Wazazi: Tuwafundishe watoto wetu mila na desturi njema za wazee

Mjamaa1

JF-Expert Member
Apr 9, 2013
7,267
5,422
Salamu, Heri kwa siku kuu ya Krisimasi.
Ndugu zangu ,leo tunaadhimisha
Dominika ya Familia Takatifu.
Katika muktadha huo, nimependa tujadiliane juu ya malezi ya watoto wetu hasa kuwafundisha mila na desturi njema za wazee wetu.
Wazazi tunawajibu huo kwasababu wengi wetu tumeacha kuwafundisha watoto wetu mila na desturi zetu njema, mfano Lugha, mapokeo ya kimaadili nk.
Kinyume chake tunawaacha wajifunze wenyewe au kufundishwa na wajakazi wetu, walimu au tunawandisha utamaduni wa kigeni tu, (Formal Education)
mwisho wa siku tunapoteza tamaduni na mila zetu nzuri.
Tutakuwa taifa la aina gani?
Copiest?
Chetu ni kipi?

Tupate Mfano Kutoka kwa Wafipa.

Wafipa wa zamani walikua na utamaduni wa kutandika shuka nyeupe kwenye kitanda cha maharusi, heshima ya wazazi wa binti iliimarika pale shuka ile litakapokutwa na damudamu asubuhi..., heshima ya binti na ya wazazi ilipotea pale shuka litakapokutwa halina alama yoyote ya damu.
Hii iliwafanya wasichana wengi wajitunze na kujilinda maana ndipo ilipokuwa heshima yao na ya wazazi wao.
Hali ya sasa vibinti vya shule ya msingi vipo kwenye mahusiano na vimeshafanya ngono bila wazazi kujua hilo.
Nawatakia Heri na baraka kwa mwaka mpya 2022.
Karibuni

1 Wamakabayo 6:59
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom