Wazazi walio na mawazo ya kuwekeza kwa watoto wao

miss_mbeya

JF-Expert Member
Mar 24, 2015
1,022
2,000
Wapendwa habarini za kazi, nipende kwenda kwenye hoja yangu, wazazi wengi huwa wanasomesha watoto kama ni sehemu ya uwekezaji wao ili baadaye mtoto akipata kazi amtegemee kwa kila kitu.

Binafsi hii hali inanikera sana, tukiwa kama wazazi tusijefanya hivo ni mawazo finyu kabisa, mzazi ni wajibu kumsomesha mtoto lakini usifuje mali zako ikitegemea watoto baadaye wakubebe.
 

Mgirik

JF-Expert Member
Apr 27, 2013
13,113
2,000
Ww ulisikia wapi kuwa kila mzazi anayemsomesha mwanaye anategemea misaada kwa %100 baadae??

Kumsomesha mtoto ni wajibu wa mzazi.. Mtoto kupata elimu na malazi na malezi bora ni haki yake..

Labda ww ndio umetafsiri vibaya.
 

TheChoji

JF-Expert Member
Apr 14, 2009
3,496
2,000
Elimu imeshageuzwa biashara sasa ivi na ni fasheni kumpeleka mtoto shule za ghali kwahiyo we somesha tu mkuu hakuna namna.
 

black sniper

JF-Expert Member
Dec 10, 2013
18,940
2,000
Hayo ni mawazo yako tu maana hakuna mzazi anaewasomesha watoto kwa kusubiri baadae atasaidiwa
Hakuna mwenye kujua ataishi mda gani hilo ni moja na la pili mzazi anaeweza kuwalipia kila kitu kwa uwezo huo itakuwaje awe na wazo la kusubiri kubebwa?

Watoto tunawaandaa kwa maisha yao ya baadae kama wakiwa na maisha yao
Sasa niwategee kwa vipi wakati nina maisha yangu na kuyamudu?
 

miss_mbeya

JF-Expert Member
Mar 24, 2015
1,022
2,000
Ww ulisikia wapi kuwa kila mzazi anayemsomesha mwanaye anategemea misaada kwa %100 baadae??

Kumsomesha mtoto ni wajibu wa mzazi.. Mtoto kupata elimu na malazi na malezi bora ni haki yake..

Labda ww ndio umetafsiri vibaya.
Hii mkuu nimeona kwa wazazi baadhi hata mimi pia inanitokea ,mzazi alikuwa na pesa akatusomesha na alikuwa ana matanuzi sana bila kuwekeza ,alivozeeka anatusumbua kuwa nilikuwa nawekeza kwenu wakati mnasoma kwasasa ni wajibu wenu kutulea kwa kweli ilifika hatua alitupigia hesabu kila mtoto awe anatuma laki na nusu kila mwisho wa mwezi kwa ajili ya matumizi yake
 

Azial

JF-Expert Member
Dec 12, 2017
476
1,000
Mwezi huu mambo yangu yalienda tofauti kidogo nikachelewa kumtumia mama hela! Niliumia sana
 

souljar

JF-Expert Member
Feb 16, 2021
785
1,000
Hili jambo ndio linalowamaliza wazee wakichagga kule kwao rate za wazee kufariki vijijini zanaongezeka Xmas na New year yote sababu ya vijana wao wasipo enda kuwatembelea au wameenda na hali nitete wakati jirani yake mwanae ameenda na V8 mpya, kwa kifupi nachojaribu kusema wazee wa kichagga wanategemea mengi kwa watoto wao zaidi kuliko kabila jingine.

MTAZAMO TU...
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom