Wazazi/Walezi/Wanafunzi, zingatia hili unapochagua/confirm chuo cha kwenda kusoma

analysti

JF-Expert Member
Aug 24, 2009
729
612
Wanabodi poleni na majukumu.

Nafahamu kipindi hiki ni kipindi ambacho udahili ktk vyuo mbali mbali unafanyika. Kutokana na mchakato wa udahili kuwa tofauti mwaka huu, kumekuwa na matukio ya mtu kudahiliwa zaidi ya chuo kimoja na kutakiwa kuthibitisha kukubali admission ya chuo atakachopenda kwenda kusoma na hivyo kuondolewa ktk vyuo vingine alivyochaguliwa.

Hivyo basi, ningependa kuwatahadhalisha kuhakikisha kuwa uchaguzi unaoufanya juu ya chuo fulani dhidi ya chuo fulani uwe ni uchaguzi uliozingatia masuala muhimu yatakayokuathiri ktk kipindi cha masomo na baada ya kumaliza masomo yako ktk chuo husika.

Moja ya jambo muhimu sana ambalo ni muhimu mwanafunzi mtarajiwa akalifahamu vyema ni ADA (TUITION FEE).

Ni vyema mwanafunzi mtarajiwa akafanya utafiti juu ya tution fees za vyuo atakavyochaguliwa kwa kuwa hili linaweza kuwa na athari kwake katika kipindi ambacho atakuwa anasoma na pia baada ya kumaliza masomo yake.

Awali kabisa, Ifahamike kuwa Bodi ya mikopo ya elimu ya Juu inakiwango cha juu (Maximum amount) cha fedha ambacho wanaweza kukitoa kwa mwanafunzi kama mkopo wa tuition fee (3.1 Mil). Hivyo basi, ikitokea chuo kinatoza tuition fee zaidi ya kiwango cha ukomo kinachoweza kutolewa na HESLB mwanafunzi atawajibika kujazia kiasi cha Tuition fee kinachopelea, mara nyingi hali hii hutokea kwa wanafunzi wanaosoma taaluma za AFYA ambapo mwanafunzi anaweza kutakiwa kuongezea kiwango ambacho kinaweza kuzidi hata Mil 3 kwa mwaka.

Jambo hili kutofahamika miongoni mwa applicants kumepelekea baadhi ya wanafunzi kushindwa kumudu gharama hizo na kujikuta wakisitisha masomo yao. Unaweza kuzijua hizi gharama kwa kupitia kwenye tovuti za vyuo husika.

Lakini pia, ifahamike kuwa haya malipo yanayotolewa na bodi ya mikopo ni mkopo ambao utatakiwa kuulipa mara tuu baada ya kumaliza masomo yako, hivyo basi kwa kuwa ni mkopo ni vyema kuhakikisha kusoma chuo ambacho kinagharama nafuu iwezekanavyo ili mwisho wa siku kiwango cha malipo utakachotakiwa kuja kukifanya kiwe ni kidogo, kwa kiasi kikubwa vyuo vyenye gharama nafuu kabisa ni vyuo vya umma (Public Universities).

Hii ni athari utakayoipata baada ya kumaliza masomo yako. Na hili halina utani, wengi humu ni wahanga wa 15% kama makato ya HESLB.

Wasalaam.
 
hawawezi wanafunzi wote kwenda public universities mkuu, hata hivyo elimu ya chuo kikuu ni gharama kwo kwa namna yoyote kikubwa ni kuwaza kupata elimu, gharama kuwa kubwa haiepukiki.
 
hawawezi wanafunzi wote kwenda public universities mkuu, hata hivyo elimu ya chuo kikuu ni gharama kwo kwa namna yoyote kikubwa ni kuwaza kupata elimu, gharama kuwa kubwa haiepukiki.

Nafikiri hukunielewa, post yangu imelenga wale waliochaguliwa zaidi ya chuo kimoja na kujikuta wanatakiwa kuchagua chuo kimojawapo.
 
Nafikiri hukunielewa, post yangu imelenga wale waliochaguliwa zaidi ya chuo kimoja na kujikuta wanatakiwa kuchagua chuo kimojawapo.
Mkuu sasa kama mtu kozi unayoipenda ndiyo umechaguliwa chuo chenye tuition fee kubwa, na wakati huo chuo kingine umechaguliwa kozi ambayo kwako ni second priority na ada yake ni ndogo, unafikiri hapo mwanafunzi achague kwenye tuition fee ndogo ili baadae ailipe kiurahisi? Hata hivyo pia priority ya kupata mkopo inategemea na kozi.
 
Ni ushauri mzuri tu, bado janga linaachwa kwa mzazi na mwanafunzi mwenyewe
 
Mkuu sasa kama mtu kozi unayoipenda ndiyo umechaguliwa chuo chenye tuition fee kubwa, na wakati huo chuo kingine umechaguliwa kozi ambayo kwako ni second priority na ada yake ni ndogo, unafikiri hapo mwanafunzi achague kwenye tuition fee ndogo ili baadae ailipe kiurahisi? Hata hivyo pia priority ya kupata mkopo inategemea na kozi.

Ukifanya hivyo ukiwa unajua kinachoambatana na uchaguzi wako hakuna shida. Ina maana gani ukaenda kozi unayoipenda halafu baada ya mwaka mmoja uka ahirisha masomo kwa kushindwa kujilipia??. Nia ya huu uzi wangu, ni kuwafungua watu macho, ili anapofanya uchaguzi awe anajua maana ya huo uchaguzi wake na awe ameshajiandaa kwa kinachofuata. Hakuna shida yoyote kujilipia ada kama uwezo wa kufanya hivyo upo, tatizo linakuja pale ambapo wazazi wanaomba Mungu upate nafasi ya chuo ili ukishapata mkopo basi uweze kuwatumia chochote ili waweze kujikimu kimaisha.
 
mkuu naomba unisaidie apo nina mdogo wango alipata 1st round saut lkn ajakipenda ivo akaomba tena second round amepata udom uvi hii inakua imekaaje mkuu.
 
Back
Top Bottom