofautiana kutegemea na shule.Wazazi wenye watoto wao wanaposhindwa kulipa hawapewi ripoti kabisa.

Watu wanahoji maana ya eelimu bure inayohubiriwa na mamlaka ni ipi? Je sio kweli kwamba serikali inauhadaa umma? Badala ya kutumia mamilion ya walipa kodi kuboresha elimu ya watoto sisi twawahonga wabunge wa upinzani na kubaki tukikenua, wabunge wanaohama ili kuunga mkono hawana budi kujibu kwanza na haya kama ni miongoni mwa juhudi wanazounga mkono au laa.

Waziri wa elimu una chakueleza?

Tujadili
Walimu watapata wapi hela Za kubrashia viatu?
 
Kabisaaaa na n ujinga wa kiwango cha PhD,nataman Magufuli afute elimu bure,

Wazazi wamekuwa watu wa hovyo sanaaaaa,ikitokea hata dharura ya kuchangia sh 2000 wazaz hawachangii kwa sababu ya elimu bure......

Kiukweli ubora wa elimu umepungua kabisaaaaa....

Mm namshauri Magufuli wazazi wachangie michango ya shule aachane na elimu bure......

Wazazi wengine wameacha kabisa kufuatilia maendeleo ya wanao kwa sabb ya elimu n bora liende tu ili mzazi awe na uchungu lazima achangie michango ya shule
Shule nyingi Za elimu bure wazazi ni kama wamewatelekeza watoto Wala hawafuatilii chochote labda itokee mchango wa elfu Moja au elfu mbili hapo ndio wanakuwa Active
 
Wewe unakurupuka kuwalaumu wazazi bure tu, sasa kabla ya mahubiri ya elimu bure waliwahi kukulilia kwamba wameshindwa kuwasomesha watoto wao? Wanakosa gani kuhoji kuhusu malipo hayo kwa kuwa wao wameaminishwa ni elimu bure? UVCCM bwana!
Kwani walimu ndio walitangaza elimu bure?
 
michango inaruhusiwa au hairuhusiw?i Raisi alishasema ni bure unaelewa maaana ya bure? Halafu mnamshambulia mtoa maada jibuni hoja zake, Au na nyie ni waalim maslahi yenu yameguswa?
Elimu inaanzia kwenye nauli unayomlipia mwanao,Uniform,Daftari nk,je ulishawahi lipiwa Kati ya hivyo nilivyoorodhesha au mzazi ndio analipa?
Nilitarajia uanze pia kudai kulipiwa nauli,chakula shule,Daftari ,sare nk maana vyote hivyo ni sehemu ya elimu.
By the way ulivyosikia elimu bure ulielewaje?
 
Wewe ndio unapiga siasa. Waambie kwanza hao wanohubiri elimu bure waache uone kama wazazi watashindwa kugharamia elimu.
Hao wanaohubiri Elimu bure hawana hata mtoto mmoja huko kwenye elimu bure.Ukianza kuwasubiri hao utaumia mwenye
 
Ungetaja jina la shule INGEPENDEZA zaidi. Ila ninachojua kuwa katika baadhi ya shule wazazi wanakubaliana kulipia michango ya ulinzi na hata ujenzi wa mabweni kwani fedha za kugharamia matumizi hayo hazitolewi na serikali

Kwa mara ya kwanza Lizaboni unakubali kuwa "Tunapigwa changa la macho!" Dah! Ya leo kali. Baadhi ya shule!! Kwani hizo "Baadhi ya shule" ni za Msumbiji au Tz iliyojiapisha kuwa, hakuna michango wala changizo tena mashuleni?? Unamkumbuka yule mwalim aliyetumbuliwa kwa kuomba mchango huu?? Tutamfanyaje au ndo tushamsahau?? Ndumila kuwili at work.
 
Labda ni jinsi alivyo uwasilisha huu uzi ndio umeleta utata kidogo.

Ukweli ni kwamba shule nyingi jinsi ya ukusanyaji hiyo michango inawachanganya wazazi.
Mfano Shule ya msingi Uhuru wasichana, kuna mlinzi ambaye serikali inamlipa. Lakini wazazi wanalazimishwa Kila mwezi kulipa pesa ya mlinzi. Mtoto asipopeleka anapigwa viboko. Ukiuliza kazi ya huyo mlinzi wa pili ni ipi wanadai analinda mabegi ya anafunzi!
Ukienda kuuliza sababu ya kumpiga mtoto viboko mwalimu atakupeleka darasani na kuwauliza wanafunzi mbele yako kuwa.... Eti fulani nimempiga viboko?
Wanafunzi: Hapana!
Wamewafundisha watoto kuwa akija mtu hapa akisema tunawachapa kataeni, Ole wake atakaye sema. Huo ni mfano tu wa baadhi ya michango ambayo haina kichwa wala miguu.
Mkuu hiyo shule ina karaha Hamisha mwanao fasta mpekeke Tusiime hawana Longolongo wale
 
Ungetaja jina la shule INGEPENDEZA zaidi. Ila ninachojua kuwa katika baadhi ya shule wazazi wanakubaliana kulipia michango ya ulinzi na hata ujenzi wa mabweni kwani fedha za kugharamia matumizi hayo hazitolewi na serikali
Mkuu padre na msela muongo silaa kaula we bado tu mkuu.
 
Naona huu uzi walimu wamekuja resi wanatoaje povu la kufa mtu hahahhaaaa

Unapoambiwa BURE maana yake nini
Acheni mambo zenu bure maana yake hakuna gharama sasa michango ya nini alafu kwanini asipate ripoti mpaka atoe hela hizo n tamaa

Ooh wazazi wazazii mlaumu waliosema bure sisi tunafyatua tu tunaleta BUREEE
Kwa hiyo mwanao ataenda shule Bila sare,Nauli Wala daftari? Elimu bure
 
Watanzania Kazi tunayo,,watu walivyoambiwa elimu ni bure basi hawataki kuchangia chochote khaa. Halafu mkumbuke hizo ni Shule zenu,mimi wabangu wako kulee
 
Katika watu ambao thinking capacity yao ni sifuri ni huyu aliye leta huu uzi, yaani unazaa ili watu wengi wakulelee? Mhs Rais ameonesha pa kuanzia sio kila kitu yeye fikili tena tafadhali
Huu uhandishi wako mƙuu sonkuno unaniacha hoi
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom