Wazazi tuwafuatilie watoto wetu Mashuleni, Majumbani, Makanisani na hata wanapocheza

Kalpana

JF-Expert Member
Jun 16, 2017
26,833
50,015
Watoto wanapitia mambo mengi ya unyanyaswaji mashuleni, kupigwa na walimu bila sababu maalum kisa tu mwalimu hampendi mtoto, anapitia changamoto za watoto wenzie wakorofi wana mbully mara zingine au watoto watukutu kuwafanyia vitendo vibaya.

Makanisani napo si mahali salama kabisa. Tusiamini sana hizi sunday schools sijui mafundisho au zile watoto wa kiume wanapokutana kwa ajili ya kujiandaa na misa za kesho yake hasa catholic tufatilie huko.

Kwenye michezo yao tujithidi kujua watoto wanacheza na nani,je ni watoto mnaowafahamu? Je ni wenye tabia njema? Dunia kwa sas sio rafiki kwa watoto. Tujitahidi kuwa marafiki na watoto watuelezee changamoto zao. Unakuta mtoto anakosa raha akisikia shule au hataki kwenda kanisani unamlazimisha na kumchapa kabisa. Kama mtoto hataki kitu fulani au kwenda mahali tuchunguze sababu.

Wazazi tushirikishane visa vilivyowafanya mpaka mkaanza kufuatilia watoto wenu na mlipogundua unyanyasaji au matendo yoyote mabaya mlichukua hatua gani kumsaidia mtoto.

Nimekumbuka leo mtoto wangu alikua ana rafiki yake wkt yupo pre unit akawa anasema fulani anapenda kunivuta kidudu changu. Mimi kwa kweli sikupenda yani aliponiambia hivyo kama mara mbili ya tatu nikaenda shule nikaonana na mkuu wa shule akaitwa mwalimu wa darasa na mtoto husika akaulizwa akasema ndio akaulizwa kwanini akawa hana jibu akatishiwa pale na wakamwambia watamchapa na kumfukuza shule akirudia akaitwa na mzazi wake next day akaambiwa tabia ya mwanae. Aliacha ile tabia na siku hazikupita nyingi akahamishwa shule. So nikashukuru mtoto aliliripoti tukio kwahyo siku hizi niko makini sana kuwauliza kuna lolote shule? Kuna mtu anaonewa? Kuna aliepigwa?

Kisa kingine ni mtoto wa dada yangu na yeye kuna siku alipigwa akarudi amevimba mkono aisee kuulizwa akasema ticha fulani kanichapa. Lakini alishalalamika kuwa kuna ticha anatuchapa sana mama yake alipoenda shule ni kweli alikutana na kesi hizo kwa mwalimu mkuu na ndo tabia ya mwalimu so walimkanya naona siku hizi hali haijajirudia.
 
Umeongea point kubwa na muhimu sana hakika wewe ni mzazi bora. Hiyo ndiyo njia niifanyayo mimi pia. Hapa wengine watapita kimya kimya kwasababu hawana muda wa kuwafuatilia watoto wao hata wakirudi wamepigwa na walimu wakavimba uso mzazi ndo wa kwanza kumwambia mtoto "wewe ni mtundu ndo maana umepigwa"

Sasa kama mzazi anakuwa mkatili kwa maanae unadhani mtoto hata akifanyiwa jambo baya atamweleza mzazi? Lahasha.

Niliwahi kuwakuta walimu kama watatu wanawaadhibu wanafunzi pasipo utaratibu nikaenda kwa mwalkmu mkuu kumweleza kama anajua watoto wanaadhibiwa hovyo akashangaa akaniuliza wapi. Nikamwambia twende pale nje akawakuta walimu wanawadhibu watoto akawaita ofisini akawaandikisha barua za maelezo hadi leo nikipita mle hakuna ujinga huo na huwa nawauliza wanafunzi mara kwa mara.

Kwakuwa kitaaluma mimi ni mwanasheria nipo tayari kumshitaki mwalimu yeyote asiyefuata mwongozo/waraka wa adhabu kwa wanafunzi ambapo anayepaswa kumwadhibu mwanafunzi ni mkuu wa shule tu ama ampe idhini ya maandishi mwalimu mwingine kutoa adhabu hiyo tena kwa idadi ya viboko visivyozidi vitatu kwa kosa kubwa.
 
Maana mtetezi wa mtoto ni mtu mzkma kwakuwa mtoto hawezi kujitetea mwenyewe bali anakuwa inferiority pale anapokutana na adhabu za walimu wasiojua maadili yao ama wasiofuata utaratibu wa kisheria wa adhabu.

