Wazazi waliniambia nisiolewe naye lakini sikuwasikiliza, sasa najuta sana

annampole

Member
Jun 8, 2016
50
125
Mimi ni mdada Nina miaka 27 niliolewa nikiwa na miaka 25 huyu mume wangu tulikutana kwa muda mfupi sikumjua sana wazazi walikataa wakaniambia atanisumbua lakin mimi nililazimisha mpaka tukafunga ndoa kanisani niliyoyaona nilikimbia mwenyewe sikuzaa Naye nashukuru wazazi wamenisamehe wamenipokea.

Shida inayonisumbua ni kutojikubali ni mwaka na nusu sasa siwezi kutoka nje wala kwenda sehemu yoyote naona aibu nahisi majirani ndugu wananicheka kuongea na marafiki naogopa nahisi wataniuliza ndoa yangu inaendeleaje.

Najuta sanaa ningewasikiliza wazazi wangu haya yasingenikuta mpaka nimekonda kwa mawazo jamani mliowahi kuachika mliikabili vipi jamii inayowazunguka
 
Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
45,810
2,000
Kufanya kosa si kosa kosa ni kurudia kosa, kubali kuwa wewe si wa kwanza kulikoroga kimaisha na kuwa kupitia mkorogo huo utampata wewe mpya, mwenye nguvu. Hao majirani watasema watachoka, itakuja issue nyingine watakoyoiangalia yakwako wakishaizoea. Cha muhimu ni kujenga upya maisha yako.
 
Nifah

JF-Expert Member
Feb 12, 2014
26,755
2,000
Dah haya matatizo yamezidi,natamani ningekuwa na taasisi au ningekuwepo kwenye taasisi/dawati la wanawake jinsia na watoto niweze kuwashauri wanawake mwenzangu jinsi ya kukabiliana na mambo kama haya.

Maana kama wanawake wenye access na mitandao ya kijamii kama hivi ni wachache ila malalamiko ni mengi vipi kwa wanawake walio wengi huko katika jamii zetu wasioweza kupaza sauti za vilio/maumivu yao kama hivi?

Anyways, ngoja nikuitie wanawake wa shoka wakushauri,mimi nitakushauri baadae au kukutafuta kivyangu
BADILI TABIA Heaven Sent geniveros charty FaizaFoxy LadyAJ Sakayo house girl n.k
 
Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
86,641
2,000
Mimi ni mdada Nina miaka 27 niliolewa nikiwa na miaka 25 huyu mume wangu tulikutana kwa muda mfupi sikumjua sana wazazi walikataa wakaniambia atanisumbua lakin mimi nililazimisha mpaka tukafunga ndoa kanisani niliyoyaona nilikimbia mwenyewe sikuzaa Naye nashukuru wazazi wamenisamehe wamenipokea shida inayonisumbua ni kutojikubali ni mwaka na nusu sasa siwezi kutoka nje wala kwenda sehemu yoyote naona aibu nahisi majirani ndugu wananicheka kuongea na marafiki naogopa nahisi wataniuliza ndoa yangu inaendeleaje najuta sanaa ningewasikiliza wazazi wangu haya yasingenikuta mpaka nimekonda kwa mawazo jamani mliowahi kuachika mliikabili vipi jamii inayowazunguka
Wewe umeachika au we ndo umemwacha?

Halafu unaona aibu ya nini?

Kwani kumwacha ndo imekuwa mwisho wa dunia?

Come on now....just say fcuk it and keep it movin'.

Yaani jambo dogo tu kama hilo linakufanya ushindwe kuishi kwa raha?

Si wengine sijui tumeumbwaje tu maana hakuna mtu, kitu, wala jambo la kunikosesha raha aiseee.

