Wazazi wa aliyekua Ex wangu, wamenipa sehemu ya mahari ya binti yao kama kifuta jasho

Applicant

JF-Expert Member
Feb 12, 2020
1,962
1,746
Back in d' dayz!

Nilikua na mtoto mzuri, kitu black beauty mwenye asili ya mbeya, kiufupi ni kwamba nilimsaidia sana, nilikua naplay part kama mzazi wake, ada ya chuo, mahitaji yote, na alipomalza chuo nilimpa mtaji wa shilingi milioni 5 akaanza biashara na yote hayo wazazi wake walikua wanajua kua mimi ni mchumba wa binti yao na ndie ninaemgharamia.

Habari mbaya ni kwamba mtaji niliompa, aliukuza na akafikia stage ya kwenda kuchukua mzigo mwenyewe China, hapo ndipo akaanza majivuno na kuniona mimi si lolote, ilikua mwaka jana mwezi wa 12, akanitamkia rasmi kua hanitaki na amepata mume wa kichina na wanapendana sana, akaenda mbali zaidi na kuadai kua kama kuna kitu namdai aseme shingapi ili anilipe!! Aiseeee!!

Ila kwakua sikua na njaa kivile, mimi mwenyewe si haba chenchi zipo kiaina, nikampotezea nikamtakia kila la heri, nakumbuka wazazi wake waliumia sana na maamuzi ya binti yao, kwani walikua wameshanikubali kwani mimi ndio nilikua kama namlea binti yao, na walishaniambia akimalza chuo nimuoe binti yao, ila ikawa sio bahati yangu, nikaamua niachane nae.

Toka hicho kipindi wazazi wake wamekua wakinijulia hali kwani walikua wananipenda sana, week iliopita nilishangaa wananiita nyumbani kwao, nilipoenda wakaniambia kua binti yao anaelekea kuolewa na yule mchina na tayari yule mchina katoa mahari! Basi mimi nikawaambia ni jambo la kheeeriii.

Nikashangazwa na yule mzee alipopewa kimfuko Cha kaki na mke wake akaambiwa anikabidhi kama kifuta jasho, kwa yale niliomtendea binti yao! Nikawauliza " Bahasha hii ina nini!?" Ndio yule mzee mwaipopo akaniambia kua kuna shilingi milioni 8 pale kwenye mfuko.

Nikashangaa sana! Nikawauliza kwanini wanafanya yote haya?! Mzee yule pamoja na mke wake wakaniambia ni kama fadhila tuu kwa jinsi nilivyopambana kumpigania binti yao katika maisha yake, pia wakaongeza kua bila mimi hata mtoto wao asingekutana na huyo mchina,

alinishangaza sana, aliposema kua yule mchina alitoa mahari ya shilingi milioni 45 za kitanzania kama mahari! Nilishangaa sana, ikabidi nichukue tuu mzigo nikawashukuru na kuwaaga, ila walinisihi kua TUENDELEE KUWASILIANA.
 
chai.jpg
 
Back
Top Bottom