Shida walimu wengi ni failure sasa hawajui maana ya muongozo/waraka wa elimu juu ya adhabu. Pia hata codes of ethics za ualimu hawazijui.

Siku nikikuta mwalimu anatoa adhabu kinyjme na utaratibu ni moja kwa moja na deal nae kisheria kukomesha uonevu kwa watoto wasio na hatia.
 
Me nilifanyiwa ukatili mkubwa Sana baada ya kuanza halakati za kudai haki Elimu, kitendo kilichopelekea Headmistress kunihisi ni watu wa usalama na kuanza kuniona Adui mkubwa,

Me nimtu wakupuuzia vitu hasa kama sijatenda Mimi sasa kukaa kwangu kimya Kumbe wenzangu wananiwinda ili kunifukuzisha Shule ili nyoyo zao zifurahi, mbaya zaidi Kuna baba mmoja alienda kwa Afsa Elimu kumueleza madhaifu ya Mwalimu mkuu basi walimu wakajua moja kwa moja ni Mimi

Mambo yakawa moto walimu woote wakawa hawataki hata kuniona Darasa nililokuwepo wakalisusa ikawa tunakaa Hadi week bila kusoma kisa Mimi kuwa mnoko jamani wakati sijui chochote wala sihusiki na Chochote

Niliishi maisha Magumu Sana pale shule Soo hayo ndiyo yalinikuta nikiwa shule ingawa yapo mengi ila nimejaribu kusamulize.
 
Kuna jamaa alimpiga mwalimu na kichwa kwenye paji la uso na kupelekea yule mwalimu kupasuka
Mwalimu hakukubari akampeleka yule mwanafunzi police akaona haitoshi hasira akaziamishia kwa wanafunzi woote

Jamaa alianza kutafuta visababu vya kijinga mara nata notes za vipindi vyote kama huna anakularua kama anaua Nyoka ili kupoza machungu

Yule jamaa aliempeleka police naye alifukuzwa Shule yaani haya Maisha usione mtu kakosa Elimu unamlaumu watu wanapitia masahibu mengi
 
Umeongea point kubwa na muhimu sana hakika wewe ni mzazi bora. Hiyo ndiyo njia niifanyayo mimi pia. Hapa wengine watapita kimya kimya kwasababu hawana muda wa kuwafuatilia watoto wao hata wakirudi wamepigwa na walimu wakavimba uso mzazi ndo wa kwanza kumwambia mtoto "wewe ni mtundu ndo maana umepigwa"

Sasa kama mzazi anakuwa mkatili kwa maanae unadhani mtoto hata akifanyiwa jambo baya atamweleza mzazi? Lahasha.

Niliwahi kuwakuta walimu kama watatu wanawaadhibu wanafunzi pasipo utaratibu nikaenda kwa mwalkmu mkuu kumweleza kama anajua watoto wanaadhibiwa hovyo akashangaa akaniuliza wapi. Nikamwambia twende pale nje akawakuta walimu wanawadhibu watoto akawaita ofisini akawaandikisha barua za maelezo hadi leo nikipita mle hakuna ujinga huo na huwa nawauliza wanafunzi mara kwa mara.

Kwakuwa kitaaluma mimi ni mwanasheria nipo tayari kumshitaki mwalimu yeyote asiyefuata mwongozo/waraka wa adhabu kwa wanafunzi ambapo anayepaswa kumwadhibu mwanafunzi ni mkuu wa shule tu ama ampe idhini ya maandishi mwalimu mwingine kutoa adhabu hiyo tena kwa idadi ya viboko visivyozidi vitatu kwa kosa kubwa.
Safi sana mkuu. Kuna kisa kimetokea Nigeria amepost Mercy Johnson kimeniuma ndo nikapata muda wa kuandika hii kitu. Yani mashuleni watt wanafanyiwa ndivyo sivyo na huyo mtoto amekufa kwa maumivu makubwaa alipigwa na wenzie kisa amekataa kujiunga na kikundi chao. You know what? Walimu wameficha hiyo kitu wanasema ameumia wakati anacheza mpira. Wakati huo huo baadhi ya wazazi wa watoto washukiwa waliofanya hivyo wamehamishwa shule fasta wamepelekwa nje ya nchi.
 