Hahahaa wakati mwingine hadi huwa najishangaa mwenyewe.
 
socket

JF-Expert Member
Nov 21, 2014
203
250
Mimi ni mdada Nina miaka 27 niliolewa nikiwa na miaka 25 huyu mume wangu tulikutana kwa muda mfupi sikumjua sana wazazi walikataa wakaniambia atanisumbua lakin mimi nililazimisha mpaka tukafunga ndoa kanisani niliyoyaona nilikimbia mwenyewe sikuzaa Naye nashukuru wazazi wamenisamehe wamenipokea shida inayonisumbua ni kutojikubali ni mwaka na nusu sasa siwezi kutoka nje wala kwenda sehemu yoyote naona aibu nahisi majirani ndugu wananicheka kuongea na marafiki naogopa nahisi wataniuliza ndoa yangu inaendeleaje najuta sanaa ningewasikiliza wazazi wangu haya yasingenikuta mpaka nimekonda kwa mawazo jamani mliowahi kuachika mliikabili vipi jamii inayowazunguka
Unaadhiri mtazamo wako sana sababu unakaa bila kazi yoyote so nakushauri tafuta rafiki yoyote wa mbali na ukaanzishe biashara yoyote unayoweza kuimudu.
sijajua kwa upande wa kuanzisha familia nyingine itakuja kuwaje maana kama katika mda mfupi jamaa aliamua kukuona pengine na mahari mlimpiga kubwa akija sikia unaishi na mtu lazima alete shida
 
Kakole

JF-Expert Member
Jul 29, 2015
2,101
2,000
Kwani wewe umeachika au umemuacha mwenyewe? kwani alikuwa na mapungufu gani yasiovumilika.
 
Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
86,641
2,000
Kwani wewe umeachika au umemuacha mwenyewe? kwani alikuwa na mapungufu gani yasiovumilika.
Kwa mujibu wa alivyoelezea yeye ndo kamuacha jamaa.

Ila kwa jinsi jamii ilivyo stigmatize suala zima, nadhani ndo maana yeye anaishia kujiona kama kaachika.

That is some fuckery right there.

Ila pia inawezekana akawa na matatizo mengine kama ya kutokujiamini na/au low self esteem....
 
mattargsm

JF-Expert Member
Apr 12, 2016
391
250
hayo ni kawaida wa usijitie sad thinking nyingi waambie hivi majirani sitofanya Tena kosa kama hili lá kumuona mtu tu alafu nikavamia
 
Kakole

JF-Expert Member
Jul 29, 2015
2,101
2,000
Kwa mujibu wa alivyoelezea yeye ndo kamuacha jamaa.

Ila kwa jinsi jamii ilivyo stigmatize suala zima, yeye ndo anaishia kujiona kama kaachika.

That is some fuckery right there.
Hiyo ndio shida ya mabinti wa siku hiz sio wavumilivu, badala avumilie anakimbilia hom tena wakati mume kamchagua mwenyewe.
 
barafuyamoto

JF-Expert Member
Jul 26, 2014
29,253
2,000
Mshukuru Mungu ishu yako ni reversible, kuna wengine wanapingana na wazazi wao na kufanya maamuzi yenye irreversible and eternal scar!! Imagine ungekuwa umezaa nae au imagine angekuwa amekupa virusi ingekuaje!
Jipongeze kwa kufungua akili mapema, 27 bado sana!!
 
Asprin

JF-Expert Member
Mar 8, 2008
61,748
2,000
Mbona huna moyo wa uvumilivu ata honey moon ujamaliza miaka 2 tu kasoro umekimbia nyumba yako ? Tuambie kilichokukimbiza kwenye ndoa na si kutafuta huruma huku
Nadhani alikutana na dushe size kubwa kama nanga ya meli Titanic...
 
Kiboko.

JF-Expert Member
Jul 31, 2013
2,834
2,000
Mimi ni mdada Nina miaka 27 niliolewa nikiwa na miaka 25 huyu mume wangu tulikutana kwa muda mfupi sikumjua sana wazazi walikataa wakaniambia atanisumbua lakin mimi nililazimisha mpaka tukafunga ndoa kanisani niliyoyaona nilikimbia mwenyewe sikuzaa Naye nashukuru wazazi wamenisamehe wamenipokea.

Shida inayonisumbua ni kutojikubali ni mwaka na nusu sasa siwezi kutoka nje wala kwenda sehemu yoyote naona aibu nahisi majirani ndugu wananicheka kuongea na marafiki naogopa nahisi wataniuliza ndoa yangu inaendeleaje.

Najuta sanaa ningewasikiliza wazazi wangu haya yasingenikuta mpaka nimekonda kwa mawazo jamani mliowahi kuachika mliikabili vipi jamii inayowazunguka
Tatzo lako ww n tasa afu unataka rusha lawama kwa mwanaume...
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom