naina19
JF-Expert Member
- Oct 8, 2019
- 294
- 510
Habari za leo wakuu
Natumaini ni furaha ya kila mzazi au mlezi mwenye nia njema kumuona mtoto anakua katika kile anachokiamini.
Kwa nchi nyingi za kiafrika na Tanzania ikiwemo kumekuwa na desturi, mazoea au tabia ya kuwekeza mafunzo mengi, ulinzi, ukaribu kwa mtoto wa kike zaidi ya mtoto wa kiume.
Kwa miaka mingi sasa pia kumekuwa na mashirika pamoja na uhamasishaji mkubwa katika kumsaidia mtoto wa kike na wanawake huku mtoto wa kiume akiachwa akue akijifunza kwa jamii inayomzunguka tu bila kujali kama anapata kinachotakiwa na kwa usahihi.
Wazazi tunachokifanya kwa mabinti zetu sio kibaya ila tujue tunatengeneza gap kubwa kati yao na vijana wetu wa kiume. Tunakuwa na idadi kubwa ya mabinti wanaoelewa majukumu yao kijamii na vijana wa kiume wasioelewa majukumu yao japo yale ya asili.
Nadhani huu ni muda sahihi kwetu wazazi na jamii kwa ujumla ikiwepo taasisi mbalimbali (haswa zile za dini na elimu) kuliangalia hili upya kwani kwa kufanya hivyo inaweza kusaidia kupunguza matatizo mengi sana yanayoweza kutokea baadae haswa pale vijana wanapokuja kuingia kwenye majukumu ya ndoa.