Wazazi Ujerumani Wapigania Kumpa Jina la 'Jihad' Mtoto wao | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wazazi Ujerumani Wapigania Kumpa Jina la 'Jihad' Mtoto wao

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by MziziMkavu, Sep 4, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Sep 4, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Thursday, September 03, 2009 12:36 AM
  Wazazi wa mtoto mchanga aliyezaliwa hivi karibuni nchini Ujerumani ilibidi waende mpaka mahakamani kupigania kupata ruhsa ya kumpa jina la 'Jihad' mtoto wao mchanga aliyezaliwa hivi karibuni. Awali maofisa wa Ujerumani wanaosimamia rekodi za watoto wanaozaliwa walikataa kumsajili mtoto huyo kwa jina la "Jihad" (vita vitakatifu) wakisema kwamba jina hilo ni baya kwa mtoto huyo kwani neno jihad linahusishwa zaidi na magaidi.

  Mahakama ya mji wa Berlin ilitoa ruhusa kwa wazazi wa mtoto huyo kumpa mtoto wao jina wanalotaka la "Djehad" ambalo linamaana sawa na "Jihad" likimaanisha vita vitakatifu vya kiislamu.

  Mahakama hiyo ilivunja maamuzi ya mahakama ndogo mbili za chini zilizopinga jina hilo.

  Mahakama hiyo ilisema kwamba sababu ya kuliruhusu jina hilo ni kuwa jina hilo linatumika kama jina la kiume katika nchi zinazozungumza kiarabu.

  Mahakama hiyo pia ilisema kwamba kwa kuangalia kuwa dhumuni la jina hilo ni kuitangaza imani ya kiislamu, imewapa ruhsa wazazi wa mtoto huyo kumwita mtoto wao "Jihad" ingawa jina hilo limekuwa likihusishwa na magaidi sana sana baada ya mashambulizi ya septemba 11 mwaka 2001.

  Sheria za Ujerumani zinazuia wazazi kuwapa watoto wao majina ambayo yanaweza kutafsiriwa kama yenye madhara kwao.
  http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=2977798&&Cat=2
   
Loading...