Kuna jamaa alimpiga mwalimu na kichwa kwenye paji la uso na kupelekea yule mwalimu kupasuka
Mwalimu hakukubari akampeleka yule mwanafunzi police akaona haitoshi hasira akaziamishia kwa wanafunzi woote

Jamaa alianza kutafuta visababu vya kijinga mara nata notes za vipindi vyote kama huna anakularua kama anaua Nyoka ili kupoza machungu

Yule jamaa aliempeleka police naye alifukuzwa Shule yaani haya Maisha usione mtu kakosa Elimu unamlaumu watu wanapitia masahibu mengi
For sure. Ila hapa ni malezi sasa ya pande zote wazazi tufanye jitihada kulea wtt wetu vzr nyumbani na walimu pia watusaidie huko shule
 
Me nilifanyiwa ukatili mkubwa Sana baada ya kuanza halakati za kudai haki Elimu, kitendo kilichopelekea Headmistress kunihisi ni watu wa usalama na kuanza kuniona Adui mkubwa,

Me nimtu wakupuuzia vitu hasa kama sijatenda Mimi sasa kukaa kwangu kimya Kumbe wenzangu wananiwinda ili kunifukuzisha Shule ili nyoyo zao zifurahi, mbaya zaidi Kuna baba mmoja alienda kwa Afsa Elimu kumueleza madhaifu ya Mwalimu mkuu basi walimu wakajua moja kwa moja ni Mimi

Mambo yakawa moto walimu woote wakawa hawataki hata kuniona Darasa nililokuwepo wakalisusa ikawa tunakaa Hadi week bila kusoma kisa Mimi kuwa mnoko jamani wakati sijui chochote wala sihusiki na Chochote

Niliishi maisha Magumu Sana pale shule Soo hayo ndiyo yalinikuta nikiwa shule ingawa yapo mengi ila nimejaribu kusamulize.
Pole sana mkuu
 
Hili ni tatizo sana kiukweli, hizi shule kwa sasa zimekuwa biashara sana kuliko kuangalia na kutunza hawa watoto tunaowapelekea....

Mishahara kwa walimu ni midogo na hailipwi kwa wakati pamoja na wazazi kulipa ada kubwa.
Wafanyakazi wengine kama wafanya usafi, madereva nk hawalipwi vizuri na wanamaisha magumu mpaka inasikitisha..
Hayo yote yanashusha hali ya ufanyajikazi na matokeo yake uangalizi wa watoto unakuwa mdogo shuleni na maeneo yanayozunguka shule.

Mfumo wa kuajili wafanyakazi kwenye hizi shule unapaswa kuwekewa utaratibu mzuri ili kulinda watoto kwenye hizi shule..

Serikali inapaswa kufanya controlling kwenye hizi shule kwa kuwa na watu maalum wanaofanya ziara za mara kwa mara kujua mienendo ya kila siku....kama itatokea ukiukwaji wowote wa maadili na nidhamu mbovu kwenye shule hizi adhabu yake iwe kuubwa sana na mtoto yoyote aliyefanyiwa udhalilishaji shule husika ilipe fidia kubwa sana...
 
Kabisa kabisa mkuu.
 
wote huku mitaani tuwe wazazi wa hawa watoto huku mitaani, tuwalinde na kuwaongoza..

ukimlinda mtoto wa mwenzio badi ndio vile vile kwa uwezo wa mwenyezi Mungu wakwako atakuwa salama....

Walimu huko mashuleni pamoja na maslahi duni na stress za maisha, jitahidini kulinda hawa watoto InshaAllah mwenyezi Mungu atawapa malipo yake mazuri hapa duniani na akhera pia..

Malezi ya hawa watoto mashuleni kulingana na hizi nyakati yanahitaji umakini sana na ufuatiliaji wa kila hatua ya mtoto shuleni...
 
Wazazi majumbani tuwe na ufuatiliaji na ulinzi wa watoto kupitia ukaribu na walimu wao mashuleni hata kwa kuwapa vitip vya hapa na pale ili wawe macho na watoto angalau wanapokuwa hawana njaa....

Wazazi wenye watoto boarding msiwatelekeze hawa watoto, muwe mnafanya visiting za hapa na pale na kuwahoji watoto aina ya maisha pamoja na marafiki zao na hata kuwasoma saikolojia na miili yao, unapoona lolote geni kwa mtoto kuwa mkali hapo hapo na kuanza ufuatiliaji...

Kama hakuna ulazima saaana hakuna haja yakupeleka mtoto boarding, mlee mwenyewe awe anasoma day, boarding sio safe kwa watoto wetu hawa ambao wengi wao uelewa unakuja kuanzia miaka 10 na chini ya hapo kila kitu kwake ni sawa tu....

Vijana wengi wanamiliki watoto na familia lakini elimu hasa ya malezi na namna ya kulea mtoto kwao ni shida, matokeo yake mtoto au watoto wanajikuza wenyewe.....ni hatari sana.....Kama hujawa tayari kuzaa acha endelea kula ujana kuliko kuleta mtoto atakayeteseka....
 
Back
Top Bottom